Inaweza kuchukua siku kadhaa kwa albamu kukaguliwa, kuidhinishwa na kutumwa kwa huduma za utiririshaji.
Baada ya hatua hiyo, toleo lako linapaswa kwenda hewani mara linapoingizwa kwenye huduma za utiririshaji kulingana na makadirio yaliyo hapa chini:
- iTunes/Apple Music: Siku 1-7. Asilimia ndogo sana ya albamu hukaguliwa kwa mikono pale Apple, jambo ambalo linaweza kuchukua takriban wiki 1-2.
- Spotify: siku 2-5
- Amazon: siku 1-2
- YouTube Music: siku 1-2
- Deezer: siku 1-2
- TIDAL: siku 2
- Facebook/Instagram: wiki 1-2
- TikTok: siku 1-2
-
Anghami: siku 1-5 (baadhi zinahitaji ukaguzi unaofanywa na watu halisi kutoka timu ya Anghami; ukaguzi ambao unaweza kuchukua siku za ziada 2-3).
Kwa huduma nyingi za kutiririsha (iTunes, Amazon, Spotify, na zingine), tutagundua mara tu albamu yako inapoenda hewani, na tutakutumia barua pepe yenye kiungo!
Kucheleweshwa ni nadra, lakini huwa kunatokea, na kwa kawaida DistroKid huwa hawawezi kufanya lolote moja kwa moja. Ikiwa ni muhimu kwa albamu yako kwenda hewani katika huduma zote katika tarehe mahususi, tunashauri upakie toleo lako mapema kwa kutumia tarehe maalumu ya baadaye utakayochagua kwa ajili ya kuachia albamu. Tafadhali tazama makala haya kwa maelezo zaidi kuhusu tarehe maalum za kutolewa.
Nyimbo za Kava
Ikiwa unapakia wimbo wa kava, inaweza kuchukua hadi siku 14 za kazi kuweza kupata leseni za nyimbo za kava. Matoleo yenye nyimbo za kava yatatumwa mara tu leseni itakapoidhinishwa na Harry Fox Agency (wanaoshughulikia leseni zetu za nyimbo za kava).
Huduma Zilizochujwa
Baadhi ya huduma huchuja muziki wanaoupokea kutoka DistroKid, na zina taratibu zao wenyewe za kukubali muziki huo kuingizwa kwenye maktaba yao baada ya kuwasilishwa.
Kwa mfano, Pandora wana mchakato wao wa ndani wa kuhakiki ili kuchuja maudhui, hivyo hatuna uwezo wa kutoa taarifa juu ya muda gani inachukua kwa matoleo kuongezwa kwenye vituo vya Pandora (ikiwa yataongezwa).
Zaidi, muziki unaotumwa kwenda Roblox unachujwa na timu yao, na kutuma muziki wako Roblox haikuhakikishii kwamba utaenda hewani kwenye jukwaa lao. Kwa maelezo zaidi kuhusu kutuma muziki Roblox, angalia makala haya.
Amazon vilevile huchuja muziki kwa ajili ya Prime na Amazon Music Unlimited nchini Kanada. Tunatuma muziki wako, na unaweza kuongezwa ikiwa utaonekana unafaa. Hatuna udhibiti wowote juu ya mchakato wao wa uteuzi.
Sign Up