Majukumu ya msanii ni vitambulishi unavyoweza kutumia kuonesha huduma za utirishaji ni majukumu yepi msanii fulani alifanya katika utengenezaji au utumbuizaji wa toleo husika. Majukumu haya yanaweza kuonyeshwa katika ngazi ya wimbo au ya albamu. Huduma za Utiririshaji yanakubali majukumu yafuatayo ya msanii kutoka DistroKid:
Msanii wako wa Albamu
Msanii wa Albamu au "mtumbuizaji" ndiye msanii mkuu kwenye ngazi ya albamu. Kwa mfano, kwenye albamu ya Kendrick Lamarya DAMN., "Kendrick Lamar" ndiye Msanii wa albamu hii.
Msanii Mkuu
Msanii mkuu ni msanii muhimu zaidi katika ngazi ya wimbo. Mara nyingi hii hujumuisha Msanii wa Albamu pamoja na wasanii wengine wakuu kwenye wimbo. Jukumu la msanii mkuu hutumika kuonyesha ushirikiano. Kwa mfano kwenye albamu ya Moore Kismet ya Vendetta for Cupid, Moore Kismet ndiye Msanii wa Albamu katika ngazi ya albamu. Katika ngazi ya wimbo kwa wimbo kwenye albamu Rumor, WYN ni Msanii Mkuu wa ziada na Moore Kismet ni Msanii Mkuu.
Msanii aliyeshirikishwa
Msanii aliyeshirikishwa ni msanii yeyote anayesaidia katika uimbaji wa wimbo lakini si katika ngazi ya msingi kama ya msanii mkuu. Wasanii walioshirikishwa hujitokeza katika aya au kama wanavokali kwenye wimbo. Mfano, kwenye SOS (feat. Aloe Blacc) ya Avicii, "Aloe Blacc", ambaye anaimba kwenye wimbo huo, ni msanii anayeshirikishwa kwenye wimbo, ilhali "Avicii" ndiye Msanii Mkuu na wa Albamu.
Mtengeneza Remix
Msanii ambaye ametengeneza remix ya kazi asili. Mfano, kwa Love That Never (IMANU Remix) - TOKiMONSTA, "IMANU", ambaye alitengeneza remix ya wimbo huo, ndiye Mtengeneza Remix wa wimbo huu, ilhali "TOKiMONSTA", ambaye alikuwa msanii mkuu wa wimbo asili, bado ameorodheshwa kama msanii mkuu kwenye remix.
Mtayarishaji
Jukumu la mtayarishaji limebadilika zaidi na kukua katika miaka ya hivi punde, lakini kwa wakati huu, angalau katika Spotify, majukumu ya mtayarishaji msanii yameorodheshwa chini ya wachangiaji kwa wimbo. Kwa mfano, kwenye Buddy Holly - Weezer, "Ric Ocasek" ndiye mtayarishaji. Unaweza kuona waliochangia kwa utayarishaji kwa kubofya kitufe cha kulia kwenye kijipanya kwenye wimbo kwenye programu yako ya kompyuta na kuchagua "Onyesha Waliochangia"
Vidokezo vya kupakia!
Endapo una nyimbo chache kwenye toleo lako lenye wasanii wengi, lakini nyingi zimefanywa na msanii mmoja, tafadhali orodhesha tu msanii atakayeonekana katika kila wimbo katika Sehemu ya "Jina la Msanii/bendi". Hii itaashiria Msanii wako wa Albamu kwa toleo hilo. Kwa nyimbo zenye msanii zaidi ya mmoja, utaorodhesha wasanii wa ziada (Walioshirikishwa, Mtengeneza Remix, Msanii Mkuu wa Ziada) kwenye ngazi ya wimbo.
Ikiwa ushawahi kupakia kwenye DistroKid hapo awali, kisanduku cha kuingiza jina la Msanii/bendi kwenye fomu ya kupakia ya DistroKid kitakuwa na jina la msanii lililotumika mwisho kama chaguomsingi. Iwapo unataka kutumia jina tofauti la msanii (na una nafasi za wasanii zinazoweza kujazwa kwenye mpango wako), andika tu jina au majina ya msanii ambayo ungependa kutumia.
Sign Up