Duka la bidhaa la Direct linagharimu $70 Dola za Marekani kwa mwaka, ambayo ni takriban $5.89 kwa mwezi. Hii ni ada ya uanachama isiyobadilika ya kila mwaka inayokuwezesha kufikia duka lako la bidhaa, nyenzo za kutengeneza bidhaa na kumeneji oda.
Jinsi ya Kujisajili kwa Direct
Ili kujisajili kwa Direct, tembelea https://distrokid.com/direct na uchague msanii unayetaka kumtengenezea duka. Wakati wa kujisajili, utaombwa kuwezesha uanachama wa Direct, ambao utatozwa kwa njia ya malipo ambayo tayari imehifadhiwa kwenye akaunti yako ya DistroKid.
Kuendeleza Usajili Kunavyofanya Kazi
Uanachama wako wa Direct unaendelezwa kiotomatiki kila mwaka tarehe uliyojisajili kwa mara ya kwanza.
Hivi ndivyo unavyoweza kuona tarehe yako ya kuendeleza usajili:
Bofya ikoni ya profaili yako katika sehemu ya juu kulia ya dashibodi yako ya DistroKid.
Chagua Risiti, au nenda moja kwa moja kwa https://www.distrokid.com/receipts.
Tarehe ya kwanza iliyoorodheshwa ya usajili wako wa Direct ni siku ambayo uanachama wako ulianza na tarehe ambayo utaendelezwa kila mwaka.
Sign Up