Inapakia
Uumbizaji, Nyimbo, Wachangiaji, Hariri - Kila kinachohitajika ili kusimamia maudhui yako ya DistroKid!
Inapakia Toleo See all 19 articles
-
Je, Napakiaje Toleo kwenye DistroKid?
Ni rahisi SANA kupakia muziki wako kwenye DistroKid!
Ili kuanza, nenda tu kwenye fomu ya kupakia ya DistroKid:
http://www.distrokid.com/newKuanzia hapo tutakuongoza kwa kila kitu unachohitaji kufanya!
Ikiwa una maswali yoyote mahususi, tafadhali angalia makala hii kwa uchanganuzi wa kila sehemu ya fomu ya kupakia na makala yanayoendana na hiyo:
-
Kuwasilisha Wakati wa Likizo na Usaidizi
Wakati wa msimu wa Likizo, DistroKid huwa na upungufu wa wafanyikazi, hususani wakati wa wiki ya kazi ya Thanksgiving, wiki za kazi kabla ya likizo ya Krismasi, na vile vile siku ya Mwaka Mpya.
Huwa tunajaribu kujibu maombi yenu haraka iwezekanavyo! Kwa kawaida, huwa tunajibu maombi mengi ndani ya saa 24, lakini wakati wa Likizo, inaweza kutuchukua takriban siku 2-7 za kazi ili tuweze kufuatilia.
Vilevile wengi wa Washirika wetu wa huduma huwa na idadi pungufu ya wafanyikazi wakati wa likizo, jambo ambalo linaweza kuathiri muda wa kutoa maudhui yako.
Washirika wetu wa huduma wametoa ratiba ya jumla ya muda wa kutoa matoleo wakati wa Likizo, ili wasanii waweze kupanga matoleo yao ipasavyo.
Ikiwa unapanga kutoa muziki kati ya tarehe 29 Novemba 2024 na Januari 3, 2025, tafadhali zingatia tarehe za mwisho kuwasilisha zilizo hapa chini.
Ili kuhakikisha kuwa huduma zinapata mawasilisho yote ifikapo 11:59 p.m. PST kwa tarehe husika, ni bora kupakia angalau wiki mbili kabla. Hata hivyo, upakiaji unaofanyika wiki 3-4 kabla ya tarehe ya kutolewa utahakikisha kuwa tarehe yako ya uwasilishaji itafikiwa na toleo lako litapatikana hewani bila matatizo yoyote.
Tarehe ya Kutoa Tarehe ya mwisho ya Kuwasilisha Novemba 29, 2024 Novemba 22, 2024 Desemba 6, 2024 Novemba 22, 2024 Desemba 13, 2024 Desemba 6, 2024 Desemba 20, 2024 Desemba 13, 2024 Desemba 27, 2024 Desemba 20, 2024 Januari 3, 2025 Desemba 27, 2024 Muziki utakaowasilishwa baada ya tarehe hizi za mwisho huenda usipatikane ifikapo tarehe ya kutolewa inayotarajiwa.
Tunashukuru kwa uvumilivu wako, na tunatumai utakuwa na msimu wa likizo ulio na furaha, salama na wa kusisimua!
Go to article -
Je, Naweza Kubainisha Tarehe ya Siku za Usoni ya Kutoa Kazi ?
Ndiyo! Unaweza kuweka tarehe maalum, ya siku za usoni ya kutoa kazi zako ikiwa una mpango wa "Musician Plus" au "Ultimate".
Hii hapa ni video yenye maelekezo ya haraka kuhusu jinsi ya kuweka tarehe za matoleo yajayo:
Ikiwa tayari una akaunti ya DistroKid na unataka kupandisha uanachama, ingia na bofya "pandisha uanachama."
Unaweza kutumia tarehe ya zamani ya kutoa kazi, ili kuonyesha albamu au singo iliyotolewa awali.
Bofya hapa kwa maelezo zaidi kuhusu tarehe maalum za kutolewa.
-
Nyongeza za Albamu Ni Nini?
Nyongeza za Albamu ni manufaa ambayo una hiari ya kuyajumuisha au kutoyajumuisha kwenye upakiaji wako wowote! Hayahitajiki kufikisha muziki wako madukani (isipokuwa kwa leseni za kava, ikiwa unataka kusambaza kava) lakini husaidia kufanya muziki wako kufikiwa zaidi na mashabiki wako!
Kwenye fomu ya kupakia, unaweza kuchagua kwenda chini ya ukurasa, kabla ya kuwasilisha albamu yako!
Kwa matoleo yaliyopo, unaweza kuchagua kutokea kwenye ukurasa wa albamu yako, tembeza hadi chini ya ukurasa!
Baadhi ya Nyongeza za Albamu ni malipo ya mara moja, ilhali zingine zinatokana na usajili wa malipo, kama vile malipo yetu ya uanachama.
Discovery Pack: $0.99 kwa wimbo/mwaka
Fanya iwe rahisi kwa watu kuitambua singo hii wanapoisikia kwenye redio/TV, madukani, migahawani, kwenye sherehe n.k. Discovery Pack pia inajumuisha majukwaa ya kutambua ikiwa ni pamoja na ACRCloud, Jaxsta, Gracenote, na Luminate.Store Maximizer: $7.95 kwa albamu/mwaka
DistroKid itawasilisha singo hii moja kwa moja kwenye maduka mapya ya mtandaoni na huduma za utiririshaji kadri tunayaongeza. Ambayo ni mara nyingi. Tutakupa taarifa kabla ya kuongeza.Social Media Pack: $4.95 kwa singo/mwaka, $14.95 kwa albamu/mwaka, + 20% ya mapato ya matangazo ya YouTube
Pata taarifa na ulipwe muziki wako ukiwahikutumika katika video zozote za YouTube au TikTok. Tutaongeza nyimbo zako kwenye hifadhidata za YouTube na TikTok, na kutafuta utumizi mara kwa mara. Muziki wako ukigunduliwa katika video yoyote ya YouTube, utapokea taarifa—na mapato ya matangazo yatakujia moja kwa moja, badala ya mtu aliyepakia video. Tazama video ya YouTube inayoelezea Content IDUtoaji Leseni za Nyimbo za Kava
$12 kwa wimbo wa kava, kwa mwaka. Kwa maelezo zaidi kuhusu leseni za kava za DistroKid, tafadhali angalia makala ya Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara: https://support.distrokid.com/hc/sw/articles/360013648953
Acha Legacy: $29.00 kwa singo, $49.00 kwa albamu yenye nyimbo 2 au zaidi (ada isiyojirudia)
Nyongeza ya "Leave a Legacy" inaweza kuongezwa kwenye toleo ili lisiondolewe kwa sababu ya kuchelewa kwa malipo ya uanachama (ikiwa kadi yako ya mkopo imekataliwa, n.k.).
Zaidi ya hayo, ukiamua kusitisha usajili wako wa malipo, matoleo yoyote ambayo yana nyongeza ya Leave a Legacy yatasalia katika maduka na huduma za utiririshaji, hata ukifuta akaunti yako.
Kuongeza kipengee hiki cha ziada kwenye toleo hakuchukui nafasi ya ada yako ya kila mwaka ya uanachama ikiwa una usajili unaoendelea, na si malipo ya mara moja kwa matoleo yako yote: kila toleo lazima lijumuishe kipengee hiki cha ziada ikiwa ungependa kughairi usajili wako na kuweka matoleo yako yakiwa yameorodheshwa katika huduma za utiririshaji.
Dolby Atmos: $26.99 kwa kila wimbo
Hutambua toleo kama Dolby Atmos kwenye vifaa vinavyoitumia na huduma za utiririshaji ikiwemo Apple Music, TIDAL, na Amazon.
