Jibu fupi: Unaweza kubadilisha jina lako la msanii kwenye huduma zote isipokuwa iTunes/Apple Music kwa kutembelea ukurasa wa albamu yako, na kubofya "Hariri Toleo". Unaweza hata kuhariri jina lako la msanii kwenye matoleo yako yote kutoka kwenye ombi moja la kuhariri albamu!***
Jibu refu: Kubadilisha jina lako la msanii ni mchakato mrefu na mgumu ambao wakati mwingine unaweza kusababisha matatizo zaidi kuliko inavyotatua, na sio huduma zote zinaruhusu uwekaji upya wa chapa. Ni wazi, sote tunaelewa hisia za msanii na kutaka kujiwakilisha kwa usahihi zaidi na mradi wako wa msanii, lakini pia tunataka kuhakikisha kuwa unakuwa na taarifa zote unazohitaji ili kufanya uamuzi unaotokana na kuwa na ufahamu zaidi kwa kadri iwezekanavyo kabla ya kufanya mabadiliko kwenye miradi yako iliyopo ambayo itakuwa ni vigumu kubadili nia na inaweza kusababisha maswala mengi. Apple Music haikubali maombi ya kubadilisha chapa kwa sasa. Unaweza kupata maelezo zaidi juu ya hilo hapa.
Mambo ya kuzingatia:
-
Marekebisho ya jina la msanii na/au ya chapa yanaweza tu kuombwa kwenye matoleo ambayo yapo hewani kwa sasa
Huduma za utiririshaji haziruhusu matoleo ambayo tayari yamewasilishwa kuwasilishwa upya na metadata tofauti (Jina la Msanii na Majina ya Nyimbo). Ili kuwasilisha tena toleo lolote ambalo tayari limeorodheshwa katika huduma za utiririshaji, ni lazima liwasilishwe upya likiwa na Jina asili la Msanii na Majina ya Nyimbo.
Iwapo umefuta kazi yako kwa lengo la kuhariri au kubadilisha chapa ya Jina lako la Msanii, kumbuka kwamba, njia pekee ya kufanya hivyo, ni kupakia tena kazi yako na metadata za asili, kisha omba kuhaririwa kwenye hiyo kazi iliyopakiwa upya mara tu inapowasilishwa tena katika huduma za utiririshaji. -
Kuhifadhi wafuasi na wasikilizaji wa kila mwezi
Unapotuma ombi la kubadilisha jina lako la msanii, tafadhali kumbuka kwamba huduma nyingi za utiririshaji zitatengeneza ukurasa mpya wa msanii kwa ajili yako badala ya kusasisha maelezo ya kwenye ukurasa wako wa msanii uliopo. Kwa huduma za utiririshaji zinazofanya hivi, hatuwezi kuomba kwamba ukurasa wako wa msanii uliopo uhaririwe ili uendane jina lako jipya la msanii. Na matokeo yake, kuna uwezekano wasikilizaji na wafuasi wako wa kila mwezi wakashindwa kuhamishiwa kwenye ukurasa wako mpya wa msanii. -
Kuhifadhi idadi za kucheza na orodha za nyimbo
DistroKid haiwezi kutoa hakikisho lolote, lakini kwa ujumla ikiwa tu unahariri metadata ya toleo lililopo kupitia nyenzo yetu ya uhariri (yaani kutobadilisha ISRC), idadi yako ya mara ngapi wimbo ulisikilizwa na uwekaji wa orodha za nyimbo zinapaswa kuhamishwa. Lakini hata hivyo, sio jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wa DistroKid. -
Inaweza kuchukua muda kwa maduka yote kusasisha jina lako la msanii
Wakati uwasilishaji wa ombi lako la kutengeneza chapa mpya ni mchakato wa kiotomatiki, usimamizi halisi wa data na masasisho ya metadata ya ombi lako la kutengeneza chapa mpya; hayajakamilika kiotomatiki, na mengi ya maombi haya yanahitaji wanadamu (sio kompyuta) kuyakamilisha ipasavyo.
Hii inamaanisha nini:
Kutegemea na idadi iliyopo ya maombi ya kubadilisha chapa, inaweza kuchukua hadi wiki kadhaa kwa maduka yote kusasisha maudhui yako yaliyopo na kuonyesha jina lako jipya la msanii. Ikiwa unapanga kubadilisha chapa yako, tafadhali kumbuka hili.
-
Matoleo yasiyolingana
Kama unavyojua, DistroKid haina udhibiti wa mahali matoleo yako yametolewa kwenye huduma za utiririshaji. Ukihariri jina lako la msanii na ukurasa mpya wa msanii ukatengenezwa, matoleo yako yanaweza kugawiwa kwa ukurasa uliopo wa msanii ikiwa jina lako jipya sio la kipekee. Hilo likitokea, tafadhali tembelea https://www.distrokid.com/fixer, ambapo tutakuelekeza ili kuhakikisha mambo yanarekebishwa! -
Haiwezi kutuma maombi ya ziada ya kuhariri
Ukiamua kubadilisha jina lako la msanii katika huduma zote za utiririshaji, hutaweza kuwasilisha maombi zaidi ya kuhariri kwenye toleo lolote ambalo linatumia jina jipya la msanii uliloweka hadi ombi lako la kubadilisha jina likamilishwe. Kwa wakati huu, hakuna njia ya kuharakisha maombi haya -
Hakuna kurudi nyuma (ni kama)
Ukichagua kubadilisha jina lako la msanii, njia pekee ya kurejesha mabadiliko ni kuomba upya uhariri mwingine. Madhara yoyote ya ombi la awali hayatoi hakikisho la kutatuliwa kwa kubadilisha tu jina lako la msanii. (Ni uamuzi mkubwa!) đź§
***Ni muhimu kutambua kwamba wakati wa kubadilisha jina, kazi zako zote lazima zifanyiwe marekebisho ili ziendane na jina jipya la msanii, vinginevyo baadhi ya huduma za utiririshaji zinaweza kuficha matoleo yanayoonekana kuwa na metadata zinayokinzana.
Njia bora: Sasisha jina lako la msanii kwa matoleo yako yote kwa kutumia "Sasisha matoleo yangu yote kutoka kwa [Jina la Msanii] ili kutumia nyenzo mpya ya jina la msanii" katika sehemu ya hariri toleo. Kumbuka kuwa nyenzo hii inapatikana tu kwa matoleo yenye msanii mkuu mmoja (sio ushirikiano).
Sign Up