Tafadhali kumbuka: ikiwa unatumia sampuli zisizotoza na mirabaha, muziki wako hautakuwa na sifa za Nyongeza ya Albamu ya Social Media Pack.
Misingi
Je, wewe ni mgeni kwenye DistroKid? Je, ungependa kufahamu nini cha kufanya na nini cha kutofanya katika usambazaji wa kidijitali? Tuna majibu kwako!
DistroKid See all 14 articles
-
DistroKid ni nini?
DistroKid ni huduma ya usambazaji wa muziki kidijitali ambayo wanamuziki hutumia kuweka muziki kwenye maduka ya mtandaoni na huduma za utiririshaji. Hizi ni pamoja na iTunes, Spotify, Apple Music, YouTube Music, Amazon, Deezer, TIDAL, na nyingi zaidi.
DistroKid hukusanya mapato na malipo, na kutuma 100% ya mapato haya kwa wasanii, ukiondoa ada za benki/kodi zinazotumika.Baadhi ya faida nyingi utakazopata katika DistroKid:
- Mgawanyo wa mapato kiotomatiki - tuambie tu nani wa kumlipa, na ni kiasi gani cha kuwalipa. Tutafanya mengine.
- HyperFollow - ndani ya dakika chache baada ya kupakia muziki wako, utapata ukurasa wa kutangaza muziki wako uliohifadhiwa mapema. Toleo lako likishaenda hewani kwenye huduma zote za utiririshaji, tutaongeza viungo kiotomatiki kwenye ukurasa huo.
- Usaidizi wa mistari - ongeza mistari kwenye nyimbo zako, na tutazituma kwenye huduma za utirishashaji kwa niaba yako.
- Muda wa tarehe za kutoa ulimwenguni - toleo lako litaenda hewani wakati huo huo kila mahali kwenye Spotify
-
Na zaidi - Bofya kwenye Menyu ya Vipengele vya DistroKid
sehemu ya juu kulia, kisha nenda kwenye sehemu ya Vizawadi ili kuviona vyote mara tu unapojisajili!
-
Inagharimu Kiasi Gani?
DistroKid inatoa mipango mingi, kuanzia mpango wa msanii/bendi moja, hadi mipango ya Ultimate kwa hadi wasanii 100.
Ili kuona ni mpango upi wa malipo kwa Wanamuziki na Lebo ambao DistroKid inatoa, unaweza kujisajili au kuingia na kutembelea https://distrokid.com/plan.
Kwa watumiaji waliopo, ikiwa utahitaji nafasi zaidi au vipengele, wakati wote unaweza kupandisha malipo yako kutoka kwa dashibodi yako pia.
Kwa maelezo kuhusu nyongeza za hiari za Albamu za DistroKid, tafadhali angalia makala ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara hapa hapa.
DistroKid pia hutoa idadi kubwa ya (nyingi bila malipo!
) nyenzo na huduma ambazo tunadhani utazipenda!
Ili kuona nyenzo zote nzuri unazoweza kutumia, ingia kwenye DistroKid na ubonyeze menyu ya Vipengele vya DistroKid
na kisha tembeza hadi sehemu ya Vizawadi - na usome zaidi hapa.
-
Ni Huduma na Maduka Yapi Ambako Muziki Wangu Utaonekana?
Unaweza kubainisha muziki wako kuonekana katika baadhi ya huduma au huduma zote kati ya hizi zifuatazo:
- Spotify
- Apple Music
- iTunes
- Instagram & Facebook
-
TikTok
- Luna
- Capcut - YouTube Music
- Amazon.com
- Pandora - Kwa habari zaidi, bofya HAPA
- Deezer
- TIDAL
- iHeartRadio
- ClaroMusica
- Saavn
- Anghami
- Boomplay
- Snapchat - Maelezo zaidi HAPA
- NetEase
-
Tencent, ambayo hujumuisha huduma zifuatazo:
- QQ Music
- Kugou Music
- Kuwo Music
- WeSing
- Pretzel - Beta, Maelezo zaidi HAPA
- TouchTunes - Maelezo zaidi HAPA
- Audiomack - Maelezo zaidi HAPA
- Qobuz
- Joox - Maelezo zaidi HAPA
- Kuack Media Group - Beta, Maelezo zaidi HAPA
- Pamoja na maduka mengi madogo kupitia MediaNet, kama vile Dubset.
Endapo kuna huduma zingine za utiririshaji ambazo ungependa kuzitumia, tujulishe na tutazingatia kuziongeza! -
Vizawadi vya DistroKid: Zaidi ya Usambazaji
DistroKid inajulikana vizuri kwa kuwa njia ya haraka na rahisi zaidi ya kufikisha muziki wako kwenye huduma za utiririshaji na kupokea 100% ya mapato yako.
Lakini wanachama wa DistroKid pia wana ufikiaji mkubwa sana wa (nyingi ni bure!
) nyenzo na huduma ambazo tunadhani utazipenda!
Ingia kwenye DistroKid na bonyeza menyu ya Vipengele vya DistroKid
sehemu ya juu ya skrini ili kufikia Vizawadi - na usome zaidi hapa chini kwa habari kuhusu kila kipengele mahususi:
Pata Kusikika Sasa Hivi
-
Playlister - Taarifa za mawasiliano kwa wamiliki wa orodha ya nyimbo ya Spotify. (Ultimate pekee)
-
Slaps.com - Mtandao wa kijamii kwa wanamuziki, ulioboreshwa kwa mwingiliano mkubwa.
-
Playlist Spotlight - Pigiwa kura kwenye Orodha za aina ya muziki za DistroKid.
- Gurudumu la Orodha ya Nyimbo - Zungusha gurudumu ili uwekwe katika orodha yetu ya nyimbo zilizopo Spotify.
Jitangaze mwenyewe
-
HyperFollow - Kiungo kimoja kinacholeta pamoja vingine vyote! HyperFollow ni njia isiyo na malipo na rahisi ya kutengeneza kurasa zinazoonyesha muziki wako, video, viungo vya mitandao ya kijamii na zaidi.
-
Video Fupi - Video unazopata bila malipo, fupi zilizotanafsishwa (ili kukidhi mahitaji yako) ili kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
- Kadi za Matangazo - Makumi ya picha za bila malipo, zilizotanafsishwa (ili kukidhi mahitaji yako) hapohapo unazoweza kutumia kutangaza matoleo yako mapya mtandaoni.
Ufikiaji Maalum
-
Ufikiaji wa papo hapo wa Spotify for Artists - Spotify for Artists huwasaidia wasanii kunufaika zaidi na Spotify. Simamia profaili yako ya msanii, jifunze kuhusu wasikilizaji wako, na shirikisha maoni kwa timu ya Spotify.
-
Ufikiaji wa Papo Hapo wa Apple Music for Artists - Apple Music for Artists itakusaidia kuelewa vyema athari za muziki wako kwenye Apple Music na iTunes. Tambua hatua kubwa ambazo muziki umepiga na muziki bora katika historia. Fahamu wasikilizaji wako ni akina nani na wapi wanakopatikana. Pakia picha na wasifu wako wa umma wa msanii.
- TIDAL Artist Home - Jipatie wasifu wako wa msanii na yafanye maelezo muhimu yakidhi mahitaji yako; na malezo hayo ni kama vile picha ya wasifu wako, maelezo ya wasifu, na viungo vya kijamii. Unaweza pia kuripoti maudhui yasiyo sahihi moja kwa moja kwa TIDAL ndani ya sekunde chache, kuwaalika wanachama wa timu na kupata fursa ya kila kitu ambacho TIDAL hutengeneza kwa ajili ya wasanii katika siku zijazo.
- YouTube Official Artist Channel ("OAC") - Official Artist Channels zinaundwa ili kuwasaidia wasanii na timu zao kunufaika zaidi na YouTube. Pandisha chaneli yako leo ili uweze kuona takwimu na nyenzo ambazo zitakusaidia kuwasiliana na mamilioni ya mashabiki na kusimamia kwa ubora uwepo wako kwenye jukwaa.
-
Audiomack Connect - Unganisha na akaunti yako ya Audiomack na pakia muziki moja kwa moja kutokea DistroKid. Ili kujifunza zaidi kuhusu kupakia muziki kwenye Audiomack, tembelea Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara.
-
Twitch - Tuma maombi ya kujiunga na programu ya Twitch incubator ambayo huwasaidia wasanii kukua na kupata pesa moja kwa moja kutoka kwa mashabiki waliopo Twitch.