Usawazishaji Ukubwa wa Sauti: $2.99 kwa ada ya wimbo mara moja (isiyorudiwa)
Unapokichagua kipengele hiki cha ziada ambacho ni cha hiari, DistroKid itasawazisha kiwango na nafasi kwa ukingo wa sauti yako kiotomatiki viwe sawa na mipangilio inayopendekezwa na Spotify, -14dB iliyounganishwa LUFS na kiwango halisi cha juu zaidi (true peak maximum) cha -1dB. Sauti yako mpya iliyosawazishwa itatumwa kwa huduma zote za utiririshaji ulizochagua.
Kumbuka: Mambo fulani kama vile faili za sauti, uorodheshaji wa nyimbo, aina, lugha, Nyongeza za Albamu na ISRC haziwezi kubadilishwa kupitia sasisho la metadata. Ili kubadilisha mambo haya, utahitaji kufuta na kupakia upya toleo lako. Hivi ndivyo jinsi ya kufuta toleo lako kutoka kwa maduka: https://support.distrokid.com/hc/sw/articles/360013649193.
Ukishafuta toleo lako, tafadhali nenda kwa fomu ya kupakia kupakia upya toleo lililosahihishwa.
Go to article -
Je, Italeta Matatizo Endapo Kuna Msanii Mwingine Mwenye Jina Linalofanana Na Langu?
Kwa sababu zilizo wazi, unapaswa kutumia jina la msanii/bendi ambalo halipo katika huduma za utiririshaji. Kuwa na wasanii kadhaa wenye jina sawa husababisha kila aina ya mkanganyiko. Hebu fikiria kama pangekuwa na Led Zeppelins wawili, au Dave Matthews wawili (jina la kawaida bila shaka).Go to article
Lakini wakati mwingine jambo hili haliwezi kuepukika. Haya ni maswali makuu ambayo watu huuliza wakati kunapokuwa na msanii mwingine mwenye jina sawa na wao.
Je, nitalipwa? Au, huyo mtu mwenye jina sawa na mimi atalipwa kwa vipakuliwa vyangu?
Utalipwa kwa vipakuliwa vyako. Kiteknolojia, majina ya wasanii hayategemei kabisa ufuatiliaji wa mapato. Hivyo basi, wote mpo vizuri na hakuna cha kuhofia.
Albamu zangu zinaorodheshwa sambamba na albamu za wasanii wengine. Kwa hivyo inaonekana kama sisi ni mtu mmoja. Je, unaweza kuzitenganisha?
Wakati mwingine majukwaa ya kutiririsha muziki huwaweka pamoja wasanii walio na majina sawa (au yanayofanana), au huunda ukurasa mpya wa msanii badala ya kutumia ukurasa wako uliopo. Tunaweza kusaidia!
Tafadhali tembelea https://www.distrokid.com/fixer, ambapo tutakusaidia katika ufanyaji wa marekebisho husika!
Kwa hakika, ikiwa mtu tayari ana jina, unapaswa kuja na jina tofauti. Katika ulimwengu wa waigizaji, kwa mfano, hakuna waigizaji wawili wanaoruhusiwa kuwa na jina moja na wote wakiwa kwenye Chama cha Waigizaji, yaani SAG. Ndiyo maana Samuel L. Jackson ni Samuel L. Jackson, na sio Sam Jackson au Samuel Jackson -- majina hayo tayari yamechukuliwa. Ikiwa unataka kuonekana mwenye weledi, vumilia na upate jina tofauti ikiwa lako tayari limechukuliwa. -
Je, ninaweza kupakia toleo kwa njia ya "Waterfall", ambapo nyimbo mpya zinaongezwa kwenye albamu iliyopo?
Kwa sasa haiwezekani kutoa albamu kwa mtindo wa "waterfall", ambapo ukurasa wa albamu unajazwa kwa nyimbo mpya zinazotolewa katika tarehe maalum hadi kutolewa kwa albamu kamili. Lakini ikiwa unatazamia kutoa singo kila baada ya muda kisha kuzikusanya zote pamoja hapo baadae na kuzipakia kama albamu kamili, unaweza kutumia mbinu mbadala ya mkakati huu kwa kutumia matoleo kadhaa.
Kuna njia mbili za kufanya hivyo kwa kutumia DistroKid:
- Pakia albamu kamili iliyo na singo zote zikiwa na tarehe ya kutolewa iliyopangwa kwa siku zijazo, ambayo itatengeneza misimbo ya ISRC kwa ajili ya nyimbo. Baada ya upakiaji huu, unaweza kupakia singo hizo moja moja kwenye akaunti yako na kila singo ikiwa na tarehe yake ya kutolewa, huku ukiweka misimbo iliyopo ya ISRC kwenye fomu ya kupakia kwa kutumia chaguo la "tayari ina msimbo wa ISRC?". Au...
- Unaweza kwanza kutoa singo zako moja moja kwa kuzipakia kwenye DistroKid kila moja peke yake, na kisha tumia ISRC zinazozalishwa kwa singo hizi katika upakiaji wa albamu kamili hapo baadaye.
Katika hali yoyote, uko huru kufuta singo hizo kutoka kwenye maduka mara tu albamu inapotolewa, au kuziacha hewani pamoja na albamu!
Maelezo ya umbizo See all 25 articles
-
Je, ni Maumbizo Yapi ya Mafaili ya Sauti NinaYoweza Kupakia?
Mafaili ya sauti yanapaswa kuwa WAV, MP3, M4A, FLAC, AIFF, au Windows Media (WMA).
Ikiwa unatuma WAV, 16-bit, 44.1 kHz WAV ndiyo kiwango cha kawaida lakini kingine chochote kinafaa.
Ukubwa wa juu zaidi ambao DistroKid itakubali ni GB 1. Ikiwa una wimbo mkubwa kuliko huo, zingatia kuubadilisha kuwa na umbizo la FLAC kabla ya kupakia kwenye DistroKid. FLAC ni umbizo zuri, lisilopoteza ubora (ubora wa sauti sawa na WAV) lakini faili ni ndogo.
Nyimbo zinazopakiwa kwenye DistroKid lazima muda wake uwe chini ya saa 5 (dakika 300), na jumla ya nyimbo kwenye albamu zisizidi saa 10 (dakika 600). Zaidi ya hayo, albamu haziwezi kuwa na nyimbo ambazo kwa wastani urefu wa wimbo upo chini ya sekunde 60.
Tafadhali tazama hapa kwa maelezo maalum kuhusu kupakia kupitia iOS:
https://support.distrokid.com/hc/sw/articles/1500006315162 -
Je, Ni Yapi Mahitaji ya Mchoro wa Albamu?
Mchoro unapaswa kuwa katika faili la umbizo la .jpg. Mahitaji ya kipimo cha chini kwa mchoro wa albamu ni pikseli 1000x1000. Kimsingi, mchoro wa albamu unapaswa kuwa na umbo mraba, na pikseli 3000x3000. Ikiwa mchoro wako ni mdogo sana, au una umbo mstatili, tutaurekebisha kiotomatiki kwa ajili yako--lakini kuna hatari kwamba toleo letu lililorekebishwa halitaonekana sawa na ulivyokusudia.
Tafadhali pia hakikisha kwamba mchoro wako uko katika nafasi ya rangi ya RGB. Kwa kawaida hili sio suala la kufikiria -- kila kamera ya kidijitali na programu za kurekebisha picha (kama Photoshop) zinakuwa kwenye RGB. Hivyo, upo vizuri.
Hata hivyo, wakati mwingine kwa sababu yoyote ile, unaweza kuwa umehifadhi mchoro katika nafasi ya rangi ya CMYK au Grayscale, na DistroKid inakupa ujumbe wa hitilafu. Hili likitokea kwako, hifadhi upya mchoro wako katika umbizo la RGB.
Endapo unatumia Photoshop, bofya hapa kuona jinsi gani. Ikiwa huna Photoshop, kupakiaji na kuhifadhi upya faili lako kwa kutumia Kihariri cha Pixlr itaibadilisha kiotomatiki na kuwa RGB.
