Katika makala hii tutashuka chini sehemu kwa sehemu tukionyesha maelezo yoyote unayoweza kuyahitaji kuhusu fomu ya kupakia ya DistroKid!
Huduma
Sehemu hii ndiyo unaweza kuchagua ni huduma zipi ambazo toleo lako litawekwa hewani! Je, unataka muziki wako uende kwenye huduma mahususi pekee? Hakuna shida! Teua tu visanduku vilivyo kando ya huduma unazotaka na ondoa tiki kwenye visanduku vya huduma usizotaka.
Bofya hapa kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zipi muziki wako utawasilishwa.
Idadi ya nyimbo
Katika sehemu hii, unaweza kuchagua idadi ya nyimbo kwenye toleo hili unazotarajia kupakia. Ukichagua wimbo mmoja, utakuwa unapakia singo. Idadi nyingine yoyote zaidi ya wimbo mmoja na toleo lako liko katika eneo la EP / Albamu.
Angalia makala hii kwa maelezo zaidi kuhusu tofauti kati ya Singo, EP na Albamu.
Imewahi Kutolewa?
Katika sehemu hii, unabainisha iwapo toleo lilishawahi kusambazwa hapo kabla au hapana. Chaguo lako katika swali hili litaamua ikiwa unaweza kuchagua tarehe ya kutolewa iliyopita au ijayo. Ukichagua kuwa upakiaji wako haujawahi kutolewa hapo kabla, na una mpango wa Musician Plus au wa juu zaidi, utaweza pia kuchagua kujiunga na kuweka Oda ya Mapema kwenye huduma zinazoikubali.
Angalia makala hii kwa maelezo zaidi.
Tarehe rasmi ya kutolewa
Ikiwa ulichagua Ndiyo chini ya"Imewahi Kutolewa?”, basi hii ndio sehemu ambayo unaweza kuonyesha tarehe rasmi ya kutolewa kazi yako. Ikiwa toleo lako lilitoka kabla ya 1920, sijui jinsi ya kukusaidia rafiki. 😉
Jina la msanii/bendi
Muhimu zaidi: kisanduku hiki cha maandishi ndipo unapoingiza jina la msanii (wasanii) Mkuu wa toleo. Msanii Mkuu au "mtumbuizaji" ndiye msanii muhimu katika kiwango cha albamu. Msanii (Wasanii) mkuu ataorodheshwa kwenye kila wimbo kwenye albamu.
Ili kujifunza zaidi kuhusu Majukumu ya Msanii, tembelea makala hii hapa ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara .
Je, msanii tayari yupo Spotify?
Katika sehemu hii unaweza kuonesha kwa DistroKid ikiwa tayari una profaili ya msanii katika Spotify kwa ajili ya jina la Msanii wako Mkuu au la. Ikiwa tayari una jina la kisanii katika Spotify, unaweza kutumia sehemu hii kubainisha ukurasa wako wa msanii.
Ikiwa huna jina la msanii lililokuwepo tangu awali katika Spotify, unaweza kuchagua kutengeneza ukurasa mpya wa msanii kwa ajili ya toleo lako jipya.
Kwa maelezo zaidi kuhusu unavyoweza kupata Profaili ya Msanii wa Spotify iliyodhibitishwa, angalia Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara makala.
Je, msanii tayari yupo kwenye Apple Music?
Sawa na hapo juu, ukiingiza msanii mkuu mmoja tu katika kiwango cha albamu, utaona sehemu ya "Msanii tayari yupo kwenye Apple Music?". Ikiwa tayari una jina la msanii katika Apple Music, unaweza kutumia sehemu hii kuashiria ukurasa wako wa msanii.
Ikiwa huna jina la msanii lililokuwepo hapo awali katika Apple Music, unaweza kuchagua kutengeneza ukurasa mpya wa msanii kwa ajili ya toleo lako jipya.
Ili kupata ukurasa wako wa Msanii wa Apple Music kwa matoleo yoyote ambayo umepakia kupitia DistroKid, angalia makala hii.
Tarehe ya kutolewa
Sehemu ya tarehe ya kutoa ya fomu ya kupakia ndipo unapoonyesha ni wakati gani ungependa toleo lako liende hewani katika huduma. Ikiwa huna mpango wa Musician Plus au mpango wa juu zaidi, hutaweza kuchagua tarehe ya kutolewa kwa siku zijazo. Unaweza kutembelea https://distrokid.com/plan ili ujipandishe.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kuchagua tarehe yako ya kutoa, angalia makala hii.
Kuagiza mapema?
Katika sehemu hii, unaweza kuchagua kama ungependa toleo lako liweze Kuagizwa Mapema au hapana kwa huduma zinazokubali. Utahitaji mpango wa Musician Plus au zaidi ili uweze kutumia Kuagiza Mapema. Angalia makala hii kwa maelezo zaidi.
