Kuna sababu kadhaa zinazoweza kufanya upakiaji wa video kufeli, ikiwa ni pamoja na kodeki au aina za faili zisizokubaliwa. Hata hivyo, sababu ya kawaida zaidi ambayo husababisha hitilafu au kushindwa kwa upakiaji wa video ni muunganisho duni wa intaneti.
Ikiwezekana tunapendekeza kutumia intanet ya nyaya badala ya Wi-Fi, kwa sababu mafaili ya video kwa kawaida ni makubwa sana kuliko upakiaji wa mafaili ya sauti, na upotevu wowote wa pakiti au kukatika kwa intanet (hata kwa sekunde chache) kunaweza kuleta hitilafu ya upakiaji. Unaweza pia kutaka kujaribu kufuta hifadhi muda na vidakuzi vya kivinjari chako kabla ya kupakia.
Aidha, kwa kawaida huwa tunaona hitilafu kwenye vipakizi ambavyo havikidhi mahitaji ya kiufundi ya faili ambazo huduma zinahitaji. Upakiaji wowote ambao hautumii aina ya faili ya video, kodeki iliyobanwa au vipimo vinavyokubalika inaweza kusababisha hitilafu.
Kwa orodha kamili ya aina za mafaili ya video inayokubalika, kodeki na vipimo, angalia makala haya kuhusu vigezo vya faili za video.
Ikiwa una muunganisho imara wa intaneti na faili lako la video linakidhi mahitaji yote ya kiufundi, lakini bado unakabiliwa na matatizo ya kupakia, tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi. Wakati wote tunafurahi kusaidia kutatua matatizo yoyote ya kupakia video unayokumbana nayo.
Sign Up