Huduma za utiririshaji zitakataa mchoro wenye
- Anwani ya tovuti (URL)
- Jina la Twitter
- Maneno 'Pekee' au 'Toleo Lenye Ukomo'
- Picha yoyote yenye ukungu, pikseli zinazoonesha, iliyozungushwa, au zenye ubora duni
- picha zisizo na leseni/picha zenye leseni za kibiashara
- Bei
- Nembo za huduma za kutiririsha (kama vile iTunes au Spotify)
- Uchi
- Mambo machafu
- Marejeleo ya midia halisi (mfano: "CD" au "Compact Disc")
Aidha, tafadhali usitumie mchoro mmoja kwa albamu nyingi. Mchoro wa albamu unaojirudia unaweza kukataliwa.
-
Je, Naweza Kupakia Jina la Wimbo/Albamu/Msanii kwa herufi kubwa zote au herufi ndogo?
Ndiyo! Unaweza kutumia herufi kubwa/mtindo ambao unataka kwa jina la msanii wako, vyeo, n.k.
Tafadhali kumbuka kwamba ukichagua utumiaji usiofuata viwango kwa kutumia herufi kubwa na ndogo kwenye toleo lako, utaona onyo hili kwenye fomu ya kupakia.Hiyo ni kwa sababu baadhi ya huduma za utiririshaji hazipendi staili hii, na huenda wakabadilisha kwenda staili inayofuata viwango, kwa mujibu wa miongozo yao ya staili. Ikiwa huduma haziruhusu matumizi ya herufi yasiyofuata viwango vya uandishi, huenda tukashindwa kuomba marekebisho.
-
Majukumu ya Msanii Ni Nini?
Majukumu ya msanii ni vitambulishi unavyoweza kutumia kuonesha huduma za utirishaji ni majukumu yepi msanii fulani alifanya katika utengenezaji au utumbuizaji wa toleo husika. Majukumu haya yanaweza kuonyeshwa katika ngazi ya wimbo au ya albamu. Huduma za Utiririshaji yanakubali majukumu yafuatayo ya msanii kutoka DistroKid:
Msanii wako wa Albamu
Msanii wa Albamu au "mtumbuizaji" ndiye msanii mkuu kwenye ngazi ya albamu. Kwa mfano, kwenye albamu ya Kendrick Lamarya DAMN., "Kendrick Lamar" ndiye Msanii wa albamu hii.
Msanii Mkuu
Msanii mkuu ni msanii muhimu zaidi katika ngazi ya wimbo. Mara nyingi hii hujumuisha Msanii wa Albamu pamoja na wasanii wengine wakuu kwenye wimbo. Jukumu la msanii mkuu hutumika kuonyesha ushirikiano. Kwa mfano kwenye albamu ya Moore Kismet ya Vendetta for Cupid, Moore Kismet ndiye Msanii wa Albamu katika ngazi ya albamu. Katika ngazi ya wimbo kwa wimbo kwenye albamu Rumor, WYN ni Msanii Mkuu wa ziada na Moore Kismet ni Msanii Mkuu.
Msanii aliyeshirikishwa
Msanii aliyeshirikishwa ni msanii yeyote anayesaidia katika uimbaji wa wimbo lakini si katika ngazi ya msingi kama ya msanii mkuu. Wasanii walioshirikishwa hujitokeza katika aya au kama wanavokali kwenye wimbo. Mfano, kwenye SOS (feat. Aloe Blacc) ya Avicii, "Aloe Blacc", ambaye anaimba kwenye wimbo huo, ni msanii anayeshirikishwa kwenye wimbo, ilhali "Avicii" ndiye Msanii Mkuu na wa Albamu.
Mtengeneza Remix
Msanii ambaye ametengeneza remix ya kazi asili. Mfano, kwa Love That Never (IMANU Remix) - TOKiMONSTA, "IMANU", ambaye alitengeneza remix ya wimbo huo, ndiye Mtengeneza Remix wa wimbo huu, ilhali "TOKiMONSTA", ambaye alikuwa msanii mkuu wa wimbo asili, bado ameorodheshwa kama msanii mkuu kwenye remix.
Mtayarishaji
Jukumu la mtayarishaji limebadilika zaidi na kukua katika miaka ya hivi punde, lakini kwa wakati huu, angalau katika Spotify, majukumu ya mtayarishaji msanii yameorodheshwa chini ya wachangiaji kwa wimbo. Kwa mfano, kwenye Buddy Holly - Weezer, "Ric Ocasek" ndiye mtayarishaji. Unaweza kuona waliochangia kwa utayarishaji kwa kubofya kitufe cha kulia kwenye kijipanya kwenye wimbo kwenye programu yako ya kompyuta na kuchagua "Onyesha Waliochangia"
Vidokezo vya kupakia!
Endapo una nyimbo chache kwenye toleo lako lenye wasanii wengi, lakini nyingi zimefanywa na msanii mmoja, tafadhali orodhesha tu msanii atakayeonekana katika kila wimbo katika Sehemu ya "Jina la Msanii/bendi". Hii itaashiria Msanii wako wa Albamu kwa toleo hilo. Kwa nyimbo zenye msanii zaidi ya mmoja, utaorodhesha wasanii wa ziada (Walioshirikishwa, Mtengeneza Remix, Msanii Mkuu wa Ziada) kwenye ngazi ya wimbo.
Ikiwa ushawahi kupakia kwenye DistroKid hapo awali, kisanduku cha kuingiza jina la Msanii/bendi kwenye fomu ya kupakia ya DistroKid kitakuwa na jina la msanii lililotumika mwisho kama chaguomsingi. Iwapo unataka kutumia jina tofauti la msanii (na una nafasi za wasanii zinazoweza kujazwa kwenye mpango wako), andika tu jina au majina ya msanii ambayo ungependa kutumia.
Go to article -
Je, Naweza Kuongeza Msanii Aliyeshirikishwa kwenye Wimbo Wangu?
Kabisa!
Kwa vipakiwa vipya, kwenye fomu ya kupakia katika kiwango cha wimbo, chagua tu "Ndiyo, ongeza wasanii walioshirikishwa kwenye jina la wimbo (tafadhali taja...)"
Ingiza majina ya wasanii wako walioshirikishwa, na ikiwezekana, taarifa zao zilizopo Spotify na Apple Music kwenye sehemu ya Uunganishaji Msanii Aliyeshirikishwa inayopatikana chini ya fomu ya kupakia, na hivyo tu! Umeongeza msanii aliyeshirikishwa kwenye wimbo wako!
Kwa matoleo yaliyopo, ikiwa unahitaji kuongeza au kuhariri msanii aliyeshirikishwa, nenda kwenye ukurasa wa albamu yako, kisha bofya hariri toleo.Chagua "Ongeza msanii mwingine aliyeshirikishwa" na chagua Shirikisha kutoka kwenye menyu kunjuzi, kisha ingiza taarifa zako za msanii aliyeshirikishwa.
Kuongeza msanii aliyeshirikishwa hakuhitaji nafasi zozote za ziada za msanii (hiyo ni nzuri!).
Tafadhali kumbuka kwamba ikiwa una msanii yule yule aliyeshirikishwa kwenye nyimbo zote za albamu ya nyimbo nyingi, huduma za utiririshaji zinahitaji aorodheshwe kama Msanii Mkuu.
-
Kwa nini umbizo ambazo hazijapoteza ubora (kama WAV na FLAC) ni bora kuliko MP3?
Umbizo ambazo hazijapoteza ubora kama vile WAV na FLAC hutoa ubora wa juu wa uzalishaji mpya sauti kuliko MP3, kwa kuwa zinahifadhi data zake za asili na tofauti ndogo asili ya rekodi, bila ya mgandamizo wa faili lililopoteza kiasi cha ubora.
MP3 ni umbizo la sauti lililogandamizwa, na kupoteza kiasi cha ubora wake--ikiwa na maana kwamba baadhi ya data za sauti zimeondolewa ili kupunguzwa ukubwa wa faili. Ingawa MP3 ni umbizo la sauti maarufu na linalotumika sana, haliwezi kulinganishwa na ubora wa sautiza umbizo zisizopoteza ubora.