Lebo ya Kurekodi
Ikiwa una mpango wa Musician Plus au mpango wa juuu zaidi, unaweza kuweka Lebo ya Kurekodi maalumu kwenye sehemu hii.
Jalada la albamu
Katika sehemu hii, unaweza kuchagua mchoro unaotaka kupakia. Kwa kawaida, faili la .jpg la pixel 3000x3000 huwa ndilo bora zaidi, lakini tunakubali aina nyingi zaidi za mafaili pia! Tazama makala hii kwa maelezo zaidi kuhusu kuuweka mchoro wa albamu yako uwe sawa.
Jina la albamu
Ikiwa toleo lako lina zaidi ya wimbo 1 basi utahitaji kuingiza jina la Albamu. Usitumie jina la msanii mwingine yeyote au chapa ya biashara katika jina la albamu yako.
Bei ya albamu
Ikiwa una mpango wa Musician Plus au mpango wa juu zaidi, unaweza kuonyesha bei maalumu ya albamu katika sehemu hii. Ikiwa toleo lako lina zaidi ya wimbo 1, basi katika sehemu hii unaweza kuweka bei ya albamu kwenye iTunes na Amazon, unaweza kuchagua kuanzia $1.99 hadi $14.99, lakini kama bei ya kununua traki zote moja moja ipo chini kuliko bei ya albamu iliyobainishwa hapa, maduka yatatumia jumla ya bei za nyimbo kama bei ya albamu.
Lugha
Katika sehemu hii, unaweza kuchagua lugha kuu iliyotumika kwenye toleo. Lugha inayochaguliwa hapa lazima iwe sawa na lugha iliyotumika kwa majina ya nyimbo.
Aina kuu
Hapa unaweza kuchagua aina ya toleo lako. Orodha yetu ya aina ya muziki inajumuisha aina zote zinazokubaliwa na huduma zote tunazosambazia, kwa hivyo aina yako mahususi inaweza kukosekana. Hiyo ni sawa! Chagua tu aina ambayo inakaribiana na toleo lako. Huduma huwa na upangaji wao wenyewe wa aina ya muziki 🙂.
Aina ya Pili
Ikiwa aina moja haifafanui vya kutosha aina ya muziki wako, habari njema! Unaweza kuongeza aina nyingine tofauti! Orodha hii ya aina za muziki ni sawa na orodha ya aina kuu, kwa hivyo chagua tu aina nyingine ambayo pia inaendana na mradi wako.
TRAKI [#]
Jina la wimbo
Katika sehemu hii unaonyesha jina la toleo - Jina TU. Maelezo ya toleo na wasanii wa ziada vitaongezwa katika sehemu za baadaye za menyu ya traki.
Maelezo kwenye mabano yanakubalika, mradi tu ni sehemu ya jina na hayatumiki kuonyesha msanii wa ziada au maelezo ya toleo.
✅ Good Riddance (Time of your Life)
❌ I Can’t Sleep (feat. Iann Dior)
✅ I Can’t Sleep
❌ Scary Monsters and Nice Sprites (Noisia Remix)
✅ Scary Monsters and Nice Sprites
Ungependa kuongeza msanii aliyeshirikishwa kwenye jina la wimbo?
Kwa singo, unaweza tu kuongeza Watengeneza Remix au Wasanii Walioshirikishwa chini ya hii sehemu. Ikiwa singo yako ni ushirikiano kati ya wasanii wawili, tafadhali onyesha wasanii wawili katika sehemu ya "Jina la msanii/bendi" iliyopo juu ya fomu ya kupakia.
Kwa toleo lililo na zaidi ya wimbo mmoja, utakuwa pia na chaguo la "Msanii mkuu wa ziada"
Ikiwa unahitaji kuongeza zaidi ya msanii mmoja wa ziada kwenye wimbo wako, bofya tu kitufe cha "Ongeza msanii mwingine aliyeshirikishwa".
Kwenye menyu kunjuzi unaweza kuchagua Mtengeneza Remix, Msanii Aliyeshirikishwa, au Msanii mkuu wa ziada. Ukishachagua aina ya msanii wa ziada, tafadhali onyesha jina la msanii. Usiwe na shaka kuhusu kurasa zao za wasanii ambazo tayari zipo katika Apple na Spotify, tutashughulikia hilo katika sehemu ya Kuunganisha Msanii hapo baadaye. 🙂
Ungependa kuongeza maelezo ya "toleo" kwenye jina la wimbo?
Sehemu hii inaweza kutumika kuonyesha maelezo yoyote ya toleo kwenye mabano. Matoleo ya kawaida ni pamoja na:
-
Hewani
-
Kiakustiki
-
Toleo la Redio
-
Remix
-
Remix ya [Mtengeneza Remix]
-
Remix ya [Aina]
Faili la sauti
Tukio kuu!! Hapa ndipo utaweza kuchagua faili la sauti la wimbo wako. Angalia makala hii kwa maelezo zaidi kuhusu aina za mafaili ya sauti yanayokubalika.
