Gurudumu la Orodha ya Nyimbo ni nyenzo ya kufurahisha ya kufanyia promosheni ambayo tuliitengeneza ili kuwapa wasanii fursa ya kufurahisha ya kuwekwa kwenye orodha yetu ya nyimbo ya Spotify! Unaweza kucheza mara moja kwa siku, ili kuonyeshwa hapa kwenye hii Orodha ya nyimbo ya Spotify.
Hivi ndivyo hufanya kazi:
Hatua ya Kwanza: Chagua wimbo uliopakia DistroKid ambao ungependa uwekwe kwenye orodha ya nyimbo
Hatua ya Pili: Bofya kitufe kikubwa cha "UNGANISHA NA SPOTIFY" baada ya kuchagua wimbo wako
Hatua ya Tatu: Mara ukishaunganisha akaunti yako ya Spotify, utaweza kuzungusha gurudumu kwa kubofya kitufe kikubwa cha "ZUNGUSHA GURUDUMU".
Unaweza kuzungusha gurudumu mara tatu na mzungusho wako bora kati ya hiyo mitatu utahifadhiwa kama namba yako ya nafasi kwenye orodha ya nyimbo! Kwa mfano, ikiwa mzungusho wako bora ulikuwa 23, basi utakuwa wimbo wa 23 kwenye orodha ya nyimbo.
Mara ukishamaliza mizungusho yako, utapata skrini ya uthibitisho kukueleza jinsi ulivyofanya!
Unaweza kucheza Gurudumu la Orodha ya Nyimbo mara moja kwa siku au, ikiwa mtu mwingine anazungusha namba sawa na wewe, unaweza kucheza mara tu ukishaondolewa kwenye orodha ya nyimbo.
Wimbo wako utasalia kwenye orodha ya nyimbo mradi tu hakuna mtu mwingine atakayezungusha na kupata nambari sawa na wewe.
Sign Up