DistroKid inakubali umbizo nyingi za mafaili, ikiwa ni pamoja na WAV, FLAC na MP3. Lakini ikumbukwe kwamba msanii anapaswa tu kupakia muziki katika umbizo la MP3, ikiwa msanii ameridhika na ubora wa sauti ya MP3 yake na anataka kuitumia kwa usambazaji.
Hatimaye, ni juu ya msanii mwenyewe kuamua ni umbizo gani la kutumia kwenye muziki wake. Lakini wanapaswa kufahamu kuwa kutumia umbizo ambalo halijapoteza ubora wake wa asili kama vile WAV au FLAC kunaweza kutoa sauti yenye ubora wa juu zaidi na kuhakikisha kuwa muziki wao unakidhi viwango vya wasikilizaji tofauti.
Go to article
Kufanya marekebisho See all 13 articles
-
Kutumia Audio Swap kubadilisha faili ya sauti
Ukiwa na kipengele cha Audio Swap (Mpango wa Ultimate pekee), unaweza kubadilisha faili la sauti kwa toleo lililopo hewani tayari huku ukidumisha takwimu zako, orodha za kucheza ulizomo, mgawanyo na metadata asili.
Audio Swap inapaswa kutumiwa ikiwa unahitaji kubadilisha faili la sauti na kuweka lililo na marekebisho kidogo, kama vile kuondoa kelele au boresho mpya/lililosasishwa. Haipaswi kutumiwa ikiwa faili lako mpya la sauti lina mabadiliko mengi ya ubunifu, kama vile remix au iliyo na vipengele vipya vya muziki.
Unaweza kufikia kipengele cha Audio Swap kwa kwenda kwenye menyu ya Vipengele kwenye kona ya juu kulia ya DistroKid, na kuchagua "Vinasaidia Vinapohitajika," kisha chagua "Audio Swap". Unaweza pia kutembelea https://distrokid.com/audioswap moja kwa moja.
Mahitaji ya Faili ya Sauti
Faili za sauti zinaweza kubadilishwa kwa kutumia Audio Swap kwa marekebisho kidogo (kama vile kuondoa kliki/popu au kupunguza sauti za 's') au marekebisho ya kuboresha (kama vile kusawazisha sauti au kupunguza kelele).
Huwezi kubadilisha faili la sauti kwa toleo ikiwa faili mpya:
- Ni remix, toleo mbadala, au rekodi mpya
- Ni toleo lililorekebishwa la sauti asili (utangulizi mpya, mwisho uliorefushwa, n.k.)
- Imebadilishwa kwa vipengele vipya vya uzalishaji (vyombo vipya, madoido ya sauti yaliyobadilishwa, n.k.)
Ukiwasilisha faili isiyoruhusiwa kwa audio swap, utaarifiwa.
Kutumia Audio Swap
Ili kutumia zana ya Audio Swap pale https://distrokid.com/audioswap, chagua toleo lenye wimbo unaotaka kubadilisha kutoka kwenye menyu kunjuzi ya kwanza. Kisha, chagua wimbo unaotaka kubadilisha sauti katika menyu kunjuzi ya pili.
Ukishachagua wimbo, bofya "Chagua faili ya sauti" chini ya sehemu ya "Pakia faili yako mpya ya sauti". Hii itakuruhusu kuvinjari faili za kifaa chako ili kuchagua faili mpya ya sauti. Ukishachagua faili, bofya kitufe cha "Badilisha faili ya sauti" ili kuwasilisha faili na ombi la kubadilisha.
Baada ya faili mpya kuwasilishwa, itasasishwa katika huduma baada ya siku chache. Ikiwa faili mpya hairuhusiwi kama badilisho, utaarifiwa.
Go to article -
Je, Naweza Kubadilisha Toleo Mara Linapokuwa Limepakiwa?
Ndio! Unaweza kufanya uhariri kwa kutembelea ukurasa wa albamu yako, na kubofya "Hariri Toleo". Tutakuelekeza katika kila kitu hatua na utaweza kuhariri kutokea hapo.
🚨Kumbuka: Kwa maelezo kuhusu kubadilisha chapa au kubadilisha jina lako la msanii, tafadhali tembelea haya makala.Je, Ni Uhariri wa Aina Gani Ninaoweza Kufanya?
Aina za uhariri unazoweza kufanya hutofautiana kutoka wimbo hadi wimbo kutegemea na toleo lako na kiwango cha mpango wako, lakini kwa ujumla unaweza kuhariri yafuatayo:
-
Jina la Msanii/Bendi
- Kuongeza au kuondoa washirika katika ngazi ya Albamu
- Jina la albamu
- Lebo ya Kurekodi
- Tarehe ya kutolewa
- Hali ya uagizaji wa mapema na tarehe ya kuanza kuagiza mapema
- Jalada la albamu / Mchoro wa Albamu
- Majina ya nyimbo
- Maelezo ya toleo la wimbo
- Ikiwa mistari ya wimbo ni chafu au hapana
- Muda wa kuanza kipande cha wimbo
- Kufuta toleo kutoka kwenye huduma za utiririshaji
Je, kuna mambo ambayo siwezi kuhariri?
Yafuatayo hayawezi kubadilishwa kupitia sasisho la metadata:
- Mafaili ya sauti (pamoja na kubadilisha na Toleo la Mixea au kuongeza mafaili ya Dolby Atmos ya toleo lako)
- Mpangilio wa Nyimbo / Orodha
- Lugha ya toleo
- Kuondoa Nyongeza za Albamu
- Aina
- ISRCs
Ili kuyabadilisha, utahitaji kufuta toleo lako na kupakia upya toleo lililosahihishwa.
Je, maombi ya kuhariri huchukua muda gani?
Kwa kawaida huduma za utiririshaji huchakata maombi haya ndani ya siku chache, lakini tafadhali fahamu kwamba masasisho ya metadata yanaweza kuchukua kuanzia wiki 1-2 kwa mabadiliko kukamilika kwenye huduma zote za utiririshaji.
Huduma za Utiririshaji pia hazikuruhusu kupakia, kufuta, na kisha kupakia upya kwa kutumia metadata tofauti (jina la msanii, jina la wimbo, n.k.). Hata kama umefuta toleo la awali na kujaribu kupakia upya na marekebisho yake, huduma hazitaruhusu upakiaji mwingi wenye metadata zinazokinzana.
Iwapo unahitaji kuondoa toleo lako kutoka kwenye huduma fulani, kuliondoa kutoka nchi mahususi, kubadilisha aina ya muziki au aina ndogo au kubainisha msanii kama mtengeneza remix, wasiliana nasi na tunaweza kusaidia.
Go to article -
Jina la Msanii/Bendi
-
Je, Naweza Kubadilisha Jina Langu la Msanii?
Jibu fupi: Unaweza kubadilisha jina lako la msanii kwenye huduma zote isipokuwa iTunes/Apple Music kwa kutembelea ukurasa wa albamu yako, na kubofya "Hariri Toleo". Unaweza hata kuhariri jina lako la msanii kwenye matoleo yako yote kutoka kwenye ombi moja la kuhariri albamu!***
Jibu refu: Kubadilisha jina lako la msanii ni mchakato mrefu na mgumu ambao wakati mwingine unaweza kusababisha matatizo zaidi kuliko inavyotatua, na sio huduma zote zinaruhusu uwekaji upya wa chapa. Ni wazi, sote tunaelewa hisia za msanii na kutaka kujiwakilisha kwa usahihi zaidi na mradi wako wa msanii, lakini pia tunataka kuhakikisha kuwa unakuwa na taarifa zote unazohitaji ili kufanya uamuzi unaotokana na kuwa na ufahamu zaidi kwa kadri iwezekanavyo kabla ya kufanya mabadiliko kwenye miradi yako iliyopo ambayo itakuwa ni vigumu kubadili nia na inaweza kusababisha maswala mengi. Apple Music haikubali maombi ya kubadilisha chapa kwa sasa. Unaweza kupata maelezo zaidi juu ya hilo hapa.Mambo ya kuzingatia:
-
Marekebisho ya jina la msanii na/au ya chapa yanaweza tu kuombwa kwenye matoleo ambayo yapo hewani kwa sasa
Huduma za utiririshaji haziruhusu matoleo ambayo tayari yamewasilishwa kuwasilishwa upya na metadata tofauti (Jina la Msanii na Majina ya Nyimbo). Ili kuwasilisha tena toleo lolote ambalo tayari limeorodheshwa katika huduma za utiririshaji, ni lazima liwasilishwe upya likiwa na Jina asili la Msanii na Majina ya Nyimbo.