- Ufuatiliaji wa RIAA kwenye Gold na Platinum - Tuache tuangalie ikiwa muziki wako unakustahiki kupata cheti cha RIAA Gold au Platinum. (Ultimate pekee)
Boresha Muziki Wako
- Spotify Canvas Generator - Tengeneza video tanafsi(yaani zinazokidhi mahitaji yako) na za bila malipo za Canvas kwa ajili ya toleo lako Spotify.
-
Mistari - Ongeza mistari yako katika huduma za utiririshaji na injini za kutafuta. Ukishaweka maneno ya wimbo, unaweza pia kuongeza mistari iliyooanishwa na muda kwa ajili ya Instagram, Spotify, TIDAL na zaidi kwa kuchagua kuingia kwa Lyric Blaster.
-
Waliochangia & Maelezo ya Jalada - Wasilisha majina ya waliochangia, watunzi wa nyimbo, watayarishaji, wanamuziki, wahandisi na zaidi.
- Dave - Dave ni roboti yetu ya kiotomatiki ya A.I. ambaye atachambua muziki wako. Mjaribu!
Linda muziki wako
-
DistroLock - Linda muziki wako dhidi ya utolewaji usioidhinishwa.
- Hifadhi Salama - Uhifadhi bila malipo wa idadi yoyote wa kila kitu ambacho umewahi kupakia kwenye DistroKid. Inajumuisha mafaili ya sauti, michoro, UPC, ISRC na zaidi.
Vinasaidia Vinapohitajika
-
Mapya Kuhusu Miunganisho - Huduma za kutiririsha wakati mwingine huwaweka pamoja wasanii walio na majina sawa (au yanayofanana), au hutengeneza ukurasa mpya wa msanii badala ya kutumia ukurasa wako uliopo. Habari njema ni kwamba, tumeunda kitu cha kusuluisha shida hii haswa!
-
Kiangalizi cha URI ya Spotify - Pata URI yako ya Msanii/Albamu/Wimbo wa Spotify
-
Kiangalizi cha Apple ID - Chukua ID yako ya Msanii/Albamu/Wimbo wa Apple kwa toleo lolote ambalo umepakia.
- YouTube Allowlist - Kama ulichagua YouTube Content ID lakini unataka kuondoa madai kutoka kwenye video yoyote mahususi, unaweza kuongeza kwenye Allowlist, yaani orodha inayoruhisiwa hapa.
DistroKid mara kwa mara hutoa vipengele vipya vya kufurahisha na vilivyo muhimu kwa wanachama wa DistroKid, kwa hivyo hakikisha unaangalia menyu ya "Goodies" mara kwa mara!
Go to article -
Playlister - Taarifa za mawasiliano kwa wamiliki wa orodha ya nyimbo ya Spotify. (Ultimate pekee)
-
Ni Vipengele Vipi Zinapatikana katika kila Mpango?
Vipengele Musician Musician Plus Ultimate! Pakia nyimbo bila kikomo
✔️ ✔️ ✔️ Pakia mashairi bila kikomo
✔️ ✔️ ✔️ Tiki ya Spotify ya uthibitisho
✔️ ✔️ ✔️ Pokea mapato kutoka kwenye mgawanyo wa mirabaha
✔️ ✔️ ✔️ Takwimu za utiririshaji za kila siku
❌ ✔️ ✔️ Jina la lebo linaloweza kubinafsishwa
❌ ✔️ ✔️ Tarehe ya kutolewa inayoweza kubinafsishwa
❌ ✔️ ✔️ Tarehe ya kuagiza mapema inayoweza kubinafsishwa
❌ ✔️ ✔️ Bei ya iTunes inayoweza kubinafsishwa
❌ ✔️ ✔️ Misimbo ya ISRC inayoweza kubinafsishwa
❌ ✔️ ✔️ Wasanii au bendi 2
❌ ✔️ ✔️ Wasanii au bendi 5–100
❌
❌
✔️ Nafasi ya 1 TB ya Instant Share
❌
❌
✔️ Ufikiaji wa Playlister
❌
❌
✔️ Ufuatiliaji wa Tuzo za RIAA
❌
❌
✔️ -
Je, DistroKid ina Bidhaa?
Ndiyo!
Kofia, Mashati, Sweta, Vikata Kucha, hata Kitabu cha Mtoto!
Iangalie na ujinyakulie bidhaa hapa.
Kitabu Chetu cha Watoto, Music Production ABCs, kinaweza kununuliwa hapa!
Usambazaji See all 25 articles
-
Inachukua Muda Gani kwa Albamu Yangu Kupatikana Kwenye Huduma za Utiririshaji?
Inaweza kuchukua siku kadhaa kwa albamu kukaguliwa, kuidhinishwa na kutumwa kwenye huduma za utiririshaji. Endapo ni muhimu kwa albamu yako kwenda hewani katika tarehe mahususi, bofya hapa kusoma kuhusu tarehe za kutolewa. Vinginevyo, kimsingi, toleo lako linapaswa kuenda hewani mara tu inapoongezwa kwenye huduma za utiririshaji kulingana na ratiba ngumu hapa chini.
- iTunes/Apple Music: siku 1-7. Asilimia ndogo sana ya albamu kwenye Apple hupitia ukaguzi unaofanywa na watu halisi, ukaguzi ambao huchukua wiki za ziada 1-2 au zaidi.
- Spotify: siku 2-5
- Amazon: siku 1-2
- YouTube Music: siku 1-2
- Deezer: siku 1-2
- TIDAL: Siku 2
- Facebook/Instagram: Wiki 1-2
- TikTok: siku 1-2
- Anghami: siku 1-5 (baadhi zinahitaji ukaguzi unaofanywa na watu halisi kutoka timu ya Anghami; ukaguzi ambao unaweza kuchukua siku za ziada 2-3).
Ikiwa unapakia wimbo wa kava, kupata leseni za nyimbo za kava inaweza kuchukua hadi siku 14 za kazi. Matoleo yenye nyimbo za kava yatawasilishwa mara leseni itakapoidhinishwa na Harry Fox Agency (ambao hushughulikia leseni zetu za kava).
Kumbuka: Ucheleweshaji ni nadra, lakini hutokea, na kwa kawaida ni jambo lililo nje ya uwezo wa moja kwa moja wa DistroKid.
Pandora ina mchakato wao wa ukaguzi wa ndani ili kuratibu maudhui, kwa hivyo hatuwezi kutoa maelezo mengi sana kuhusu muda ambao unaweza kuchukua matoleo kuongezwa kwenye vituo vya Pandora (ikiwa imeongezwa). Ili kujumuishwa katika Pandora Premium (huduma ya utiririshaji ya redio ya Pandora), tafadhali soma HAYA.
Bonasi: Kwa huduma nyingi za utiririshaji (iTunes, Amazon, Spotify, na zaidi) tutagundua pindi tu albamu yako inapoenda hewani, na kukutumia barua pepe iliyo na kiungo!
-
Muziki Wangu Utapatikana Katika Nchi Zipi?
Nyimbo nyingi zinazopakiwa huonekana ulimwenguni kote katika kila nchi ambako huduma tofauti za utiririshaji zimeidhinishwa. Ikiwa unataka kuzuia toleo lako kwenye baadhi ya nchi, unaweza kupakia kwenye DistroKid, kisha tunaweza kuwasilisha sasisho la metadata kwa huduma za utiririshaji ili kuondoa nchi ambayo au ambazo hutaki kuwamo. Ili hili lifanyike, ni bora kwako kupakia angalau siku 10-14 kabla ya tarehe iliyopangwa kutolewa kazi yako (Mpango wa Musician Plus/Ultimate unahitajika kwa hili kufanyika).
Baadhi ya matoleo yanaweza yasisambazwe kwa nchi zote kutokana na lugha, maudhui ya lugha chafu, utoaji leseni na masuala mengine mbalimbali ambayo yako nje ya uwezo wa DistroKid.
Kwa sasa, Saavn ina sehemu isiyo ya Kihindi pekee ya katalogi yao inayopatikana katika nchi chache: India, Pakistan, Nepal, Sri Lanka, na Bhutan. Kwingineko ulimwenguni, ni maudhui ya Kihindi pekee ndiyo yanapatikana kwa wakati huu.
Katalogi ya kimataifa ya Anghami inapatikana Mashariki ya Kati pekee. Kwingine ulimwenguni, ni maudhui ya Kiarabu pekee ndiyo yanapatikana kwa wakati huu.
