Tunaelewa sana suala hilo: unaweza kuwa umeweka kila kitu sawa kabisa kwenye toleo lako, lakini tarehe ya kutolewa inapowadia, unagundua kuwa muziki wako umewekwa kwenye wasifu wa msanii mwingine. 😱😭
Hii ni mojawapo ya mambo yanayotatiza sana ambayo wasanii hupitia kwenye ulimwengu wa kisasa wa huduma za utiririshaji. Ingawa DistroKid imeweka zana kadhaa ili kujaribu kuunganisha ukurasa wa msanii kwa usahihi katika jaribio la kwanza, hatimaye miunganisho sio jambo ambalo msambazaji wako ana udhibiti wa moja kwa moja kwa sababu ni jambo linaloshughulikiwa na huduma.
KUTOKANA NA HAYO, DistroKid PIA imetengeneza zana kadhaa za kukusadia kuthibitisha muziki wako upo kwenye ukurasa sahihi baada ya kuuwasilisha.
Ili kuangalia ni wasifu upi ambao toleo lako litaunganishwa siku ya kutolewa kabla ya tarehe yako ya kutolewa, unaweza kuomba URI zako au Apple IDs kwa kutumia Spotify URI na Apple ID yaani Looker Upper Tools! Unaweza kuzipata zana hizi kwenye viungo vifuatavyo...
Kiangalizi cha URI ya Spotify https://distrokid.com/uri/spotify
Kiangalizi cha Apple ID: https://distrokid.com/uri/apple
Hebu tujaribu kwa kutumia Kiangalizi cha URI ya Spotify. Kwanza nenda kwenye https://distrokid.com/uri/spotify. Kisha, chagua toleo lako kutoka kwenye menyu kunjuzi. Nina toleo moja pekee kwenye akaunti hii kwa hivyo tayari limeshachaguliwa. Kumbuka kwamba ikiwa huoni toleo, inawezekana bado hatujaliwasilisha Spotify, tafadhali angalia tena kesho!
Baada ya kuwa umechagua toleo lako, endelea na bofya kitufe cha "Spotify URI ni nini". Ikiwa toleo lako tayari limeshachukuliwa na Spotify, unapaswa kuona albamu yako, wimbo na URI za msanii
Ikiwa una wasanii wengi kwenye toleo lako unalojaribu kuthibitisha wanaelekea kwenye wasifu sahihi, ondoa shaka! Wasifu wote wa wasanii na majukumu yao vitaorodheshwa chini ya sehemu ya "Msanii:". Angalia!
Endapo toleo lako bado halijachukuliwa na Spotify, kuna uwezekano utakutana na skrini hii:
Ondoa shaka! Kwa ujumla huchukua siku moja au zaidi kwa Spotify kuyachukua matoleo. Maelezo ya URI yako yatapatikana siku inayofuata au zaidi!
Kama hivyo ndivyo, angalia tena siku chache zijazo. Spotify itakuwa imeliingiza toleo lako na litapatikana kwa maombi ya URI kwenye ukurasa huu.
Mara unapoona URI za msanii / Apple ID kwa kutumia zana za kuangalia, hakikisha wasifu hizo za wasanii zinafanana na wasifu zako zilizopo kwenye maduka. Unaweza kufanya hivyo kwa kufuata URL zilizotolewa kwenye kurasa za kiangalizi, au kwa kuingiza URI moja kwa moja kwenye kitafutaji cha Spotify.
Ikiwa wasifu zako zinafanana, woohoo!! Kila kitu kimeunganishwa kwa usahihi, na uwe tayari kwa ajili ya siku ya kutolewa toleo husika.
Ikiwa havijaunganishwa ipasavyo, unaweza kutembelea https://distrokid.com/fixer ili kuwasilisha ombi la kutengeneza ukurasa mpya ikiwa inahitajika, au hamishia kazi yako kwenye ukurasa wako uliopo ikiwa huduma zilishindwa. Kwa maelezo zaidi kuhusu Zana yetu ya Kurekebisha, bofya hapa.
Sign Up