Dolby Atmos/Spatial audio
Katika sehemu hii, unaweza kupakia mchanganyiko wako wa Sauti ya Dolby Atmos/Spatial ya wimbo wako. Ikiwa hufahamu lolote kuhusu hii ni nini, kwa ufupi:
Dolby Atmos ni hisia nzuri sana ya usikilizaji wa stereo unaopatikana kwenye Apple Music, TIDAL na Amazon. Angalia makala hii kwa habari zaidi juu ya Dolby Atmos na makala hii kuhusu jinsi ya kutengeneza mchanganyiko wako wa Dolby Atmos.
Mtunzi wa nyimbo
Katika sehemu hii utaonyesha ikiwa wimbo huo ni wimbo asili au wimbo wa kava.
Jina halisi la mtunzi (watunzi) wa wimbo (nyimbo)
Kwa nyimbo asili, utahitaji kuorodhesha jina halisi la mtunzi(watunzi), kwa maelezo zaidi angalia makala hii.
Wimbo wa Kava
Iwapo umeonyesha kuwa wimbo wako ni kava basi utahitaji kukagua maelezo ya wimbo wa kava, kuongeza maelezo ya jina la msanii Halisi na jina la wimbo, na pia onyesha kuwa wimbo huo hausampuli au kuchanganya rekodi za msanii mwingine (inahitajika).
Mistari yenye lugha chafu
Ikiwa toleo lako lina mistari chafu utahitaji kuonyesha hivyo katika sehemu hii.
Je, hili ni "toleo la redio"?
Iwapo umeubainisha kwamba wimbo wako hauna mistari chafu basi kwenye sehemu hii utaombwa kuonyesha iwapo wimbo ni safi, na umekuwa hivyo wakati wote au kama kuna toleo chafu la wimbo huu, na hili ndilo toleo safi (au lililokaguliwa)
Ala Pekee
Katika sehemu hii unaweza kuonyesha ikiwa wimbo wako una mistari au ni ala pekee
Apple Digital Master?
Katika sehemu hii unaweza kuonyesha ikiwa toleo lako limeboreshwa na Mastering House iliyoidhinishwa ya Apple Digital Mastering. Kwa habari zaidi, bofya hapa.
Muda wa kuanza kipande cha wimbo
Katika sehemu hii unaweza kutafsinisha (yaani kufanya ikidhi mahitaji yako) sehemu ya nyimbo zako ambazo ungependa zipatikane katika maonyesho ya duka! Chagua tu "Sehemu nzuri inapoanzia" ili kubainisha ni sehemu ipi ya wimbo wako unayotaka ipatikane kwa ajili ya onyesho katika TikTok, Apple Music na iTunes.
Kumbuka kuwa ubadilishaji wa muda wa kipande cha wimbo kitakachoonyeshwa unapatikana tu kwa nyimbo zenye urefu wa zaidi ya 1:16.
Bei ya Wimbo
Ikiwa una mpango wa Musician Plus au wa juu zaidi, unaweza kuonyesha bei maalum ya wimbo katika sehemu hii ya iTunes na Amazon. Unaweza kuchagua $0.69, $0.99, au $1.29, kumbuka tu kwamba nyimbo za muda wa zaidi ya dakika 10 zitakuwa na bei ya juu zaidi.
Rudia hatua hizi kwa kila wimbo kwenye toleo lako hadi uwe umepakia zote. Karibu kumaliza!
KUUNGANISHA MSANII
Katika sehemu hii unaweza kuhakikisha wasanii wote wanaunganishwa ipasavyo katika huduma za utiririshaji. Ikiwa wasanii wako hawa kurasa za msanii tayari, unaweza kuchagua tu "Ruhusu huduma za utiririshaji ziamue". Ikiwa wasanii wako tayari wana kurasa za wasanii pale Spotify na Apple Music, unaweza kuzibanisha kwa kuchagua "[Jina la Msanii]" tayari ana ukurasa katika Spotify au Apple ambao ningependa kubainisha…"
Kutoka hapo, unaweza kuonyesha URI ya Spotify na Apple Artist URL za wasanii wako.
VYA ZIADA (SI LAZIMA LAKINI VYAPENDEZA)
Sehemu ya Vya Ziada hukuruhusu kuongeza vipengele vya hiari kwenye toleo lako.
Kwa maelezo zaidi kuhusu vya ziada kimoja kimoja vilivyopo na bei zake, bofya hapa.
VISANDUKU MUHIMU VYA KUCHAGUA (LAZIMA)
Sehemu ya mwisho ni Visanduku Muhimu vya Kuteua (Lazima). Unahitajika kukamilisha sehemu hii ili kutuma toleo lako kwa huduma.
Unaweza kuangalia Masharti ya Huduma na Makubaliano ya Usambazaji ya DistroKid hapa.
Hapa ndio mwisho! Bofya Imekamilika na toleo lako litatumwa kwa huduma ulizochagua. Hongera!!
Sign Up