Ukiona ujumbe unaosema "Faili ulilopakia ni byte sufuri," inamaanisha kuwa faili lako la sauti haliwezi kuchezwa. Wakati mwingine hii hutokea unapojaribu kupakia kwa kutumia kifaa cha mkononi, kama vile simu au hifadhi ya mtandaoni (cloud storage), kwa kuwa hifadhi ya faili inashughulikiwa tofauti na inavyokuwa kwa kompyuta iliyohifadhi faili husika. Utahitaji kusitisha jaribio la awali na kupakia upya toleo lako.
Ikiwa unapakia muziki wako kwa kutumia kifaa cha iOS, utahitaji kuhakikisha unachagua mafaili yako kutoka kwenye kivinjari cha faili cha iOS, vinginevyo unaweza kupata shida kupakia jalada la albamu yako au mafaili ya sauti, kama vile kuona ujumbe wa hitilafu ukisema kwamba " Faili uliyopakia ni byte sufuri."
Ukianzia kwenye Dashibodi yako ya DistroKid, chagua "Menyu", na kisha chagua "Pakia" ili kufika kwenye fomu ya kupakia.
Ukiwa kwenye fomu ya kupakia, jaza maelezo kwa kadri inavyohitajika. Unapofika sehemu ambayo unapakia mchoro, bofya kisanduku kinachosema "Chagua picha mpya". Kutoka hapa utapewa chaguo la kuchagua picha kutoka kwenye maktaba yako ya picha, kupiga picha, au kutafuta kwenye kivinjari cha faili cha kifaa chako cha iOS. Kwa wakati huu, ili kupakia mchoro wako kutoka kwenye kifaa cha iOS utahitaji kuchagua faili lako la mchoro kutoka kwenye kivinjari cha faili cha kifaa chako. Bofya "Browse".
Ukishachagua browse, utaletewa programu iliyopachikwa ya kutafuta Faili kwenye kifaa chako. Sasa unaweza kwenda mahali ambapo umehifadhi mafaili yako kwa ajili ya kupakiwa. Kwa kuangalia mfano huu, nimehifadhi faili langu la sauti na mchoro wa albamu kwenye folda la "Vipakuliwa" kwenye iPhone yangu.
Kutoka hapa, tunaweza kusonga chini kwenye fomu ya kupakia hadi tunapofika sehemu ambayo tutapakia faili la sauti. Ukifika sehemu ya "Faili la sauti" ya fomu ya kupakia, bofya "Chagua Faili". Utaletewa chaguzi tatu zilezile, na tena utahitaji kuchagua "Browse" ili kukupeleka kwenye kivinjari cha faili la iOS.
Ukishachagua faili lako la sauti, hapo unakuwa sawa kuendelea! Ukikumbana na changamoto, hakikisha kuwa unahifadhi mafaili yako kwenye kifaa chako cha iOS badala ya kuifadhi kwenye iCloud. Kwa sasa, fomu ya kupakia ya DistroKid haikubali upakiaji wa mafaili yaliyo kwenye hifadhi za mtandaoni, kwa hivyo utahitaji kupakia mafaili moja kwa moja kutoka kwenye kifaa chako cha iOS.
Sign Up