Unapotuma muziki Facebook/Instagram kupitia DistroKid, matoleo yako yanapaswa kuwa tu na sauti ambazo umetengeneza mwenyewe. Vinginevyo, hazistahiki kutumwa Facebook au Instagram na zinaweza kuondolewa.
Kwa habari zaidi, angalia nakala ya Facebook hapa: https://www.facebook.com/business/help/585591922881993
Sauti Tofauti
Sauti ya toleo lako lazima iwe tofauti vya kutosha ili istahiki kwa Facebook na Instagram. Sauti ambazo zinaweza kukosa kuwa tofauti vya kutosha ni kama:
• Sehemu zinazojirudia za uzalishaji
• Msingi wa Sauti
• Madoido ya sauti
• Sauti zinazofanana
• Rekodi za karaoke
• Rekodi za muziki wa Classical zisizolindwa na sheria ya hatimiliki
• Muziki wa filamu
• Taamuli (yaani meditation), Yoga, au muziki wa kulala
• Seti za DJ au Mix endelevu
Maudhui ya Muziki
Toleo lako lazima pia liwe maudhui ya muziki. Matoleo ambayo huenda yasichukuliwe kama maudhui ya muziki ni pamoja na:
• Rekodi za mashairi ya kusemwa
• Rekodi za ucheshi
• Rekodi za filamu (mbali na muziki wa filamu hiyo)
• Hotuba
• Rekodi za maombi
• Audiobooks
• Podikasti
• Rekodi za mazingira asili au wanyamapori
• Rekodi za sauti za mazingira
• Rekodi au maelezo ya vitendo vya ngono
Sign Up