YouTube Music kwa sasa inapatikana Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uhispania, Italia, Urusi, Kanada, Norway, Ayalandi, Ufini, Uswidi, Australia, New Zealand, Mexico na Korea Kusini na itapatikana popote ambako YouTube itakuwa na huduma ya kulipia utiririshaji muziki kadri maeneo mapya yanavyotumia huduma. Endapo unajaribu kucheza video za YouTube Music Art Track nje ya maeneo haya, unaweza kupokea ujumbe ukisema kuwa maudhui hayapatikani.
Go to article -
Je, Naweza Kutumia Sampuli Zisizotoza Mrabaha?
Ni sawa kabisa kutumia sampuli zisizotoza mirabaha kutoka huduma za maktaba ya sampuli kama vile Splice, Sounds, LoopCloud n.k. Aidha, ni sawa kutumia sampuli zisizo na mrabaha ambazo zimejumuishwa kama maktaba za sampuli ambazo ni chaguo-msingi katika DAW yako.
-
Je, Naweza kupakia DJ Mixes au remix kwenye DistroKid?
Haiwezekani kupakia nyimbo za sampuli (yaani sample) hadi upate ruhusa toka kwa wote wanaohusika na nyimbo hizo.
Unakaribishwa kupakia remix ambazo umefanya mwenyewe. Hata hivyo, endapo remix yako ni wimbo wa msanii mwingine au ina baadhi ya vipande vya muziki asili wa msanii mwingine, huduma za utiririshaji zitahitaji ruhusa kutoka kwa msanii asili.
Kama unafanyia remix wimbo wako mwenyewe...
...Huna haja ya kujitaja kama mtengenezaji wa remix (yaani remixer) husika. Unaweza tu kuongeza "Remix" kama maelezo ya toleo. Hivi ndivyo unavyofanya kwenye fomu ya kupakia:
Chini ya sehemu Ungependa kuongeza maelezo ya "toleo" kwenye jina la wimbo?, orodhesha maelezo ya toleo linalofaa. Katika hali hii, tunaweza kuchagua "Nyingine" na kuandika tu "Remix"
Chini ya kifungu kinachosema Onyesho la jina la wimbo: unapaswa kuona kitu kama hiki:
YourSongTitle (Remix)
Ikiwa unapakia remix za wimbo wako mwenyewe toka kwa msanii mfanya remix...
...Utahitaji tu kuongeza mshirika mwenye jukumu la "Remixer", hakuna haja yakuongeza maelezo ya toleo. Hivi ndivyo unavyofanya hilo kwenye fomu ya kupakia:
Chini ya sehemu Ongeza msanii aliyeshirikishwa kwenye jina la wimbo, tafadhali onyesha "Ndiyo" kisha chagua jukumu la msanii. Kakatika hali hii, jukumu la msanii ni "Remixer." Tafadhali kisha ingiza jina la msanii aliyefanya remix katika kisanduku kilicho karibu na jukumu la msanii.
Tazama makala hii kwa mchanganuo wa majukumu ya msanii!
Chini ya kifungu kinachosema Onyesho la jina la wimbo: unapaswa kuona kitu kama hiki:
YourSongTitle (RemixingArtist Remix)
Kama unapakia remix ya muziki wa msanii mwingine...
...Lazima upate ruhusa ya kufanya hivyo kutoka kwa msanii husika.
Iwapo una ruhusa kutoka kwa msanii asili ya kupakia remix yako inayotokana na wimbo wao, utahitaji kuorodhesha jina la msanii asili katika sehemu ya "Jina la Msanii/bendi" ya fomu ya kupakia. Kumbuka kuwa hii itatumia nafasi ya ziada ya msanii. Ikiwa unahitaji nafasi zaidi za wasanii unaweza pandisha hapa.
Katika kiwango cha wimbo, utahitaji kuongeza jina la msanii wako na jukumu la "Remixer". Hivi ndivyo unavyofanya hilo kwenye fomu ya kupakia:
Chini ya sehemu Ongeza msanii aliyeshirikishwa kwenye jina la wimbo, tafadhali onyesha "Ndiyo" na kisha chagua jukumu la msanii. Katika hili "Remixer" ndilo jukumu la msanii. Tafadhali kisha ingiza jina la msanii aliyefanya remix (katika hili jina lako la msanii) kwenye kisanduku kando ya jukumu la msanii.
Tazama makala hii kwa mchanganuo wa majukumu ya msanii!
Chini ya kifungu kinachosema Onyesho la jina la wimbo: unapaswa kuona kitu kama hiki:
OriginalSongTitle (YourArtistName Remix)
Katika sehemu ya Mtunzi wa Nyimbo, usichague wimbo wa kava -- Remix sio kava.
-
Je, Naweza Kupakia Nyimbo za Kava?
Ndiyo! DistroKid hurahisisha kusambaza nyimbo zako za kava. Tutashughulikia kila kitu kwa niaba yako, ikiwemo kutuma malipo kwa watunzi wa nyimbo na kushughulikia mahitaji yote ya ziada ya kisheria.
Kumbuka: Kwa maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya kupakia kazi zisizolindwa na sheria ya hakimiliki, tafadhali angalia makala ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara hapa.
Wimbo unaoutengenezea kava lazima ukidhi mahitaji haya ya hakimiliki (hili ni jambo la kisheria, si jambo la DistroKid):
✅ Wimbo unaorekodi kava yake tayari umetolewa nchini Marekani
✅ Wimbo wako hauna sampuli na sio remix
❌ Wimbo wako haupaswi kuwa na sauti usiyomiliki (kutoka kwa TV, filamu, mitandao ya kijamii, michezo ya video, nyimbo zingine, n.k).
❌ Wimbo wako haubadilishi kimsingi maneno ya asili, wimbo au mada.
✅ Mabadiliko ya aina muziki na ya urembo ni sawa kabisa (na yanapendekezwa)!
✅Mifano zaidi ya nyimbo ambazo ZINAWEZA kupata leseni:
- Wimbo ambao ulitolewa wakati fulani kwenye iTunes na/au Amazon MP3.
- Wimbo uliotolewa kwa vifaa chache vya vinyl vinavyoweza kununuliwa katika duka la rekodi nchini Marekani
- Wimbo ambao uliwekwa upatikane kwa ajili ya kupakuliwa kumtangaza msanii kwenye tovuti yake
Pia kuna vikwazo vichache unapaswa kujua:
❌ Kusampuli pengine si sawa
Kusampuli ni pale unapotumia rekodi halisi iliyoimbwa na msanii mwingine. Kwa mfano, ukiitumia rekodi ya 1971 ya Led Zeppelin inayoitwa "When The Levee Breaks" kama ngoma kwa wimbo wako. Hiyo kwa ujumla hairuhusiwi, pengine kama una ruhusa kutoka kwa msanii mwenyewe.
❌ Remix pengine si sawa
Remix ya muziki wa msanii mwingine ni tofauti na kava. Kava ni endapo uliucheza wimbo huo mwenyewe. Kwa upande mwingine, remix inahitaji ruhusa ya msanii asili wa wimbo na ni kitu tofauti kabisa.
❌Mifano mingine ya nyimbo ambazo HAZIWEZI kupata leseni:
- Wimbo ambao ulitumika katika muziki wa filamu, lakini wenyewe haukutolewa kando na muziki wa filamu
- Wimbo ambao ulionekana katika mchezo wa video, lakini wenyewe haukutolewa kando na muziki wa mchezo
- Wimbo ambao ulitolewa kama sehemu ya mkusanyiko wa CD, lakini katika nchi fulani ambayo haikuwa Marekani
- Wimbo wa kitamaduni wa zamani ambao sasa hailindwi na sheria ya hatimiliki
- Medleys, mashups, n.k.
Ada
DistroKid hutoza ada ya $1 kwa mwezi (hulipwa kwa mwaka, hivyo $12 hutozwa kwenye kadi yako ya mkopo) ili kuusimamia wimbo huu wa Kava kwa niaba yako. Tutafanya:
- Kuchukua leseni
- Kulipa mtunzi (watunzi) asilia wa wimbo kila mwezi
- Kufanya mambo tuliyoyaelezea hapa na hapa
Malipo ya kiotomatiki kwa watunzi wa nyimbo
DistroKid itaondoa kiotomatiki ada inayotakiwa kisheria ya 9.1¢ kwa kila wimbo unaouzwa Marekani kutokana na mapato yako na uitume kwa HFA, ambao huituma kwa mtunzi asilia. Utapata 100% ya baki.
