Je, unaona upau mwekundu?
Ikiwa upao au ufito wa maendeleo unageuka kuwa mwekundu wakati wa kupakia albamu yako, inamaanisha kuna kitu hakipo sawa kwenye intaneti yako na kwahiyo itabidi uanze upya upakiaji.
Tuna uhakika hitilafu hiyo haipo upande wa DistroKid. Ili kuthibitisha hilo, hapa kuna machache kuhusu jinsi fomu yetu ya kupakia inavyofanya kazi, kiteknolojia:
Unapotembelea fomu ya kupakia ya DistroKid, teknolojia inayoitwa Cross Origin Resource Sharing (CORS) huunganisha moja kwa moja kivinjari chako na kituo cha kuhifadhi mafaili cha (Amazon S3) Tofauti na upakiaji wa kawaida unaohitaji seva ya kati, CORS hadi S3 huhakikisha mafaili hayagusi kamwe seva za DistroKid wakati wa kuingia. Hii inamaanisha kwamba upakiaji ni wa haraka sana, na uwezekano wa kutofaulu ni mdogo mno. Hata tukitaka kuuvunja, hatuwezi.
Ikiwa upakiaji wako unafeli, angalia muunganisho wa intaneti yako. Labda jaribu kupakia kutokea eneo lingine. Au jaribu tena baadaye.
Kupakia mafaili kubwa ni changamoto. DistroKid ina teknolojia nzuri sana ambayo hufanya upakiaji wa mafaili kubwa kuwa wa haraka na (kwa kawaida) bila hitilafu. Lakini ni mtandao, na mambo hayawi kamilifu kila wakati (ingawa tunajaribu!)
Kumbuka: Intaneti iliyounganishwa kwa nyaya ndiyo inapendekezwa, kwa kuwa ukatikaji wowote wa WiFi unaweza kusababisha matatizo wakati wa kupakia.
Sign Up