Iwapo umefuta kazi yako kwa lengo la kuhariri au kubadilisha chapa ya Jina lako la Msanii, kumbuka kwamba, njia pekee ya kufanya hivyo, ni kupakia tena kazi yako na metadata za asili, kisha omba kuhaririwa kwenye hiyo kazi iliyopakiwa upya mara tu inapowasilishwa tena katika huduma za utiririshaji. -
Kuhifadhi wafuasi na wasikilizaji wa kila mwezi
Unapotuma ombi la kubadilisha jina lako la msanii, tafadhali kumbuka kwamba huduma nyingi za utiririshaji zitatengeneza ukurasa mpya wa msanii kwa ajili yako badala ya kusasisha maelezo ya kwenye ukurasa wako wa msanii uliopo. Kwa huduma za utiririshaji zinazofanya hivi, hatuwezi kuomba kwamba ukurasa wako wa msanii uliopo uhaririwe ili uendane jina lako jipya la msanii. Na matokeo yake, kuna uwezekano wasikilizaji na wafuasi wako wa kila mwezi wakashindwa kuhamishiwa kwenye ukurasa wako mpya wa msanii. -
Kuhifadhi idadi za kucheza na orodha za nyimbo
DistroKid haiwezi kutoa hakikisho lolote, lakini kwa ujumla ikiwa tu unahariri metadata ya toleo lililopo kupitia nyenzo yetu ya uhariri (yaani kutobadilisha ISRC), idadi yako ya mara ngapi wimbo ulisikilizwa na uwekaji wa orodha za nyimbo zinapaswa kuhamishwa. Lakini hata hivyo, sio jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wa DistroKid. -
Inaweza kuchukua muda kwa maduka yote kusasisha jina lako la msanii
Wakati uwasilishaji wa ombi lako la kutengeneza chapa mpya ni mchakato wa kiotomatiki, usimamizi halisi wa data na masasisho ya metadata ya ombi lako la kutengeneza chapa mpya; hayajakamilika kiotomatiki, na mengi ya maombi haya yanahitaji wanadamu (sio kompyuta) kuyakamilisha ipasavyo.
Hii inamaanisha nini:
Kutegemea na idadi iliyopo ya maombi ya kubadilisha chapa, inaweza kuchukua hadi wiki kadhaa kwa maduka yote kusasisha maudhui yako yaliyopo na kuonyesha jina lako jipya la msanii. Ikiwa unapanga kubadilisha chapa yako, tafadhali kumbuka hili.
-
Matoleo yasiyolingana
Kama unavyojua, DistroKid haina udhibiti wa mahali matoleo yako yametolewa kwenye huduma za utiririshaji. Ukihariri jina lako la msanii na ukurasa mpya wa msanii ukatengenezwa, matoleo yako yanaweza kugawiwa kwa ukurasa uliopo wa msanii ikiwa jina lako jipya sio la kipekee. Hilo likitokea, tafadhali tembelea https://www.distrokid.com/fixer, ambapo tutakuelekeza ili kuhakikisha mambo yanarekebishwa! -
Haiwezi kutuma maombi ya ziada ya kuhariri
Ukiamua kubadilisha jina lako la msanii katika huduma zote za utiririshaji, hutaweza kuwasilisha maombi zaidi ya kuhariri kwenye toleo lolote ambalo linatumia jina jipya la msanii uliloweka hadi ombi lako la kubadilisha jina likamilishwe. Kwa wakati huu, hakuna njia ya kuharakisha maombi haya -
Hakuna kurudi nyuma (ni kama)
Ukichagua kubadilisha jina lako la msanii, njia pekee ya kurejesha mabadiliko ni kuomba upya uhariri mwingine. Madhara yoyote ya ombi la awali hayatoi hakikisho la kutatuliwa kwa kubadilisha tu jina lako la msanii. (Ni uamuzi mkubwa!) 🧠
***Ni muhimu kutambua kwamba wakati wa kubadilisha jina, kazi zako zote lazima zifanyiwe marekebisho ili ziendane na jina jipya la msanii, vinginevyo baadhi ya huduma za utiririshaji zinaweza kuficha matoleo yanayoonekana kuwa na metadata zinayokinzana.
Njia bora: Sasisha jina lako la msanii kwa matoleo yako yote kwa kutumia "Sasisha matoleo yangu yote kutoka kwa [Jina la Msanii] ili kutumia nyenzo mpya ya jina la msanii" katika sehemu ya hariri toleo. Kumbuka kuwa nyenzo hii inapatikana tu kwa matoleo yenye msanii mkuu mmoja (sio ushirikiano).
Go to article -
-
Je, Nafutaje Toleo kutoka Kwenye Huduma za Utiririshaji?
Ili kufuta albamu au singo:
- Hakikisha umeingia katika akaunti yako ya DistroKid
- Bofya toleo unalotaka kufuta
- Bofya "Hariri Toleo"
- Teremka hadi chini, kisha bofya "Ondoa toleo hili kwenye maduka yote"
- Mara tu unapobofya kitufe, muda ambao huduma wanatumia kufuta ni karibu sawa na muda waliokuwa wametumia kuongeza albamu au wimbo husika.
- Tarajia kusubiri kuanzia wiki 1-2 ili kutoweka kutoka kwenye huduma zote, wakati mwingine mapema zaidi.
Uondoaji kwenye Spotify huchukua angalau siku 2 za kazi.
Uondoaji kwenye Anghami huchukua takriban saa 48.
-
Je, Naweza Kuondoa Toleo Langu Kutoka kwa Huduma Maalum ya Utiririshaji?
Ndiyo! Wasiliana nasi hapa, chini ya "Muziki Wangu" > "Hariri na Uwekaji Bei".
Ukibadilisha nia yako hapo baadaye, unaweza kuongeza toleo lako wakati wowote kwenye huduma zozote za utiririshaji kwa kuchagua "Ongeza kwenye maduka zaidi" kwenye ukurasa wa dashibodi ya albamu yako.
Tafadhali kumbuka: Pindi ombi lako litakapowasilishwa, tarajia kusubiri hadi wiki 1-2 ili toleo lako litoweke kutoka kwenye huduma za utiririshaji zilizochaguliwa, wakati mwingine huwa mapema zaidi. -
Je, akaunti nyingi za DistroKid zinaruhusiwa kupakia rekodi ile ile ya sauti?
Hapana.
Kutokana na jinsi huduma za utiririshaji zinavyolipa, na matatizo mengine, haturuhusu rekodi moja ya sauti kupakiwa na mtumiaji zaidi ya mmoja wa DistroKid.
Ikiwa umiliki wa wimbo umebadilishwa na ungependa kuelekeza mapato ya wimbo kutoka akaunti moja ya DistroKid hadi nyingine, tunaweza kufanya hivyo. Angalia kipengele chetu cha Mgawanyo Kwa Mgawanyo, unaelekeza mapato kwa yeyote—huku ukibaki na takwimu, nyongeza za orodha ya nyimbo, wafuasi wa Spotify, ISRC na metadata zingine zote bila kubadilika.
