Kupitia DistroKid Publishing, DistroKid wanakusanya mirabaha inayohusiana na utunzi wa wimbo, ikiwa ni pamoja na ifuatayo:
- Mirabaha inayotokana na matumizi ya wimbo kidijitali duniani: Mirahaba ya utunzi inayotokana na kutiririshwa na kupakuliwa kwa muziki wako. Hii ni tofauti na mirahaba yako ya kawaida ya utiririshaji, ambayo DistroKid tayari hukusanya kwa wanachama wote.
- Mirabaha ya matumizi ya wimbo Marekani kwa njia zisizo za kidijitali, kama vile CD and Vinyl: Mirabaha inayopatikana muziki wako unapozalishwa tena nje ya mtandao, kama vile mauzo ya CD and Vinly.
- Mirabaha ya kucheza nyimbo kidijitali hadharani kokote duniani: Mirabaha kutoka kwa redio za mtandaoni zisizoshirikisha wasikilizaji (ambapo wasikilizaji hawawezi kuchagua wimbo unaofuata), na redio ya setilaiti.
- Mirabaha ya kucheza muziki hadharani kupitia njia zisizo za kidijitali Marekani: Mirabaha inayotokana na nyimbo kuchezwa sehemu za umma, ikiwemo maonyesho, matangazo, kwenye kumbi, n.k.
- Mapato ya kutumia wimbo katika kazi za video ulimwenguni (bila kunyima haki kwa wengine): Mirabaha inayopatikana pale wimbo unatumika pamoja na picha, kama vile filamu au kipindi cha televisheni.
- Malipo ya makubaliano ya kesi/ya kulazimisha kisheria: Fedha wanazolipwa watunzi wa nyimbo kama sehemu ya makubaliano kwa kesi za kundi kwa pamoja au faini.
Ikiwa tayari umejiunga na Shirika la Haki za Wasanii (PRO), DistroKid wanakusanya mgao wa mirabaha wa mchapishaji na wa mtunzi wa wimbo kwenye mirabaha iliyotajwa hapo juu . Ikiwa hujajiunga na Shirika la Haki za Wasanii (PRO), DistroKid watakusanya tu mgao wa mchapishaji wa mirabaha hiyo. Jifunze zaidi kuhusu PROs hapa.
Sign Up