Kabla ya kujumuisha muziki wako kwa nyongeza ya albamu ya Kifurushi cha Mitandao ya Kijamii, lazima kwanza ubaini ikiwa unatimiza masharti ya YouTube Content ID. Ikiwa toleo lako lina sauti yoyote ambayo hukutengeneza mwenyewe kama vile midundo, vipande vinavyojirudia, sampuli au sauti za michezo ya video, basi kwa bahati mbaya halitakidhi masharti ya YouTube Content ID.
YouTube inachukua hili kwa uzito sana. Yote yafuatayo lazima yawe kweli ili toleo likidhi vigezo:
- Ulitengeneza sauti zote.
- Toleo lako HALIFAI kuwa na midundo, vipande vinayojirudia, madoido ya sauti, au sauti yoyote kutoka kwa sampuli za maktaba au rasilimali za umma, pamoja na sauti za bila malipo kutoka GarageBand, Ableton, Logic au Fruity Loops.
- Hutaruhusu wasanii wengine kufanya remix ya nyimbo zako au kutumia sauti zozote kutoka kwa nyimbo hizo. Ikiwa remix itapakiwa kwenye YouTube, Content ID inaweza kudai kuwa ni yako kimakosa, au kinyume chake ikiwa mtengeneza remix anatumia Content ID.
- Toleo lako HALINA rekodi au nyimbo zisizolindwa na sheria ya hakimiliki.
- Toleo lako HALINA sauti kutoka kwa michezo ya video, televisheni, filamu, au rasilimali zingine za maudhui.
- Toleo lako HALINA sauti yoyote kutoka kwa video za watu wengine kwenye YouTube.
- Wewe ndiye mtu pekee aliye na jukumu la kuwasilisha singo hii kwa YouTube Content ID. Ili kuepuka mkanganyiko, hakuna mtu mwingine, hata wanachama wa bendi au watayarishaji wa muziki, anapaswa kujaribu kufanya hivyo.
- HUJATUMIA kampuni nyingine, kama vile TuneCore au CD Baby, kuwasilisha singo hii kwa YouTube Content ID. Hii itasababisha mzozo.
Sign Up