Unaweza kuongeza michango ya Mtayarishaji wa Muziki kwenye matoleo yako wakati wowote kwa kutembelea ukurasa wako wa Waliochangia, hata kama toleo lako tayari lipo hewani madukani!
Ili kufanya hivyo, nenda tu kwenye ukurasa wa albamu wa toleo ambalo ungependa kuhariri. Bofya "Waliochangia"
Kutoka kwenye ukurasa wa waliochangia, bofya menyu kunjuzi "Ongeza Mpya..." na chagu "Mtayarishaji."
Baada ya kuchagua aina ya mchango wa Mtayarishaji, unaweza kuchagua aina maalumu ya mtayarishaji katika menyu kunjuzi ifuatayo. Baada ya kuchagua vipengele hivi, unaweza kwenda mbele na kuingiza jina la Mtayarishaji wako. Aidha, una hiari ya kuongeza ama kutoongeza barua pepe zao (barua pepe za watayarishaji hazitaonyeshwa kwenye huduma za utiririshaji).
Sign Up