DistroKid itachukua leseni kwa niaba yako kupitia mchuuzi mwingine
leseni za kimakanika za lazima za DistroKid zinalindwa na Harry Fox Agency ("HFA"). Kulingana na sheria ya hakimiliki ya Marekani, leseni za nyimbo za kava hutoa ulinzi wa kisheria ikiwa wimbo halisi tayari umetolewa Marekani, na vipengele vikuu vya wimbo asilia (mistari asilia ya wimbo, tuni na jina la wimbo) havitabadilishwa katika rekodi mpya ya sauti. Mabadiliko ya aina ya muziki na madoido ni sawa kabisa na yanahamasishwa kufanywa. Mabadiliko ya lugha pengine si sawa. Ikiwa huna uhakika endapo kava yako inaruhusiwa au hapana, tafadhali angalia Maswali na Majibu katika Harry Fox Agency (hapa) na hakikisha kuwa unapakia tu zile kava zinazoweza kulindwa na leseni za lazima za kimakanika. Kanuni hizi ni suala la hakimiliki, sio suala la DistroKid (au la HFA) na huwaathiri wasambazaji na watoaji leseni wote. Matoleo yaliyo na nyimbo za kava hayawezi kuuzwa nchini India, Pakistani, Mexico au Kanada.
Lazima ununue leseni ya kava ya DistroKid kila unapopakia wimbo wa kava kwenye DistroKid. Kwa mfano, ukipakia wimbo huo wa kava mara mbili, unahitaji kuchagua chaguo la "Wimbo wa Kava" kwa kila upakiaji, hivyo kununua leseni mbili. Hivyo ndivyo mfumo wetu unavyofahamu kukata sehemu ya mapato ya mtunzi kutoka kwenye mapato yako (kwa upakiaji wote wa wimbo huo, katika mfano huu). Zaidi ya hayo, leseni za DistroKid zinatumika tu kwa maudhui yanayosambazwa moja kwa moja na DistroKid, na hayawezi kutumika kwa madhumuni yoyote nje ya DistroKid.
Ni wajibu wako kuhakikisha kuwa wimbo wako utasimamiwa chini ya leseni ya kimekanika ya lazima.
Sisi sio wanasheria na hatuwezi kutoa ushauri wa kisheria. Tafadhali kumbuka kuwa sheria ya hakimiliki ya Marekani hairuhusu kazi zilizozalishwa kutoka kwa kazi nyingine kama vile tafsiri za mistari inayolindwa na sheria ya hakimiliki kutoka kwa lugha asilia. Chini ya sheria ya hakimiliki ya Marekani, leseni za kava (pia huitwa "leseni za lazima") hutoa ulinzi tu ikiwa vipengele kuu vya wimbo, maneno ya wimbo asilia na melodia, havibadilishwi kwenye rekodi mpya ya sauti. Hili ni suala la hakimiliki na linaathiri wasambazaji wote, sio DistroKid pekee.
Tafadhali usijumuishe jina la msanii asili kwenye kichwa cha wimbo. Kwa mfano,
KICHWA SAHIHI KWA WIMBO
Enter Sandman
KICHWA KISICHO SAHIHI KWA WIMBO
Enter Sandman (awali ilifanywa na Metallica)
Enter Sandman na Metallica
Kwa maelezo zaidi kuhusu kununua leseni za kava kwa nyimbo kupitia DistroKid, tafadhali tazama makala hii.Tafadhali Kumbuka: Kupata leseni za nyimbo za kava inaweza kuchukua hadi siku 14 za kazi. Matoleo yenye nyimbo za kava yatawasilishwa pindi tu leseni itakapoidhinishwa na huduma yetu ya kivyake ya kutoa leseni.
Tazama video hii fupi kwa habari zaidi!
-
Je, Naweza Kupakia Sound-a-like?
Hapana, samahani.
Sound-a-likes--au matoleo ya kava, au nyimbo za heshima ambazo husikika sawa na za msanii mwingine--hazikubaliwi na huduma za utiririshaji.
Huduma za utiririshaji zinaweza pia kukataa nyimbo za kava ambazo zinaiga kwa karibu sana jina la msanii asili au mchoro wa albamu.
Hata kama maudhui hayakiuki sheria, yanaweza kuwachanganya wateja. Ndio maana huduma zinaweza kukataa.
Go to article
DistroVid See all 15 articles
-
DistroVid ni nini?
DistroVid ni huduma ya usambazaji wa Video za Muziki inayotolewa na DistroKid!
Bofya hapa ili kuiangalia!
Kama msanii wa DistroVid, unaweza kupakia idadi isiyo na kikomo ya video za muziki, na kubaki na 100% ya mapato yako kutoka kwenye video zako.
Wasanii wanaopakia video za muziki kupitia DistroVid watakuwa na video zilizosambazwa kwa Apple Music, Vevo, TikTok Music, Boomplay na TIDAL.
Pamoja na hizo huduma, wasanii pia wana chaguo la kusambaza kwenye DistroVid Gallery, ambayo ni mkusanyiko wa video zote za muziki zilizowasilishwa kwa DistroVid.
Ili kupakia video bila kikomo za msanii 1, uanachama wa DistroVid unagharimu $99 kwa mwaka. Nafasi ya msanii wa ziada ni $49 kwa mwaka juu ya usajili wa msingi.
-
Je, Inachukua Muda Gani Kwa Video Yangu Kwenda Hewani?
Kwa kawaida, inaweza kuchukua muda wowote kuanzia siku 1-5 kwa video kwenda hewani katika huduma mara zikishachakatwa na kuidhinishwa.
Kumbuka: Iwapo ni muhimu kwamba video yako ya muziki kwenda hewani kwa tarehe mahususi (katika huduma zote ulizochagua kwa wakati mmoja), chagua tarehe ya kutolewa angalau wiki nne zijazo. Ukichagua tarehe ya kutolewa iliyo chini ya wiki nne kabla, kuna uwezekano mdogo lakini sio sufuri kuwa video yako bado inaweza kukwama katika foleni ya ukaguzi wa huduma (au ucheleweshaji mwingine usiotarajiwa) wakati tarehe yako ya kutolewa itakapowadia.
Go to article -
Mahitaji ya Jumla ya Kupakia Video ya Muziki ni yepi?
Sheria za Jumla za Video za Muziki:
- Ubora. Huduma za kutiririsha zinahitaji video za muziki zenye ubora wa juu ambazo "zinaonekana kama video za muziki". Hii inamaanisha kwamba, video za staili ya TikTok haziruhusiwi. Aidha, huduma zinakataa video zenye mapungufu yasiyokusudiwa ya ubora, ikiwemo hitilafu, matatizo ya sauti, sauti ambayo haijaoanishwa n.k.
- Maudhui asili. Huduma za utiririshaji zinahitaji maudhui ya video yawe ya asili kwa 100% na yasiwe na alama za biashara, yapatikane mtandaoni, au yawe ni video ya hisa (hata ikibadilishwa). Hii ni pamoja na maudhui kutoka kwenye vipindi vya televisheni/filamu vinavyojulikana.
- Zisiwe na alama za utambuzi. Huduma za utiririshaji zitakataa video zenye alama za utambuzi, nembo, maandishi/picha mnato, manukuu, au viwekeleo vingine vya picha.
- Hakuna maelezo ya mitandao ya kijamii. Huduma za kutiririsha zitakataa video zilizo na URL, maelezo ya kuwasiliana, misimbo ya QR, au majina ya kukutambua/nembo za mitandao jamii.
- Hakuna matangazo. Huduma za utiririshaji haziruhusu kuweka tarehe za kuachia kazi, nembo au matangazo kwenye video. Hii ni pamoja na maneno kama "inatiririshwa kila mahali" au "inakuja hivi karibuni!".
- Hakuna picha mnato au matangazo. Huduma za kutiririsha zitakataa video zinazoonyesha fremu za michoro mnato ya albamu au maonyesho mengine ya slaidi ya picha. Lazima iwe VIDEO ya muziki.
- Hakuna nyimbo vipande. Huduma za utiririshaji zitakataa video ambazo zimefupishwa au kuhaririwa kuwa kionjo cha promosheni, kionjo au toleo lisilo kamili.
- Hakuna michanganyiko ya nyimbo, wimbo mmoja kwa kila video. Huduma za utiririshaji zitakataa michanganyiko ya nyimbo. Video za muziki (pamoja na video za maonyesho ya mubashara) lazima ziwe na wimbo mmoja tu.
