Ikiwa hukumbuki nenosiri lako la DistroKid na unahitaji kuweka jingine, unaweza kutumia nyenzo yetu ya kuweka nenosiri upya kutuma barua pepe kwa anwani ya barua pepe inayohusiana na akaunti yako ambayo itakuruhusu kuweka upya nenosiri.
Maombi ya Kuweka Upya Nenosiri
Hizi hapa chini ni hatua za kuomba barua pepe ya kuweka upya nenosiri ikiwa hukumbuki nenosiri lako la sasa.
- Hakikisha unaondoka katika akaunti ya DistroKid. (Bofya hapa, au bofya picha yako ya wasifu iliyo upande wa juu kulia, kisha bofya "Ondoka" ili kuondoka kwenye akunti)
- Nenda pale distrokid.com kisha bofya "Ingia" upande wa juu kulia, kisha bofya "Umesahau nenosiri lako?"
- Weka barua pepe uliyotumia wakati wa kujiunga na DistroKid, na tutakutumia barua pepe yenye hatua za kuweka upya nenosiri lako
Kuweka upya Nenosiri Ukiwa Umeingia kwa Akaunti
Ikiwa unataka kuweka upya nenosiri lako lakini unakumbuka nenosiri la sasa, unaweza kubadilisha nenosiri lako kupitia akaunti yako ya DistroKid. Ili kufanya hivyo, ingia kwenye akaunti yako ya DistroKid ukitumia nenosiri la sasa, kisha bofya aikoni ya wasifu wako upande wa juu kulia, bofya "Akaunti," kisha bofya "Badilisha nenosiri langu."
Ikiwa Hujui Anwani Yako ya Barua Pepe ya Akaunti
Ikiwa hujui anwani ya barua pepe inayohusiana na akaunti yako na unahitaji usaidizi kuingia, tujulishe kwa kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi.
Sign Up