DistroKid na Twitch wameshirikiana ili kuwapa wasanii wa DistroKid wenye sifa fursa zaidi za kukuza jumuiya zao na kupata pesa kutokana na muziki. Utiririshaji kwenye Twitch huwaruhusu wasanii kuchangamana moja kwa moja na mashabiki wao katika hali ya kuwa pamoja hewani ambayo haipatikani kwingine.
Kupitia ushirikiano wetu, wasanii wa DistroKid wana fursa ya kuzingatiwa kujiunga na The Collective. Wasanii wanaochaguliwa na Twitch kwa ajili ya programu watapata usaidizi endelevu kutoka Twitch, na kustahiki mpango wa ugunduzi uliopewa kipaumbele, promosheni, na amsha amsha kutoka Twitch, Discord na washirika wengine wa tasnia.
Twitch ina taarifa zote unazohitaji ili kwenda hewani, kujenga jumuiya yako na kupata pesa kwa kufanya kile unachopenda.
Tuma maombi ya kujiunga na The Collective leo!
Vidokezo: Kwa sasa, mpango huu upo wazi kwa wasanii wanaoishi Marekani au Kanada pekee na ambao wana umri wa miaka 18+.
Je, unahitaji usaidizi zaidi? Jiunge na Jumuiya ya Twitch Music Assist kwenye Discord kwa ushauri kutoka kwa watengenezaji muziki wa Twitch kuhusu maunzingumu, yaani hardware, programu na kupangalia chaneli yako.
Sign Up