Aina ya Faili: .mov au .mp4 pekee
Aina ya Ugandamizaji/Kodeki: ProRes 422 au 422 HQ, MPEG-2 au H.264
Ukubwa wa Faili: Hadi 30GB
Ung'avu 1920 x 1080 au zaidi (hadi 3840x2160)
Muda: Sekunde 30 au zaidi
Usimbaji wa Video: Variable Bit Rate (VBR) pekee
Kiwango cha Fremu ni mojawapo ya 23.976, 24, 25, au 30 (ili tuweze kuisambaza video yako kila mahali!)
Aina ya Video Scan: Endelevu (Progressive) pekee
Umbizo la Sauti: 44.1 kHz au zaidi, Stereo pekee
Ikiwa unakumbana na matatizo ya upakiaji na mafaili yoyote ya video za 4K, mbinu bora zaidi ni kupakia kwa kutumia kodeki ya H.264. Tafadhali kumbuka kuwa, kwa sasa huduma hazikubali kodeki ya HEVC/H.265. -
Ninawezaje Kuhariri Video yangu Baada ya Kuwa Nimeshaipakia kwenye DistroVid?
Ingawa DistroVid haina kipengele cha "Hariri Toleo" kwa wakati huu (kinafanyiwa kazi!), tuna furaha zaidi kusaidia kwa baadhi ya maombi ya kuhariri.
Iwapo unahitaji kurekebisha kosa la uandishi, jina la wimbo, aina ya muziki, jina la lebo, tarehe ya kutolewa au picha ya onyesho/kijipicha, wasiliana nasi hapa.
Kumbuka: Tunaweza kuhariri vijipicha, lakini maduka yanahitaji kijipicha hicho lazima kiwe picha iliyotolewa moja kwa moja kutoka kwa video. Unapowasiliana na timu yetu kuhusu kuhariri vijipicha, tafadhali jumuisha picha ya skrini ya kijipicha ambacho ungependa kutumia, pamoja na maelezo ya muda ambapo picha hiyo inaonekana ndani ya video yako.
Pia, tafadhali kumbuka kuwa kuna mambo fulani ambayo hatuwezi kuyahariri kwa wakati huu, yakiwa ni pamoja na kubadilisha faili la video au kuhariri majina ya wasanii. Ili kubadilisha faili la video, au jina la msanii, utahitaji kufuta na kupakia tena video na faili sahihi na/au jina la msanii.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta video yako, angalia makala hii.
Go to article -
Ninawezaje Kubinafsisha Chaneli Yangu ya Vevo?
Vevo haina tovuti ya kufikiwa na msanii au dashibodi kwa wakati huu, lakini tuna furaha kusaidia kuwasilisha picha ya profaili, picha ya bango na maelezo ya chaneli kwa Vevo kwa niaba yako!
Haya ndio mahitaji:
1. Picha ya Profaili: (pikseli 800x800, jpg)
2. Picha ya Bango: (pikseli 2048x1152, jpg).Unaweza kutumia kiolezo hiki kupima ukubwa wa picha yako ipasavyo ikiwa itahitajika(bonyeza kulia kwenye kipanya ili kupakia picha):
3. Sehemu ya maelezo yako, sheria za jumla hapa chini- Herufi 1000 au pungufu, bila kutaja maduka mengine (kama vile Spotify au Apple)
- Usitaje majina ya wasanii wengine. Jiepushe na utajaji wa moja kwa moja kama vile: "Mimi hupata msukumo wangu kutoka kwa The Beatles na Drake", au "Nilishirikiana na Madonna". Majukwaa yanaweza kuona hili kama kujaza maneno muhimu, na wakaondoa tawasifu au maelezo yako.
- Pasiwe na maelezo yanayoweza kuashiria muda wa sehemu ya maelezo. Epuka maelezo sawa na: "Albamu yangu mpya inatoka Julai 31, 2022", au "Albamu yangu ya karibuni ilitoka miezi 2 iliyopita".
Wasiliana nasi hapa ukiwa na picha yako ya profaili, picha ya bango na maelezo ya chaneli, na tunaweza kuwasilisha hayo moja kwa moja kwa Vevo!
Go to article
Kumbuka: Ombi la kusasisha chaneli likishawasilishwa, inaweza kuchukua kati ya siku 1-5 za kazi kwa picha na maelezo kuonekana kwenye chaneli yako ya Vevo. -
Kwa Nini Video Yangu Inakataa Kupakia?
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kufanya upakiaji wa video kushindwa, ambazo ni pamoja na kodeki au aina za faili zisizokubalika, lakini sababu ya kawaida kabisa inayosababisha hitilafu au kushindwa kwa upakiaji wa video ni kutokana na muunganisho duni wa intaneti.
Ikiwezekana tunapendekeza kutumia intanet ya nyaya badala ya Wi-Fi, kwa sababu mafaili ya video kwa kawaida ni makubwa sana kuliko upakiaji wa mafaili ya sauti, na upotevu wowote wa pakiti au kukatika kwa intanet (hata kwa sekunde chache) kunaweza kuleta hitilafu ya upakiaji. Unaweza pia kutaka kujaribu kufuta hifadhi muda na vidakuzi vya kivinjari chako kabla ya kupakia.
Aidha, kwa kawaida huwa tunaona hitilafu kwenye vipakizi ambavyo havikidhi mahitaji ya kiufundi ya faili ambazo huduma zinahitaji. Upakiaji wowote ambao hautumii aina ya faili ya video, kodeki iliyobanwa au vipimo vinavyokubalika inaweza kusababisha hitilafu.
Kwa orodha kamili ya aina za mafaili ya video inayokubalika, kodeki na vipimo, angalia makala hii kuhusu vigezo vya faili za video.
Ikiwa una muunganiko wa intaneti ulio imara na mafaili yako ya video yanakidhi mahitaji yote ya kiufundi, lakini bado unakabiliwa na matatizo ya kupakia, tafadhali wasiliana nasi hapa! Wakati wote tunafurahi kusaidia kutatua matatizo yoyote ya upakiaji wa video unayokumbana nayo.
Mixea See all 10 articles
-
Mixea ni nini?
Mixea ni huduma ya DistroKid ya kuboresha sauti mtandaoni! Unaweza kuitumia Mixea kuongeza mguso wa mwisho, kung'arisha mguso kwenye kazi yako kabla ya kuisambaza kwenye maduka.
Mixea huakisi mbinu za kisasa za uboreshaji ili kutoa mfululizo wa matokeo mahiri na yaliyopangwa vizuri ambayo unaweza kuchagua kati yao ili kupata sauti bora iliyoboreshwa kwa nyimbo zako.
Kama ilivyo kwa vipengele vingine vya DistroKid, Mixea ni huduma inayotegemea usajili, na kwa $99 kwa mwaka, unaweza kuboresha idadi yisiyo na kikomo ya nyimbo, kwa idadi isiyo na kikomo ya wasanii.
Unaweza kuelekea www.mixea.com ili kuijaribu na kupokea wimbo wako wa kwanza ulioboreshwa bila malipo!
-
Nitatumia Vipi Mixea?
Ni rahisi sana!
Ili kuanza, nenda kwenye Mixea kutoka kwenye Menyu ya "Vizawadi" iliyo juu kulia. Ukiwa kwenye ukurasa mkuu, chagua faili unalotaka kuweka kwenye injini ya uboreshaji kwa kubonyeza "Chagua Faili" au kushusha faili ndani.Kumbuka: Mixea inakubali tu mafaili ya WAV, FLAC, MP3 na M4A pekee kwa wakati huu.
Faili lako likishachaguliwa, bonyeza "Boresha Wimbo Wangu" ili kuanzisha injini ya kuboresha!
Katika hatua hii, kulingana na faili unalotumia, inaweza kuchukua dakika kadhaa kwa injini ya kuboresha kukamilisha mchakato huo. Katika hatua hii, inazalisha machaguo 15 (ndio 15!!!!) tofauti ya uboreshaji kwa wimbo wako.
Injini inapomaliza kufanya kazi, utaona dashibodi ya wimbi la wimbo, ambayo inaonyesha wimbi la onyesho la wimbo wako ulioboreshwa, pamoja na wimbi la wimbo wako asili ili uweze kuzilinganisha zote mbili.
Chini tu ya wimbi, utaona mizani mbili za kuteleza:
Nguvu - Chini, Kati, Juu
Nguvu hudhibiti vipengele tofauti vya wimbo wako. Kadiri nguvu inavyozidi kuongezeka, ndivyo wimbo wako unavyosikika kwa sauti kubwa na iliyogandamizwa zaidi, kwa gharama ya masafa fulani yanayobadilika.
