URI ni nini?
URI ni kifupi cha Uniform Resource Indicator. Kwa ufanisi ni kitambulisha upekee au sifa maalumu. Kwa upande wa Spotify, URI hutumika kuonesha Wasanii, Nyimbo, Albamu, Orodha za Nyimbo, Watunzi wa Nyimbo, Watumiaji na zaidi! Apple ina kionesha rasilimali sawa na hicho kinachoitwa Apple ID ambacho hufanya kazi kwa njia sawa.
Je, nazitumiaje URI?
Wasanii wanaweza kuhitaji URI/ vitambulisha raslimali kwa sababu mbalimbali. Kwa kutaja mifano michache, wakati mwingine blogu na vituo vya redio vinaweza kukuuliza URI ya wimbo wako wa singo yako mpya kabla ya tarehe ya kutolewa ili waweze kuiongeza kwenye orodha za nyimbo zao mara moja inapofikia tarehe ya kutolewa.
Zaidi ya hayo, URI za wasanii pia zinaweza kutumika katika maombi ya kuunganisha wasanii ili wasambazaji kama DistroKid waweze kuomba matoleo mahususi kuunganishwa kwenye ukurasa wako sahihi wa msanii.
Kwa njia hizi na nyinginezo zaidi, URI zinaweza kuwa muhimu katika kazi zako mwenyewe.
Je, nitapataje URI yangu?
Unaweza kutumia Viangalizi vyetu vya Spotify URI na Apple ID ! Unaweza kuvipata kwenye viungo vifuatavyo...
Kiangalizi cha URI ya Spotify https://distrokid.com/uri/spotify
Kiangalizi cha Apple ID: https://distrokid.com/uri/apple
...au kwa kuangalia viungo kwenye Menyu ya Vipengele ya DistroKid , chini ya sehemu ya Vizawadi. Bofya kwenye Menyu ya Vipengee kwenye kona ya juu kulia ya dashibodi yako ya DistroKid, kisha sogeza chini hadi sehemu ya Vizawadi na hatimae bofya menyu ya "Vinasaidia Vinapohitajika". Kutoka hapo utapata nyenzo za Kiangalizi!
Sign Up