DistroKid inaweza kugawanya mapato kutoka kwenye wimbo au albamu yoyote, na kutuma mapato hayo kiotomatiki kwa watumiaji wengine wa DistroKid. Ongeza washirika wako, watayarishaji, wana bendi, mameneja na zaidi. Tutawalipa moja kwa moja, ili lisikusumbue akili. Ili kuanza, ingia katika DistroKid na bonyeza "Mgawanyo", au nenda kwenye ukurasa wa albamu unaotaka kusanidi mgawanyo - katikati ya ukurasa kutakuwa na chaguo la kuunda mgawanyo moja kwa moja kutoka kwenye ukurasa wa albamu yako.
Mambo mengine ya kufurahisha kuhusu Migawanyo:
- Unaweza kubadilisha mgawanyo wakati wowote.
- Unaweza kuongeza au kuondoa washirika wakati wowote.
- Unaweza kurudi nyuma na kuona migawanyiko yoyote ya awali.
- Kwa ajili ya faragha, washirika wanaweza tu kuona ni asilimia ngapi wanapata. Hawawezi kuona washirika wako wengine ni akina nani, au ni asilimia ngapi watu wengine wanapata.
- Matoleo yako hayatacheleweshwa emdapo mshirika wako anachelewa kujisajili. Badala yake, tutazizuilia pesa hadi wanajiunga.
- Ikiwa mshirika wako hatajiunga kamwe, unaweza kughairisha mwaliko wao kwa urahisi na mapato yaliyokuwa yametengwa kwa ajili yao yatarudi kwako.
Kumbuka: Kila mshirika atahitaji kuwa na akaunti ya DistroKid ili kupokea mapato yao. Ikiwa bado hawatumii DistroKid, watapata punguzo la 50% ili wajisajili! Ikiwa hawataki kujisajili, unaweza hata kulipia "Uanachama wa Split" ($10 kwa mwaka) kwenye akaunti yako, ili waweze kupokea mapato yako moja kwa moja na taarifa zote za kihasibu zinafanywa kiotomatiki kwa ajili yako!
Mgawo wa mapato aliotengewa mshirika wako utazuiliwa katika benki ya DistroKid hadi atakapokubali mwaliko wako. Akishakubali na kufungua akaunti, mapato yaliyozuiliwa yatawekwa katika Benki yake ndani ya saa 24.
Kwa maelezo ya haraka kuhusu jinsi ya kugawanya mapato, tazama video hii:
Sign Up