Chaguzi za EQ - Angavu zaidi, Angavu, Isiyoegemea, Joto, Joto zaidi
EQ yenye joto zaidi huinua masafa ya chini na ya kati katika mchanganyiko wako, ilhali mpangilio angavu zaidi wa EQ huyainua masafa ya juu zaidi na kufanya mchanganyiko wako kusisimua zaidi.
Zijaribu zote ili kuona ni uboreshaji upi unaskika vizuri kwa kazi yako! Ukishachagua master unayoipenda, bonyeza "Pakua Wimbo Ulioboreshwa". Hii itakupeleka kwenye dashibodi yako ya Nyimbo Zilizoboreshwa, ambapo unaweza kuchagua mafaili matatu tofauti ya kazi yako iliyoboreshwa:
Ultra HD: HD WAV, 24-bit, 48k
Ubora wa juu: WAV, 16-bit, 44.1k
Ubora wa Kati: MP3, 256kbps
Chagua faili lako unalopendelea, bonyeza "Pakua" na kwa haraka, una wimbo ulioboreshwa!
Go to article -
Je, Nitatayarisha Vipi Nyimbo Zangu Kabla ya Kuzipakia kwenye Mixea?
Ili ufaidike zaidi na nyimbo zako zilizoboreshwa, tunapendekeza ufanye yafuatayo kabla ya kupakia faili zako:
- Programu-jalizi: Ondoa programu-jalizi zozote za kuboresha kutoka kwa kifurushi cha kuunganisha (ikiwa ni pamoja na compressor, kusawazisha, vidhibiti, na viboreshaji stereo).
- Nafasi kutoka kwa ukingo (Headroom): Jaribu kuhakikisha kuwa faili yako ya sauti haijapunguzwa. Ikipunguzwa kidogo ni sawa ikiwa huwezi kuibadilisha na huwezi kuisikia (labda kikuza sauti chako kilikuwa na joto sana mlipokuwa kwa kipindi hicho kizuri cha kucheza muziki), lakini inapendekezwa upakie kitu ambacho hakijakatwa.
- Ubora wa Kurekodi: Jaribu kutoa rekodi zenye ubora zaidi kwa kadri uwezavyo na zikiwa na kelele kidogo (yaani kelele ya nyuma iliyochukuliwa na kinasa sauti chako). Kelele kidogo ni sawa, lakini rekodi safi isiyo na kelele kabisa ni bora zaidi. Tunapendekeza uweke kiwango chako cha kusampuli kiwe 44.1 au 48 kHz. Kitu chochote cha juu zaidi ya 48 kHz kitapunguzwa hadi 48 kHz kabla ya uboreshaji.
- Umbizo la Faili: Hamisha nyimbo yako kwa kutumia umbizo lisilogandamizwa au ambalo halijapoteza ubora wake (yaani WAV, AIFF, au FLAC). Umbizo la ubora wa juu lililogandamizwa kama vile MP3 iliyosimbwa kwa kbps 256 au zaidi ni sawa pia, lakini umbizo lisilogandamzwa au lisilo la hasara ni bora zaidi.
- Majaribio: Ikiwa hupati matokeo unayotafuta, fanya majaribio! Jaribu kufanya mabadiliko kwenye mchanganyiko wako au kiuka mapendekezo yetu kwa kuongeza programu-jalizi moja au mbili kwenye kifurushi cha kuunganisha.
-
Je! Mixea Inaweza Kuboresha Aina Gani Za Mafaili?
Mixea inakubali mafaili ya WAV, FLAC, MP3, AIFF na MP4, yaburuze na yashushe kwenye injini ya kuboresha, na utakuwa umemaliza!
Unaweza kupakua nyimbo zako zilizokamilika kwenye Ultra HD (HD WAV, 24-bit, 48k), Ubora wa Juu (WAV, 16-bit, 44.1k), au Ubora wa Kati - (MP3, 256kpbs).
-
Je, Mixea Inagharimu Kiasi gani?
Mixea hugharimu $99 kwa mwaka, na hutozwa kila mwaka, katika tarehe ile ile ambayo ulijisajili katika huduma hiyo.
Kwa $99 kwa mwaka, unaweza kuboresha idadi ya nyimbo zisizo na kikomo, kwa idadi ya wasanii isiyo na kikomo, na kuwa na eneo moja la kuhifadhi kazi zako zote ulizoboresha. -
Je Napaswa Kuchagua Mipangilio Ipi ya Nguvu/EQ?
Unaujua muziki wako vizuri zaidi kuliko mtu yeyote! Chagua mipangilio ya Nguvu na EQ ambayo inasikika kwa ubora zaidi kwako. Mpangilio angavu wa EQ utaleta uwazi zaidi kwa sauti zako, huku mipangilio nyororo zaidi ya EQ itaongeza uwepo zaidi kwenye besi yako. Nguvu ya juu zaidi itazalisha toleo lililo na kiwango cha juu cha sauti ya wimbo wako na uchakataji na mgandamizo zaidi. Nguvu ya chini itaweka mguso laini zaidi kwenyewimbo wako. Watumiaji wengi huwa wanachagua Kiwango cha Kati na Usawa wa Kuegemea, lakini sio lazima!
Go to article
Kumbuka kuwa majukwaa mengi ya kutiririsha yanaweza kubadilisha ukubwa wa sauti ya wimbo wako ulizoboreshwa, lakini mengine yanaweza yasibadilishe, na hilo ni sawa kabisa! Inahakikisha kiwango cha sauti kinafanana kati ya nyimbo zote kwa ajili ya wasikilizaji wao. Kwa mara nyingine tena, chagua kiwango cha sauti kinachosikika vyema zaidi kwako katika kiwango cha kawaida cha mpangilio wa ukubwa wa sauti.
HyperFollow See all 3 articles
-
HyperFollow ni nini?
HyperFollow ni nyenzo ya promosheni bila malipo (na yenye nguvu ya ajabu) inayopatikana kwa wasanii wote wa DistroKid.
Siku hizi, ni lazima kuwa na kiungo kimoja kinachoongoza kwenye muziki wako kwenye huduma zote za utiririshaji, na hapo ndipo HyperFollow inapoingia!
Mara unapomaliza kupakia toleo lako, unaweza kuanza kutangaza na kukusanya hifadhi za awali kwenye Spotify (pamoja na anwani za barua pepe za mashabiki) ukitumia HyperFollow. Punde tu toleo lako linapoenda hewani kwenye tarehe yake ya kutolewa, ukurasa wako wa HyperFollow UTASASISHA KIOTOMATIKI(!) ili kujumuisha viungo vya huduma zingine za utiririshaji.
Kiungo chako cha HyperFollow hakibadiliki, na hutahitaji kusasisha nakala yako ya matangazo au machapisho ya mitandao ya kijamii.
Unaweza kupata kiungo chako cha HyperFollow kwenye ukurasa wa albamu yako ya DistroKid, au kwa kubofya Menyu ya Vipengele vya DistroKid upande wa juu kulia
na kisha kubofya "Jitangaze".
Hapa ni baadhi ya faida za ziada za kutumia HyperFollow:
Wafuasi zaidi! Yeyote anayebofya kitufe kwenye ukurasa wako wa HyperFollow ili kuhifadhi mapema toleo lako, moja kwa moja atakufuata Spotify.
Wasikilizaji zaidi! Mbali na kufuata ukurasa wako wa msanii kwenye Spotify, yeyote atakayebofya kitufe pia atahifadhi albamu yako moja kwa moja kwenye maktaba yake ya Spotify.
Utafiti zaidi! Utakuwa unapata taarifa za eneo la kijiografia kwa kiwango cha jiji, na taarifa zingine za kidemografia {ambazo hazipo wazi) zinazohusu mashabiki wako katika eneo husika.
Ufahamu zaidi! Utaweza kuona muziki mwingine ambao mashabiki wako wanasikiliza, hata kama hao wasanii wengine hawatumii DistroKid.
Takwimu zaidi! Utafahamu ni watu wangapi walitembelea ukurasa wako wa HyperFollow, na ni wafuasi wangapi ulioongeza.
Wawasiliani zaidi!** Utapewa barua pepe ya kila shabiki.
** Ni Musician Plus na Akaunti za Mpango wa Ultimate pekee ndizo zina fursa ya kufaidika na anwani za barua pepe za mashabiki.Je, unahitaji kufanya mabadiliko kwenye ukurasa wako wa HyperFollow? Bofya hapa!
-
Je, ninaweza kuweka pikseli za ufuatiliaji za Facebook au Google kwenye ukurasa wangu wa HyperFollow?
Ndiyo!
