Mchoro unapaswa kuwa katika faili la umbizo la .jpg. Mahitaji ya kipimo cha chini kwa mchoro wa albamu ni pikseli 1000x1000. Kimsingi, mchoro wa albamu unapaswa kuwa na umbo mraba, na pikseli 3000x3000. Ikiwa mchoro wako ni mdogo sana, au una umbo mstatili, tutaurekebisha kiotomatiki kwa ajili yako--lakini kuna hatari kwamba toleo letu lililorekebishwa halitaonekana sawa na ulivyokusudia.
Tafadhali pia hakikisha kwamba mchoro wako uko katika nafasi ya rangi ya RGB. Kwa kawaida hili sio suala la kufikiria -- kila kamera ya kidijitali na programu za kurekebisha picha (kama Photoshop) zinakuwa kwenye RGB. Hivyo, upo vizuri.
Hata hivyo, wakati mwingine kwa sababu yoyote ile, unaweza kuwa umehifadhi mchoro katika nafasi ya rangi ya CMYK au Grayscale, na DistroKid inakupa ujumbe wa hitilafu. Hili likitokea kwako, hifadhi upya mchoro wako katika umbizo la RGB.
Endapo unatumia Photoshop, bofya hapa kuona jinsi gani. Ikiwa huna Photoshop, kupakiaji na kuhifadhi upya faili lako kwa kutumia Kihariri cha Pixlr itaibadilisha kiotomatiki na kuwa RGB.
Huduma za utiririshaji zitakataa mchoro wenye
- Anwani ya tovuti (URL)
- Jina la Twitter
- Maneno 'Pekee' au 'Toleo Lenye Ukomo'
- Picha yoyote yenye ukungu, pikseli zinazoonesha, iliyozungushwa, au zenye ubora duni
- picha zisizo na leseni/picha zenye leseni za kibiashara
- Bei
- Nembo za huduma za kutiririsha (kama vile iTunes au Spotify)
- Uchi
- Mambo machafu
- Marejeleo ya midia halisi (mfano: "CD" au "Compact Disc")
Aidha, tafadhali usitumie mchoro mmoja kwa albamu nyingi. Mchoro wa albamu unaojirudia unaweza kukataliwa.
Sign Up