Kwenye programu ya Spotify ya simu
- Bonyeza kwenye "Now Playing View" kwenye wimbo.
- Unaposikiliza, telezesha kidole juu kutoka chini ya skrini.
- Utaona mistari ya nyimbo inayosonga muda sawa na wimbo ukichezwa!
- Ili kusambaza, bonyeza tu kitufe cha "Sambaza" chini ya skrini ya mistari na kisha chagua
mistari unayotaka kusambaza--na pahali unapotaka kuisambaza-kupitia majukwaa ya wahusika wa upande wa tatu.
Kwenye programu ya Spotify ya kompyuta
- Ukiwa kwenye eneo la "Now Playing", bonyeza kwenye ikoni ya maikrofoni wakati wimbo unacheza.
- Tazama! Utaiona mistari ya nyimbo inayosonga muda huo huo wakati wimbo unapocheza.
Kwenye programu ya SpotifyTV
- Fungua "Now Playing View" kwenye wimbo.
- Nenda kwenye kona ya kulia hadi kwenye "Mistari" na chagua ikiwa ungependa kuwezesha Mistari.
- Mara baada ya kuwezeshwa, utaaona mistari katika Mwonekano wa "Inayocheza Sasa".
Unaweza kuangalia Makala ya Spotify kuhusu Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara juu ya hili hapa: https://support.spotify.com/us/article/lyrics/
Sign Up