DistroKid Spotlight ni shindano, kama vile mashindano ya rap au mashindano ya bendi, ambapo nyimbo hushindanishwa na wasikilizaji wanaweza kupigia kura nyimbo wapendazo. Washindi hupata nafasi kwenye orodha maalumu ya DistroKid Spotify playlist, baadhi zimekaribia wafuasi 200,000! Ili kupata nafasi ya kushinda,, yeyote anaweza kupiga kura — sio wanachama wa DistroKid pekee (hakuna usajili unaohitajika ili kupiga kura).
Hivi ndivyo hufanya kazi:
- Kwanza, nenda kwenye https://distrokid.com/spotlight/submit/ ili kuwasilisha wimbo wako.
- Chagua msanii ambaye ungependa kumwasilisha kwa Playlist Spotlight (unaweza kuwasilisha wimbo mmoja kwa msanii kwenye akaunti yako)
- Chagua wimbo unaotaka kuuwasilisha (nyimbo zitakazoonyeshwa hapa ni zile tu ambazo kwa sasa zipo hewani Spotify)
- Chagua Muda wa Kuanza wa Kipande cha Video (ni sekunde 29 zinazosisimua zaidi)
- Bofya kitufe cha "CONNECT WITH SPOTIFY" ili kuunganisha na Spotify na kufuata orodha za nyimbo za Spotlight.
Ili kutazama takwimu zako, shirikisha nyimbo na mashabiki wako, au futa wimbo wako nenda kwenye https://distrokid.com/spotlight/me/ na kutoka hapo unaweza kutazama kila wimbo uliowasilisha kwa ajili ya wasanii wako, kupata kiungo cha kusambaza kwa mashabiki, au kuondoa wimbo (bofya tu ondoa karibu na ikoni la taka chini ya wimbo)
Je, unashindaje?
Mara wimbo wako unapowasilishwa, utapata kiungo cha kutuma kwa mashabiki wako ili kupiga kura kwa ajili ya wimbo wako. Nyimbo zenye kura nyingi zaidi kila wiki zitawekwa kwenye DistroKid Spotify playlist! Hutajua ni kura ngapi umepokea, lakini hakuna kiasi kilichowekwa unachohitaji, kwa hivyo utataka kusambaza na kukitangaza kiungo kwa mashabiki wako ili kupata kura nyingi uwezavyo!
Hizi ni baadhi tu ya orodha za nyimbo ambazo una nafasi ya kuwekwa, angalia zingine hapa.
Sheria:
- Wasanii wanaweza kuwasilisha (au kuondoa) wimbo wakati wowote
- Wimbo mmoja tu kwa msanii ndio unaweza kuwa kwenye shindano kwa wakati mmoja
- Hakuna ukomo wa mara ngapi wimbo unaweza kuongezwa kwenye orodha za nyimbo
- Kura zinazofanana kutoka kwa mtu mmoja zitaondolewa wakati kura zinapolinganishwa
- Orodha za nyimbo husasishwa kila wiki na kura huwekwa upya hadi sufuri
- Nyimbo zenye kura nyingi zaidi zitaongezwa kwenye orodha ya nyimbo za DistroKid Spotify
Kwa maelezo zaidi juu ya Sheria za DistroKid Spotlight, bofya hapa. Tunaboresha orodha za nyimbo kila wiki, kwa hivyo endelea kuangalia ili kuona ikiwa wimbo wako umechaguliwa! Bahati njema!
Sign Up