Utatuzi wa shida See all 10 articles
-
Msaada! Albamu/Singo Yangu Ilienda Hewani Kabla Ya Tarehe Yake Ya Kutolewa
Ikiwa toleo lako lilienda hewani katika majukwaa kabla ya tarehe uliyokusudia kutolewa, tafadhali hakikisha kuwa ulichagua mwaka sahihi kwa ajili ya tarehe ya baadaye ya kutolewa. Hili ni muhimu hasa kuelekea mwishoni mwa mwaka, unapopanga tarehe ya kutolewa iwe katika mwaka unaofuata.
Kwa mfano, ikiwa unapanga kupakia albamu au wimbo Oktoba 2024, ukiwa na nia ya kuitoa Januari 2025, lakini ikaenda hewani mara tu baada ya kuipakia, kuna uwezekano mkubwa kuwa mwaka haukuchaguliwa ipasavyo. Matokeo yake, mwaka wa kutolewa utakuwa mwaka wa sasa.
Ikiwa ulichagua mwaka usiostahili, unaweza kuhariri toleo lako ili kuchagua tarehe/mwaka sahihi, na toleo hilo litaondolewa kwenye huduma baada ya muda mfupi na kisha litaonekana tena katika tarehe iliyochaguliwa.
Ikiwa umethibitisha kuwa tarehe ya kutolewa ni sahihi lakini bado kuna tatizo, tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi ili kupata msaada.
-
Toleo Langu Lilikataliwa, Nitarekebisha vipi?
Ikiwa albamu yako ilikataliwa, utahitaji kulifuta na kupakia upya toleo lako ili kurekebisha chochote kilicholeta shida wakati wa ukaguzi, isipokuwa maduka yakihitaji uthibitisho - ukipokea ombi la kuthibitisha, tafadhali usifute upakiaji wako. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuthibitisha jina la msanii kwenye DistroKid, bofya hapa.
Ikiwa toleo lako lilikataliwa kwa sababu ya suala la mchoro, unaweza pia kubadilisha mchoro kwenye toleo lililopo ili kulirekebisha. Kwenye ukurasa wa albamu yako, bonyeza "Badilisha Kazi ya Sanaa" kwenye upande wa kulia wa sehemu ya Mchoro ili kusasisha mchoro wa albamu yako:Kwa maelezo zaidi kuhusu mahitaji ya mchoro wa albamu, bofya hapa.
Kumbuka, kila duka lina miongozo mahususi ya jinsi matoleo yanavyopangwa, na ni aina gani ya kazi watakazokubali.
-
DistroKid imeniomba Uthibitisho, Je! Nafanyaje Hilo?
Wakati mwingine, maduka humtaka msanii athibitishe jina lake la kisanii. Hili husaidia kulinda kazi zako kwenye DistroKid na ndani ya maduka, na kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayepakia muziki wako, au kutumia jina lako la kisanii bila idhini yako.
Ili kutoa ruhusa, msanii anahitaji kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia mojawapo ya njia hizi mbili:
1. Ikiwa msanii anatumia X, anaweza kutuma ujumbe mfupi ("DM") kwa @distrokid ili kuthibitisha. Katika DM, tafadhali taja UPC (au jina la albamu). Kitu kama "Ninathibitisha msanii kwa UPC". Kumbuka kuwa akaunti mpya ya X haiwezi kutumika kwa madhumuni ya uthibitisho. Au...
2. Picha ya leseni ya udereva au pasipoti ya msanii (unaweza kuziba taarifa binafsi kama vile anwani) pamoja na jina au UPC ya toleo linalohitaji uthibitisho.
Kumbuka: Ikiwa msanii anatofautiana na jina halali kwenye kitambulisho, tafadhali pia toa kiungo cha tovuti ambapo tunaweza kulinganisha jina hilo halali na msanii. -
Kwa nini Mafaili Yangu Yana Byte Sufuri?
Ukiona ujumbe unaosema "Faili ulilopakia ni byte sufuri," inamaanisha kuwa faili lako la sauti haliwezi kuchezwa. Wakati mwingine hii hutokea unapojaribu kupakia kwa kutumia kifaa cha mkononi, kama vile simu au hifadhi ya mtandaoni (cloud storage), kwa kuwa hifadhi ya faili inashughulikiwa tofauti na inavyokuwa kwa kompyuta iliyohifadhi faili husika. Utahitaji kusitisha jaribio la awali na kupakia upya toleo lako.
Ikiwa unapakia muziki wako kwa kutumia kifaa cha iOS, utahitaji kuhakikisha unachagua mafaili yako kutoka kwenye kivinjari cha faili cha iOS, vinginevyo unaweza kupata shida kupakia jalada la albamu yako au mafaili ya sauti, kama vile kuona ujumbe wa hitilafu ukisema kwamba " Faili uliyopakia ni byte sufuri."
Ukianzia kwenye Dashibodi yako ya DistroKid, chagua "Menyu", na kisha chagua "Pakia" ili kufika kwenye fomu ya kupakia.
Ukiwa kwenye fomu ya kupakia, jaza maelezo kwa kadri inavyohitajika. Unapofika sehemu ambayo unapakia mchoro, bofya kisanduku kinachosema "Chagua picha mpya". Kutoka hapa utapewa chaguo la kuchagua picha kutoka kwenye maktaba yako ya picha, kupiga picha, au kutafuta kwenye kivinjari cha faili cha kifaa chako cha iOS. Kwa wakati huu, ili kupakia mchoro wako kutoka kwenye kifaa cha iOS utahitaji kuchagua faili lako la mchoro kutoka kwenye kivinjari cha faili cha kifaa chako. Bofya "Browse".
Ukishachagua browse, utaletewa programu iliyopachikwa ya kutafuta Faili kwenye kifaa chako. Sasa unaweza kwenda mahali ambapo umehifadhi mafaili yako kwa ajili ya kupakiwa. Kwa kuangalia mfano huu, nimehifadhi faili langu la sauti na mchoro wa albamu kwenye folda la "Vipakuliwa" kwenye iPhone yangu.
Kutoka hapa, tunaweza kusonga chini kwenye fomu ya kupakia hadi tunapofika sehemu ambayo tutapakia faili la sauti. Ukifika sehemu ya "Faili la sauti" ya fomu ya kupakia, bofya "Chagua Faili". Utaletewa chaguzi tatu zilezile, na tena utahitaji kuchagua "Browse" ili kukupeleka kwenye kivinjari cha faili la iOS.
Ukishachagua faili lako la sauti, hapo unakuwa sawa kuendelea! Ukikumbana na changamoto, hakikisha kuwa unahifadhi mafaili yako kwenye kifaa chako cha iOS badala ya kuifadhi kwenye iCloud. Kwa sasa, fomu ya kupakia ya DistroKid haikubali upakiaji wa mafaili yaliyo kwenye hifadhi za mtandaoni, kwa hivyo utahitaji kupakia mafaili moja kwa moja kutoka kwenye kifaa chako cha iOS.
- Kwa nini Ukubwa wa Sauti ya Wimbo Wangu Unaonekana Tofauti kwenye Huduma za Utiririshaji?
-
Toleo Langu Limekwama kwenye Uchakataji
Je, toleo lako linaonekana kukwama kuchakatwa huku kukiwa na mduara wa manjano karibu na albamu/wimbo/mchoro wako? Hii kwa kawaida inamaanisha kuwa muda wa ziada wa uchakataji unahitajika.
Inaweza kuchukua siku kadhaa kwa albamu kukaguliwa, kuidhinishwa na kutumwa kwenye huduma za utiririshaji. Endapo ni muhimu kwa albamu yako kwenda hewani katika tarehe mahususi, bofya hapa kusoma kuhusu tarehe za kutolewa. Vinginevyo, kimsingi, toleo lako linapaswa kuenda hewani mara tu linapochukuliwa na huduma kulingana na ratiba ngumu hapa chini.