Huduma hii haina malipo kwa wanachama wote wa DistroKid na inatolewa ili kuwasaidia wasani na malengo yao yakutafuta masoko mtandaoni.
Ili kuongeza pikseli ya ufuatiliaji:
- Ingia kwenye DistroKid
- Tembelea ukurasa wako wa HyperFollow (hakikisha umeingia)
- Bofya "Customize" hapo juu
- Bofya "Hariri ukurasa huu"
- Bofya "Una pikseli ya tangazo au uchanganuzi?"
Imekamilika! Utembeleaji wote kwenye ukurasa utafuatiliwa kupitia kitambulisho chako cha pikseli.
Kuna baadhi ya matukio maalum vilevile (kwa kutumia kipengele cha "trackCustom" cha Facebook). Matukio hayo ni:
- clickSpotifyPresave - Huwaka mtu anapobofya kiungo chako cha Spotify cha kuhifadhi kabla
- spotifyPresaveSuccess - Wakati mtu amefaulu kuhifadhi toleo lako mapema
- click[store] (kwa mfano: "clickSpotify" au "clickAppleMusic") - Mtu anapobofya mojawapo ya viungo vya huduma za utiririshaji ili kusikiliza muziki wako
- clickOut - Mtu anapobofya kiungo chochote miongoni mwa viungo vikuu kwenye ukurasa wako wa HyperFollow. Hii itafanya kazi sambamba na click[store] (ambayo huonyesha ni kiungo kipi hasa walibofya)
- clickSocial - Mtu anapobofya kiungo chochote cha mitandao ya kijamii kwenye ukurasa wako wa HyperFollow
- audioPlay - Mtu anapobofya kitufe cha kucheza ili kusikiliza kipande kidogo cha muziki wako
- audioPause - Mtu anapobofya kitufe cha kusitisha ili kusimamisha usikilizaji wa kipande cha sauti
- audioSkipForward - Ikiwa toleo lako lina nyimbo nyingi, mtu aliruka hadi kwenye wimbo unaofuata
- audioSkipBack - Ikiwa toleo lako lina nyimbo nyingi, mtu aliruka hadi kwenye wimbo uliotangulia
- showFullImage - Mtu alibofya mchoro wa albamu yako ili kuonyesha picha ya ukubwa kamili
Natumai hii inasaidia!
-
Je, Naweza Kuhariri Ukurasa Wangu Wa HyperFollow?
Ndio! Sasa kuna vipengele vichache vinavyopatikana kwenye kurasa za HyperFollow, sambamba na uwezo wa kufanya marekebisho, na kurasa mpya zisizotegemea matoleo yako!
Kwanza, ili kuona na kufanya marekebisho kwenye kurasa zako za HyperFollow, unaweza kwenda kwenye https://distrokid.com/hyperfollow au bofya kwenye Menyu ya Vipengele vya DistroKid upande wa juu kulia
na kisha bofya "Jitangaze".
Kutokea hapo, unaweza kubofya "HyperFollow" ili kutazama dashibodi yako ya HyperFollow, ambayo inajumuisha matoleo yako yote.
Chini ya jina la kila toleo utaona hesabu ya waliotazama, na ikiwa ni toleo lililojitengeneza kiotomatiki la ukurasa wa HyperFollow, unaweza kuona hifadhi zote za awali, idadi ya waliotazama, na barua pepe ulizokusanya kwa kubofya kiungo cha "# hifadhi kabla" karibu.na kaunta ya maoni.
Ili kuhariri ukurasa wowote wa hyperfollow.com/yourlink au distrokid.com/hyperfollow/kiungochako unaweza kutembelea www.distrokid.com/hyperfollow, na bofya kitufe cha "Hariri" chini ya ukurasa wa HyperFollow ambao ungependa kufanya marekebisho.
Kwa kurasa zozote za HyperFollow zinazozalishwa kiotomatiki, unaweza pia kuhariri kurasa hizo moja kwa moja kutoka kwenye ukurasa husika. Mara unapokuwa kwenye ukurasa wa HyperFollow unaotaka kuhariri, bofya "Customize" kwenye kona ya juu kulia ya ukurasa ili kuonyesha machaguo kadhaa, kisha bofya "Hariri ukurasa huu" (hii pia inafanya kazi kwenye vifaa vya mkononi kama vile simu janja!):
- Onyesho la vipande vya sauti
- YouTube pachika
- Ongeza viungo vya mitandao ya kijamii
- Ficha kurasa zako zozote za HyperFollow (ziweke wazi wakati wowote!)
Huu hapa ni mfano wa ukurasa wa HyperFollow ukiwa na baadhi ya vipengele vipya:
https://distrokid.com/hyperfollow/butchersofthefinalfrontier/kh4
Ukikumbana na masuala yoyote wakati wa kuhariri au kufanyia marekebisho ukurasa wako wa HyperFollow, tafadhali tujulishe hapa: www.distrokid.com/contact
Vizy See all 4 articles
-
Vizy ni nini?
Vizy ni kitengeneza video za muziki ambacho wanamuziki wanaweza kutumia kupata video za kuchapisha muziki wao kwenye Instagram, YouTube, TikTok, Twitter, Facebook na zaidi.
Chagua kutoka kwa violezo 20 tendaji na vinavyovutia ambavyo husisimua na kuwaweka makini wasikilizaji wako.
Ni rahisi! Anzia kwa Vizy.com.
-
Je, Vizy Inagharimu Kiasi gani?
Kila video iliyotengenezwa na Vizy inagharimu $8.99 kwa dakika 5 za kwanza za wimbo wowote na senti 99 kwa kila dakika ya inayoongezeka.
Ukinunua saizi nyingi za kiolezo kimoja kwa mara moja, utapokea punguzo la 10%.
Go to article -
Je, Ni Wapi Naweza Kupata Video Zangu Za Muziki za Vizy?
Ili kuzipata video za muziki ulizotengeneza na Vizy, ingia katika akaunti yako ya DistroKid, na tembelea https://distrokid.com/videos/.
Tafadhali kumbuka kwamba, kwa kawaida huchukua takribani siku moja kutengeneza video. Tutakutumia barua pepe ikikamilika. 🙂
-
Ninapataje Hiyo Video Nzuri ya Baby Yoda?
Utahitajika kutembelea kwenye Kitengeneza Marcel chetu!
Elekea https://distrokid.com/marcel kutengeneza yako mwenyewe!
Video hizi ndogo ni nzuri na zinafurahisha kuzisambaza, lakini kwa mwonekano wa kitaalamu zaidi, nenda kwenye Vizy.com kwa video maalum za taswira za sauti za muziki wako. ⚡️👽⚡️
Maelezo zaidi juu ya Vizy yanaweza kupatikana hapa.
DistroLock See all 2 articles
-
DistroLock ni nini?
DistroLock hufanya iwe vigumu kwa yeyote (ambaye sio wewe) kupakia muziki wako asili kwenye huduma za utiririshaji.
Hivi ndivyo hufanya kazi:
Pakia Muziki Wako Bila Malipo.
Pakia nyimbo zako asili kwenye DistroLock, au tutumie tu alama ya utambuzi wa sauti.
Tunalinda Alama ya Utambuzi.
Tunabainisha kwamba sauti "mefungwa" wakati huduma za muziki zinapouliza. Ni wewe pekee ndie unayeweza kuifungua.
Unalindwa.
Pia tunasajili sauti yako na huduma zingine zinazoongoza kwenye shughuli za utambuzi wa sauti.
DistroLock huchukua "alama ya utambuzi wa sauti," huiweka kumbukumbu, na kisha kufuta sauti yako kutoka kwenye seva zetu. Ikiwa hutaki kupakia muziki wako kwenye DistroLock, unaweza kutengeneza alama ya utambuzi kwenye kompyuta yako mwenyewe kwa kutumia Chromaprint na tuma hizo tu.
DistroLock pia inaweza kusajili muziki wako na kanzidata za umma zinazoongoza kwenye shughuli za utunzaji wa alama za utambuzi. Baadhi ya huduma hizi zinaweza kutambua sauti zinazofanana hata kama kasi ya sauti imefanywa kuwa kubwa, ukubwa wa sauti umedadilishwa, au kubadilishwa vinginevyo. Huduma nyingi za muziki hutumia huduma hizi kuzuia matoleo yasiyoidhinishwa, ikiwa ni pamoja na YouTube, DistroKid, SoundCloud, Facebook, Vimeo, Twitch, na wengine.
-
Ni Aina Gani ya Sauti Ninayoweza Kuifunga kwenye DistroLock?
