iTunes Match ni huduma ambapo mashabiki wa muziki hulipa Apple ili kuweza kupakia muziki wao wote kwenye hifadhi ya mtandaoni ya Apple (Apple cloud) na kuutiririsha kutoka Apple cloud kwa kutumia kifaa chochote. Wanaweza hata kupakia na kutiririsha muziki ambao hawakununua kutoka iTunes.
Kisha, wasanii kama wewe hulipwa kila wakati mmoja wa wasajiliwa hawa wa iTunes Match wanapotiririsha mojawapo ya nyimbo zako.
Kuna sababu mbili za kwa nini iTunes Match ni nzuri kwa wasanii:
- Wasanii wanalipwa kila wakati shabiki anapotiririsha wimbo wao, hata kama shabiki tayari alishanunua wimbo huo. Katika hali hii, msanii analipwa mara mbili (mara moja kwa kupakua, mara moja kwa mtiririsho).
- Endapo shabiki alipakua wimbo wako kinyume na sheria au kupitia njia zingine ambapo hakulipia, msanii bado analipwa kila wakati wimbo huo unatiririshwa na mteja wa iTunes Match.
Sign Up