DistroKid inajulikana vizuri kwa kuwa njia ya haraka na rahisi zaidi ya kufikisha muziki wako kwenye huduma za utiririshaji na kupokea 100% ya mapato yako.
Lakini wanachama wa DistroKid pia wana ufikiaji mkubwa sana wa (nyingi ni bure!
) nyenzo na huduma ambazo tunadhani utazipenda!
Ingia kwenye DistroKid na bonyeza menyu ya Vipengele vya DistroKid sehemu ya juu ya skrini ili kufikia Vizawadi - na usome zaidi hapa chini kwa habari kuhusu kila kipengele mahususi:
Â
Pata Kusikika Sasa Hivi
-
Playlister - Taarifa za mawasiliano kwa wamiliki wa orodha ya nyimbo ya Spotify. (Ultimate pekee)
-
Slaps.com - Mtandao wa kijamii kwa wanamuziki, ulioboreshwa kwa mwingiliano mkubwa.
-
Playlist Spotlight - Pigiwa kura kwenye Orodha za aina ya muziki za DistroKid.
- Gurudumu la Orodha ya Nyimbo - Zungusha gurudumu ili uwekwe katika orodha yetu ya nyimbo zilizopo Spotify.
Â
Jitangaze mwenyewe
-
HyperFollow - Kiungo kimoja kinacholeta pamoja vingine vyote! HyperFollow ni njia isiyo na malipo na rahisi ya kutengeneza kurasa zinazoonyesha muziki wako, video, viungo vya mitandao ya kijamii na zaidi.
-
Video Fupi - Video unazopata bila malipo, fupi zilizotanafsishwa (ili kukidhi mahitaji yako) ili kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
- Kadi za Matangazo - Makumi ya picha za bila malipo, zilizotanafsishwa (ili kukidhi mahitaji yako) hapohapo unazoweza kutumia kutangaza matoleo yako mapya mtandaoni.
Ufikiaji Maalum
-
Ufikiaji wa papo hapo wa Spotify for Artists - Spotify for Artists huwasaidia wasanii kunufaika zaidi na Spotify. Simamia profaili yako ya msanii, jifunze kuhusu wasikilizaji wako, na shirikisha maoni kwa timu ya Spotify.
-
Ufikiaji wa Papo Hapo wa Apple Music for Artists - Apple Music for Artists itakusaidia kuelewa vyema athari za muziki wako kwenye Apple Music na iTunes. Tambua hatua kubwa ambazo muziki umepiga na muziki bora katika historia. Fahamu wasikilizaji wako ni akina nani na wapi wanakopatikana. Pakia picha na wasifu wako wa umma wa msanii.
- TIDAL Artist Home - Jipatie wasifu wako wa msanii na yafanye maelezo muhimu yakidhi mahitaji yako; na malezo hayo ni kama vile picha ya wasifu wako, maelezo ya wasifu, na viungo vya kijamii. Unaweza pia kuripoti maudhui yasiyo sahihi moja kwa moja kwa TIDAL ndani ya sekunde chache, kuwaalika wanachama wa timu na kupata fursa ya kila kitu ambacho TIDAL hutengeneza kwa ajili ya wasanii katika siku zijazo.
- YouTube Official Artist Channel ("OAC") - Official Artist Channels zinaundwa ili kuwasaidia wasanii na timu zao kunufaika zaidi na YouTube. Pandisha chaneli yako leo ili uweze kuona takwimu na nyenzo ambazo zitakusaidia kuwasiliana na mamilioni ya mashabiki na kusimamia kwa ubora uwepo wako kwenye jukwaa.
-
Audiomack Connect - Unganisha na akaunti yako ya Audiomack na pakia muziki moja kwa moja kutokea DistroKid. Ili kujifunza zaidi kuhusu kupakia muziki kwenye Audiomack, tembelea Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara.
-
Twitch - Tuma maombi ya kujiunga na programu ya Twitch incubator ambayo huwasaidia wasanii kukua na kupata pesa moja kwa moja kutoka kwa mashabiki waliopo Twitch.
- Ufuatiliaji wa RIAA kwenye Gold na Platinum - Tuache tuangalie ikiwa muziki wako unakustahiki kupata cheti cha RIAA Gold au Platinum. (Ultimate pekee)
Boresha Muziki Wako
- Spotify Canvas Generator - Tengeneza video tanafsi(yaani zinazokidhi mahitaji yako) na za bila malipo za Canvas kwa ajili ya toleo lako Spotify.
-
Mistari - Ongeza mistari yako katika huduma za utiririshaji na injini za kutafuta. Ukishaweka maneno ya wimbo, unaweza pia kuongeza mistari iliyooanishwa na muda kwa ajili ya Instagram, Spotify, TIDAL na zaidi kwa kuchagua kuingia kwa Lyric Blaster.
-
Waliochangia & Maelezo ya Jalada - Wasilisha majina ya waliochangia, watunzi wa nyimbo, watayarishaji, wanamuziki, wahandisi na zaidi.
- Dave - Dave ni roboti yetu ya kiotomatiki ya A.I. ambaye atachambua muziki wako. Mjaribu!
Linda muziki wako
-
DistroLock - Linda muziki wako dhidi ya utolewaji usioidhinishwa.
- Hifadhi Salama - Uhifadhi bila malipo wa idadi yoyote wa kila kitu ambacho umewahi kupakia kwenye DistroKid. Inajumuisha mafaili ya sauti, michoro, UPC, ISRC na zaidi.
Vinasaidia Vinapohitajika
-
Mapya Kuhusu Miunganisho - Huduma za kutiririsha wakati mwingine huwaweka pamoja wasanii walio na majina sawa (au yanayofanana), au hutengeneza ukurasa mpya wa msanii badala ya kutumia ukurasa wako uliopo. Habari njema ni kwamba, tumeunda kitu cha kusuluisha shida hii haswa!
-
Kiangalizi cha URI ya Spotify - Pata URI yako ya Msanii/Albamu/Wimbo wa Spotify
-
Kiangalizi cha Apple ID - Chukua ID yako ya Msanii/Albamu/Wimbo wa Apple kwa toleo lolote ambalo umepakia.
- YouTube Allowlist - Kama ulichagua YouTube Content ID lakini unataka kuondoa madai kutoka kwenye video yoyote mahususi, unaweza kuongeza kwenye Allowlist, yaani orodha inayoruhisiwa hapa.
DistroKid mara kwa mara hutoa vipengele vipya vya kufurahisha na vilivyo muhimu kwa wanachama wa DistroKid, kwa hivyo hakikisha unaangalia menyu ya "Goodies" mara kwa mara!
Sign Up