- iTunes/Apple Music: siku 1-7. Asilimia ndogo sana ya albamu kwenye Apple hupitia ukaguzi unaofanywa na watu halisi, ukaguzi ambao huchukua wiki za ziada 1-2 au zaidi.
- Spotify: siku 2-5
- Amazon: siku 1-2
- YouTube Music: siku 1-2.
- Deezer: siku 1-2
- TIDAL: siku 1-2
- Facebook/Instagram: wiki 1-2.
- TikTok: wiki 1 hadi 3.
Kumbuka: Ucheleweshaji ni nadra, lakini hutokea, na kwa kawaida ni jambo lililo nje ya uwezo wa moja kwa moja wa DistroKid.
Pandora ina mchakato wao wa ukaguzi wa ndani ili kuratibu maudhui, kwa hivyo hatuwezi kutoa maelezo mengi sana kuhusu muda ambao unaweza kuchukua matoleo kuongezwa kwenye vituo vya Pandora (ikiwa imeongezwa). Ili kujumuishwa katika Pandora Premium (huduma ya utiririshaji ya redio ya Pandora), tafadhali soma HAYA.
Bonasi: Kwa huduma nyingi za utiririshaji (iTunes, Amazon, YouTube Music, Spotify, na zaidi) tutagundua mara albamu yako inapoenda hewani, na hivyo kukutumia barua pepe yenye kiungo!
Tafadhali kumbuka: Kupata leseni za nyimbo za kava inaweza kuchukua hadi siku 14 za kazi. Matoleo yenye nyimbo za kava yatawasilishwa pindi tu leseni itakapoidhinishwa na Harry Fox Agency (ambao hushughulikia leseni zetu za kava).
ISRC // UPC See all 8 articles
-
Je, DistroKid Inatoa Misimbo ya ISRC?
Ndiyo.
Msimbo wa ISRC ni msimbo wa kipekee unaotolewa kwa kila wimbo unaopakia.
DistroKid imeteuliwa na Wakala wa ISRC Marekani kutoa ISRC, na itazalisha kiotomatiki misimbo mipya ya ISRC ya DistroKid kwa kila wimbo unaopakia. Hakuna malipo na huzalishwa kiotomatiki.
Endapo ungependelea kubainisha misimbo yako mwenyewe ya ISRC, unaweza kufanya hivyo ikiwa una akaunti ya "Musician Plus" au "Ultimate".
Maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia misimbo yako mwenyewe ya ISRC kwenye DistroKid.
-
Je! Nahitaji Kufahamu Msimbo wa ISRC au UPC Ni Nini ili Kutumia DistroKid?
Hapana.
ISRC na UPC ni misimbo inayotumika katika tasnia ya muziki. Inasaidia kutambua matoleo na nyimbo zako.
DistroKid imeteuliwa na Wakala wa ISRC Marekani kutoai ISRC, na itazalisha kiotomatiki misimbo mipya ya ISRC ya DistroKid kwa kila wimbo unaopakia. Hakuna malipo na hufanyika kiotomatiki, na utapokea 100% ya mapato.
Ikiwa ungependelea kununua UPC na ISRC zako mwenyewe, tembelea:
https://www.gs1us.org/
https://www.usisrc.org/Ikiwa una mpango wa usajili wa kulipia wa Musician Plus au Ultimate, unaweza kutumia ISRC zako mwenyewe wakati unapopakia.
-
Je, Naionaje UPC ya Toleo Langu?
UPC kwa urefu "Universal Product Code." Ni msimbo wa kipekee unaotumiwa kutambua bidhaa, kama vile albamu au singo.
UPC ya DistroKid inatengenezwa kiotomatiki kwa ajili yako, kila wakati unapopakia albamu. Ili kuiona UPC ya DistroKid:
- Ingia kwenye DistroKid
- Bofya albamu unayopendelea
- Tafuta "UPC" iliyoonyeshwa chini ya mchoro wako
UPC za DistroKid ni kwa ajili ya usambazaji wa kidijitali ndani ya DistroKid. Ikiwa unataka kutuma maombi ya UPC iliyotolewa na GS1, tafadhali wasiliana na ofisi ya GS1 iliyo karibu nawe hapa.
-
Tayari Nina Misimbo ya UPC na ISRC. Je, Naweza Kuitumia?
Ndiyo kwa Misimbo ya ISRC. Hapana kwa Misimbo ya UPC.
DistroKid imeteuliwa na Wakala wa ISRC Marekani kuzitoa ISRC, na itazalisha kiotomatiki misimbo mipya ya ISRC ya DistroKid kwa kila wimbo unaopakia. Hakuna malipo na huzalishwa kiotomatiki.
Lakini kama unataka kubainisha misimbo yako mwenyewe ya ISRC kwa sababu yoyote, hiyo ni rahisi kufanya:
(1) Hakikisha kuwa umejisajili kwa akaunti ya DistroKid ya "Musician Plus" au "Ultimate".
(2) Kisha bofya "tayari una msimbo wa ISRC?" kwenye fomu ya kupakia ya DistroKid.
Hakuna njia ya kubainisha msimbo maalum wa UPC.
Ikiwa unataka kutuma ombi la kupata UPC inayotolewa na GS1, tafadhali wasiliana na ofisi ya GS1 iliyo karibu nawe hapa.
Endapo ungependa kununua ISRC zako mwenyewe, tembelea https://www.usisrc.org/
-
Je, Nahitajika Kutoa Misimbo ya UPC au ISRC?
Hapana, huhitajiki kutoa misimbo ya UPC au ISRC kwa DistroKid.
DistroKid imeteuliwa na Wakala wa ISRC Marekani kuzitoa ISRC, na itazalisha kiotomatiki misimbo mipya ya ISRC ya DistroKid kwa kila wimbo unaopakia. Hakuna malipo na huzalishwa kiotomatiki.
Unaweza kubainisha misimbo yako mwenyewe ya ISRC ikiwa una akaunti ya Musician Plus au Ultimate.
Maelezo zaidi juu ya kutoa ISRC zako mwenyewe kwa DistroKid.
Ikiwa unataka kutuma ombi la kupata UPC inayotolewa na GS1, tafadhali wasiliana na ofisi ya GS1 iliyo karibu nawe hapa.
-
Je, Nipachike Misimbo Yangu ya ISRC Moja kwa Moja kwenye Mafaili Yangu ya Sauti?
Hapana.
Usijisumbue kupachika misimbo ya ISRC moja kwa moja kwenye mafaili yako ya sauti ya .wav (au umbizo lingine).
Ukifanya hivyo, haitaleta madhara yoyote. Lakini utapoteza muda, kwa sababu huduma za utiririshaji hupuuza data hizo.
Ikiwa unapendelea kutumia misimbo yako mwenyewe ya ISRC (badala ya misimbo ya ISRC ya DistroKid isiyo na malipo ambayo DistroKid hutengenezea kiotomatiki kwa ajili yako), ni rahisi. Bofya hapa kwa maelezo zaidi kuhusu kutumia misimbo yako mwenyewe ya ISRC.
Mistari See all 5 articles
-
Kwa Nini Mistari Yangu Ilikataliwa?
Huduma za utiririshaji zina mahitaji maalum ya kuwasilisha mistari yako:
- Usijumuishe jina la mwimbaji
- Usijumuishe maandishi ya ziada (mfano: "intro", "chorus", viunga vya mitandao ya kijamii, n.k.)
- Mistari inayorudiwa lazima iandikwe. Kwa mfano, usiandike "Chorus 2x" n.k.
- Anza kila mstari kwa herufi kubwa
- Usitumie alama za uakifishaji mwishoni mwa mstari isipokuwa alama za mshangao na kuuliza
- Usijumuishe mistari tupu isipokuwa kati ya aya na aya au kiitikio
- Epuka kuingiza mistari refu kupita kiasi. Sentensi moja kwa kila mstari
- Usidhibiti au kuondoa maneno machafu isipokuwa kama maneno husika yameachwa/yamefunikwa kwa sauti kwenye rekodi
Kwa mfano: Usiweke "Mse***", isipokuwa kama neno husika liliachwa au kuzibwa kwa sauti - Usiweke herufi za tarakimu kwa namba kati ya 1-10. Namba 2 lazima iandikwe kama mbili.
