Ndiyo!
Endapo una mpango wa Musician Plus au Ultimate! unaweza kubainisha bei ya wimbo au albamu yako kwenye iTunes na Amazon.
Ikiwa hutabainisha bei yako (na kwa maduka ambayo sio iTunes/Amazon.com), muziki wako utauzwa kwa bei yoyote ambayo ni chaguomsingi (yaani default price) la maduka. Kwa mfano, wakati wa kuandika maelezo haya, singo ni senti 99 kwenye iTunes (unabaki na senti 70). Wewe na maduka wote mnataka kuuza muziki wako kwa wingi kadri iwezekanavyo. Kuruhusu maduka kubainisha bei kunaweza kukuletea mauzo makubwa na pesa nyingi.
Tafadhali kumbuka kwamba tutatuma bei zako ulizopanga kwa iTunes na Amazon, lakini wana chaguo la kubatilisha hili na kuweka bei yao wenyewe.
Huenda maduka kama iTunes yakaweka bei ya juu kwa singo ambazo zina urefu wa zaidi ya dakika 10.
Sign Up