DistroLock hufanya kazi vyema zaidi kwa muziki ambao bado hujasambazwa. Muziki uliotolewa hapo awali unaweza kuwa tayari katika kanzidata za sauti za umma, ikiwa na maana hauwezi kufungwa na mtu yeyote.
Habari njema: Ikiwa *wewe ndie* uliyeusambaza hapo awali, tayari una ulinzi fulani. Hiyo ni kwa sababu maduka na wasambazaji husika wanaweza kulinganisha upakiaji wao mpya na kanzidata za sauti za umma, na kukataa matoleo yasiyoidhinishwa ya muziki wako.
Kumbuka: Nyimbo zilizo na sauti zinazopatikana kwa umma (mizunguko ya kawaida, sauti na sampuli) zinaweza kukataliwa na DistroLock. Sababu ni kwamba, hizo ni sauti ambazo kila mtu anaruhusiwa kuzitumia - ambazo zinaweza kusababisha utambulisho chanya na muziki wa watu wengine.
Natumai hii inasaidia na asante kwa kujaribu DistroLock.
Slaps See all 1 articles
-
Slaps.com ni nini?
Slaps ni mtandao wa kijamii wa muziki kwa wasanii na watu wanaopenda muziki.
Kwa kawaida, Wasanii kwenye Slaps hupata maoni kwa haraka kuhusu muziki wao asili.
Iangalie.
NFTs See all 1 articles
-
Sellouts
Sellouts ni ushirikiano na watengenezaji 10,000 wa muziki wanaojitegemea ili kubuni na kutengeneza NFT 10,000 za kibinafsi, zinazoweza kukusanywa, na zisizotoa kaboni ambazo huadhimisha muziki wa kila msanii.
Kuanzia tarehe 17 Novemba hadi Desemba 1, 2021, wasanii walikuwa na uwezo wa kujiunga na orodha ya wanaosubiri Sellouts, na kuunda NFT zao wenyewe hapa: https://distrokid.com/sellouts
Tumeshirikiana na Nifty Gateway, ambalo ni jukwaa rahisi kwa wasanii ambalo limeahidi utengenezaji wa NFT usiotoa kaboni (maelezo zaidi hapa) kwa mkusanyiko.
Sellout zote 10,000 zilikuwa tayari kununuliwa ($60/kila) kwenye Nifty Gateway kupitia droo ya nasibu tarehe 15 Desemba 2021, na NFT zote 10,000 halisi ziliuzwa siku iliyofuata!
Ikiwa ulijumuika katika ushirikiano, na unataka kuangalia hali ya uwasilishaji wako wa NFT, unaweza kutembelea https://distrokid.com/sellouts/me ili kuona kama wasilisho lako lilichaguliwa.
Ingawa hatutazalisha au kutoa NFT zozote za ziada za Sellouts kwa sasa, kaa tayari kwa fursa zaidi za NFT katika siku zijazo!
Tafadhali kumbuka: Nifty Gateway na DistroKid kila mmoja huchukua ada ndogo ya uchakataji inayotokana na kila mauzo ya NFT.
Zaidi, hakuna haki miliki kwa muziki zinazokuja na umiliki wa NFT za Sellouts.
Kisheria See all 8 articles
-
Nani Anamiliki Muziki Wangu?
Ni wewe! DistroKid haichukui umiliki au haki zozote za umiliki kutoka kwa wasanii. Unaendelea kumiliki kazi zako kwa 100%.
Go to article -
Ni Umri wa Chini wa Kutumia DistroKid?
Ni lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi ili kujisajili na DistroKid, kwa mujibu wa Mkataba wetu wa Usambazaji.
Ikiwa wewe ni mdogo kuliko huo umri, tafadhali acha mtu mzima ajisajili kwa niaba yako.
Go to article -
Je, Nahitaji Kuwa na Hakimiliki ya Muziki Wangu Kabla ya Kupakia?
Huu sio ushauri wa kisheria, na sisi sio wakili wako. Lakini... chini ya sheria ya sasa ya hakimiliki, ambayo ilianza kutumika Januari 1, 1978, kazi inalindwa moja kwa moja na hakimiliki mara inapotengenezwa. Kazi inatengenezwa wakati "imerekebishwa" au kujumuishwa katika nakala au fonorekodi kwa mara ya kwanza. Hautahitajika usajili katika Ofisi ya Hakimiliki wala uchapishaji ili kuwa na ulinzi wa hakimiliki kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, kuna manufaa fulani kwa kufanya usajili, ikiwa ni pamoja na kuweka rekodi ya umma ya madai ya hakimiliki. Kwa ujumla, usajili wa hakimiliki ni lazima ufanywe kabla ya kuletwa kwa madai ya ukiukaji wa hakimiliki. Usajili kwa wakati unaweza pia kutoa anuwai ya suluhu katika madai ya ukiukaji.
Kwa maelezo zaidi, tembelea http://www.copyright.gov/circs/circ50.pdf -
Masharti ya matumizi ya DistroKid ni yapi?
Tafadhali tazama Masharti yetu ya Huduma na Mkataba wa Usambazaji hapa chini.
- Masharti ya huduma: https://distrokid.com/terms/
- Makubaliano ya Usambazaji: https://distrokid.com/agreement/
-
Je, DistroKid ni ya Kipekee? Je, Bado Naweza Kutumia Wasambazaji Wengine?
DistroKid sio ya kipekee.
Ikiwa ungependa kusambaza baadhi ya (au zote) kazi zako kwa kutumia wasambazaji tofauti wakiwa pamoja na DistroKid, au pasipo na DistroKid--unakaribishwa kufanya hivyo.
Natabiri hutataka kufanya hivyo!
Go to article -
Uondoaji na Upingaji wa Madai ya DMCA
DistroKid inachukulia masuala ya haki miliki kwa uzito. Ili kuhakikisha utii wa sheria, mbinu bora na uadilifu wa huduma zake, DistroKid inafanya kazi kila mara ili kuhakikisha watumiaji wetu wanapakia tu maudhui ambayo wana haki nayo kwa 100%.
Ikiwa unaamini kwamba maudhui yoyote kwenye huduma zetu yanakiuka hakimiliki yako au hakimiliki ya mtu unayemwakilisha, tafadhali angalia masharti yetu hapa.
Walalamishi wanaweza kuwasiliana na Wakala wetu Aliyeteuliwa wa Hakimiliki au kutumia fomu yetu ya tovuti kuwasilisha ripoti ya madai ya ukiukaji wa hakimiliki hapa.
Je, maudhui au kazi zako zimeondolewa kutoka DistroKid kutokana na madai ya hakimiliki? Kwa mujibu wa DMCA, DistroKid inakubali taarifa za maombi ya kurejesha maudhui yaliyoondolewa kwa tuhuma za ukiukaji wa hakimiliki. Ingawa hatuwezi kutoa ushauri wowote wa kisheria, ikiwa una imani ya nia njema kwamba maudhui yako yaliondolewa kwa sababu ya mkanganyiko kwa kutambua au kimakosa, unaweza kuwasilisha notisi yako kwa Wakala wetu Aliyeteuliwa wa Hakimiliki kutaka maudhui yaliyoondolewa yarejeshwe kama ilivyobainishwa kwa Masharti yetu.
Iwapo unatoa taarifa zisizo sahihi kwamba maudhui hayakiuki hakimiliki au unatoa taarifa zingine zisizo za kweli, unaweza kulipa kwa madhara uliyosababisha (ikiwa ni pamoja na gharama na ada za wakili). Taarifa za ulaghai za kutaka kurejesha maudhui yaliyoondolewa au matumizi mabaya ya huduma za DistroKid, yote hayo yanaweza kusababisha kusitishwa kwa akaunti yako au kukabiliwa na hatua za kisheria.
Sio suala la DistroKid? Iwapo mtu amepakia haki miliki yako kwa kutumia huduma nyingine tofauti na DistroKid, kwa bahati mbaya hilo sio jambo tunaloweza kusaidia nalo. Hata hivyo, unaweza kuwasiliana na kila huduma ya utiririshaji kwa ombi la kuondolewa maudhui na DMCA. Huenda ukahitaji kufanya utafiti kupitia Google kuhusu mchakato wa kila huduma katika Uondoaji wa DMCA, lakini hapa kuna viungo kadhaa vya michakato husika:
Spotify: https://www.spotify.com/us/legal/infringement-form/
iTunes/Apple Music: https://www.apple.com/legal/internet-services/itunes/itunesstorenotices/
YouTube: https://support.google.com/legal/troubleshooter/1114905
Amazon: https://www.amazon.com/report/infringement