Katika YouTube, chaneli ya mada ni chaneli ambayo huzalishwa kiotomatiki na YouTube inapopokea muziki wa msanii kutoka kwa msambazaji, kama vile DistroKid. Kila msanii anayewasilisha muziki kwa YouTube kupitia msambazaji anakuwa na chaneli ya mada, na inafanya kazi bila kutegemea chaneli zingine za wasanii ambazo tayari zipo YouTube.
Huenda ukadhani kuwa DistroKid iliunda chaneli ya mada unayoiona, lakini sivyo! Ni njia ya YouTube ya kushughulikia muziki tunaotuma kwao na kuhakikisha kuwa unapatikana kusikilizwa katika YouTube na YouTube Music.
Chaneli za mada zinaruhusu muziki wako kuonekana kwenye YouTube Music, ambayo ni huduma ya kutiririsha muziki ya YouTube. Endapo unataka matoleo yako ya YouTube Music yapatikane kwenye chaneli yako ya msanii pamoja na chaneli ya mada, itakulazimu uombe chaneli yako (inayojulikana pia kama Owned and Operated Channel) igeuzwe kuwa Official Artist Channel (OAC).
Je, Nitaingizaje Chaneli ya Mada Iliyopo kwenye Fomu ya Kupakia?
Ikiwa tayari una ukurasa wa msanii kwenye YouTube Music, weka URL ya ukurasa huo wa YouTube Artist katika sehemu ya YouTube Music ya fomu ya kupakia.
Ikiwa huna wasifu uliopo wa YouTube Music, chagua tu "Hapana - [Jina la Msanii] bado hana wasifu wa msanii kwenye YouTube Music", na tutakuombea ukurasa mpya.
Muziki Wangu uko kwenye Ukurasa wa Msanii Mwingine Kimakosa katika YouTube
Ikiwa muziki wako uliwasilishwa kwa ukurasa wa msanii mwingine kimakosa katika YouTube, unaweza kutumia Nyenzo yetu ya Kirekebishaji kuwasilisha ombi la kutuma matoleo yoyote yaliyo kwenye ukurasa wa msanii usio sahihi yawekwe kwenye ukurasa sahihi wa msanii, au hata kuomba ukurasa mpya wa msanii ikihitajika.
Je, Ninaweza Kufuta Chaneli ya Mada?
Kwa kuwa chaneli za mada zinaundwa na kusimamiwa na YouTube, DistroKid haiwezi kusaidia kuzifuta. Hata hivyo, ikiwa hutaki muziki wako kuonekana katika chaneli ya mada au katika YouTube Music, unaweza kuamua kuondoa matoleo yako kwenye YouTube Music, au kuunda Official Artist Channel.
Unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi ili kuondoa muziki wako kwenye YouTube Music. Pindi muziki wako unapoondolewa kwenye YouTube Music, hautaonekana katika chaneli yoyote ya mada, na pia hautaonekana katika jukwaa la YouTube Music.
Halikadhalika, ikiwa una chaneli yako ya YouTube inayotumika kwa muziki wako, unaweza kuomba ibadilishwe kuwa Official Artist Channel. Kufanya hivyo kutaunganisha chaneli yako ya mada kwenye chaneli yako, na muziki uliowasilisha kwa YouTube kupitia DistroKid utapatikana kutoka kwa Official Artist Channel. Kwa maelezo zaidi kuhusu kupata Official Artist Channel, tafadhali tazama makala haya: https://support.distrokid.com/hc/sw/articles/360036924633.
Sign Up