- Usiongeze nafasi za ziada mwanzoni au mwishoni mwa mistari
- Tumia tahajia sanifu (mfano: Tryna inapaswa kuandikwa kama Trying to)
Sababu za kawaida zinazofanya huduma za utiririshaji kukataa mistari ya wimbo ni:
-
Hakuna vigawa mstari kati ya sehemu na sehemu (mstari/kiitikio/daraja/n.k.)
Usiumbize mistari yako ifuatavyo:
So I pointed my fingers
And shouted few quotes I knew
As if something that's written
Should be taken as true
But every path I had taken
And conclusion I drew
Would put truth back under the knifeAnd now the only piece of advice that continues to help
Is anyone that's making anything new only break something elseWhen my time comes
Oh oh oh oh
When my time comes
Oh oh oh oh
Umbiza mistari yako ifuatavyo:
So I pointed my fingers
And shouted few quotes I knew
As if something that's written
Should be taken as true
But every path I had taken
And conclusion I drew
Would put truth back under the knifeAnd now the only piece of advice that continues to help
Is anyone that's making anything new only break something elseWhen my time comes
Oh oh oh oh
When my time comes
Oh oh oh oh
-
Vigawa mstari vingi mno (nafasi zisizo na maana kati ya kila mstari)
Usiumbize mistari yako ifuatavyo:
There's traffic on the bridgeThere's traffic on the bridge
But the skyline shines with a certain light
I know you're sick of it
Umbiza mistari yako ifuatavyo:
But the skyline shines with a certain light
I know you're sick of it
-
Makosa mengi sana ya kisarufi/tahajia/ uchanganyaji herufi kubwa na ndogo
Usiumbize mistari yako ifuatavyo:
2day is gona b the day
That their gonna throw it back to u
By now u shouldve some how
Realized what u gotta do
I dont believe that n e body
Feels the way I do about u now
Umbiza mistari yako ifuatavyo:
Today is gonna be the day
That they're gonna throw it back to you
By now you should've somehow
Realized what you gotta do
I don't believe that anybody
Feels the way I do about you now
-
Uakifishaji mwishoni mwa mistari
Usiumbize mistari yako ifuatavyo:
Everything is everything.
What is meant to be, will be.
After winter, must come spring.
Change, it comes eventually.
Umbiza mistari yako ifuatavyo:
Everything is everything
What is meant to be, will be
After winter, must come spring
Change, it comes eventually
Kwa orodha kamili kuhusu mahitaji ya mistari, tembelea Miongozo ya mistari ya Apple Music.
Ili kupata mistari iliyooanishwa kwenye Spotify, TIDAL na Instagram, chagua kujiunga na Lyric Blaster leo kwa kuwasilisha maneno ya mistari ya matoleo yako.
-
Je, mistari yangu itaonekana wapi?
DistroKid hutuma mistari yako kwa
- Apple Music
- YouTube Music
- LyricFind
- Matokeo ya Kutafuta kwa Google
- na zaidi
Unaweza pia kuchagua Lyric Blaster ili kuwasilisha mistari iliyooanishwa kwa Spotify, TIDAL, Instagram na Facebook! Ili kupata mistari iliyooanishwa, chagua Lyric Blaster leo kwa kuingia na kuwasilisha maneno ya mistari kwa ajili ya toleo lako.
Kumbuka: Inaweza kuchukua kuanzia wiki 1-2 kwa mistari yako kuonekana kwenye huduma.
Ucheleweshaji ni nadra, lakini wakati mwingine hutokea, na mara nyingi huwa nje ya uwezo wetu. Tunapendekeza kuangalia Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusiana na tarehe za kutolewa, hususani sehemu ya "Kumbuka".
-
Napataje mistari Iliyooanishwa kwa ajili ya nyimbo zangu?
Mistari iliyooanishwa kwa Apple Music na YouTube inapatikana kwa wasanii wote walio kwenye usajili wa Musician Plus na Ultimate!
Ikiwa unataka mistari iliyooanishwa kwa Spotify, Tidal, Instagram na Facebook, pia tunatoa huduma yetu ya Lyric Blaster , inayoendeshwa na Musixmatch.
Ni $14.99 kwa kila msanii, kwa mwaka kwa idadi ya nyimbo isiyo na kikomo.
Ili kupata mistari iliyooanishwa kwenye Spotify na Instagram, chagua kutumia Lyric Blaster leo kwa kuingia na kuwasilisha maneno ya mistari kwa ajili ya toleo lako.
Hatua ya kwanza ni kupakia maneno ya mistari. Kisha, unapowasilisha, chagua Lyric Blaster ili kujiunga kwa mistari iliyooanishwa. Baada ya maneno ya mistari yako kuidhinishwa, unaweza kuwasilisha mistari iliyooanishwa kutoka kwenye dashibodi ya mistari.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mahali ambapo mistari itawasilishwa, bofya hapa.
Vidokezo vichache:
- Mistari iliyooanishwa inaweza tu kuwasilishwa kwa nyimbo ambazo zina maneno ya nyimbo yaliyoidhinishwa. Kwa hivyo ikiwa umepakia maneno ya mistari kadhaa, subiri tu wakati tunakagua mistari yako. Inapaswa takribani siku moja kwa mistari kukaguliwa.
- Ikiwa unapata taabu kupiga wimbo wakati unajaribu kuoanisha mistari yako, unaweza kujaribu tena kutumia Google Chrome ikiwa bado hujafanya hivyo.
-
Je, kuna tofauti gani kati ya "Maneno ya Mistari" na "Mistari Iliyooanishwa"?
Maneno ya Mistari ni maandishi tu ya mistari yako. Maneno ya Mistari yanapatikana katika Apple, Google, na LyricFind.
Mistari iliyooanishwa ni mistari iliyoambatanishwa na muda kwenye muziki wako. Kwenye majukwaa ambayo yanawezesha mistari iliyooanishwa, kama vile Instagram na Spotify, mashabiki wako wataona mistari yako ikisogea sambamba na wimbo wako na hivyo kuwezesha kufuatisha uimbaji wa wimbo husika. Kwa usajili wa Musician Plus au Ultimate, tutatuma mistari iliyooanishwa kwa Apple Music na YouTube Music. Ili kupata mistari iliyooanishwa kwenye Instagram na Spotify, chagua kujiunga Lyric Blaster leo kwa kuingia na kuwasilisha maneno ya mistari kwa ajili ya toleo lako.
Kumbuka: mistari iliyooanishwa inapatikana kwa mipango ya Musician Plus na Ultimate! Lyric Blaster ni $14.99 kwa kila msanii, kwa mwaka na inajumuisha uwasilishaji mistari iliyooanishwa bila kikomo kwa Spotify, TIDAL, Instagram na Facebook kupitia Musixmatch.
-
Je, Nawasilisha Vipi Mistari Yangu kwa DistroKid?
DistroKid hurahisisha kufikisha mistari yako kwenye huduma za utiririshaji!
Ili kutembelea dashibodi ya mistari yako kwenye akaunti yako:
- Bofya kwenye Menyu ya Vipengele ya DistroKid upande wa juu kulia
- Chagua "Boresha muziki wako"
- Chagua "Mistari"
Hapa, utaweza kuwasilisha na kusimamia Maneno ya Mistari yako.
Tafadhali hakikisha mistari yako inafuata miongozo iliyo hapa chini
Mara tu unapowasilisha Maneno ya Mistari, inachukua takriban wiki 1-2 kwa mistari hiyo kwenda hewani katika huduma za utiririshaji kama vile:
- Apple Music
- LyricFind
- Google / matokeo ya kutafuta
- n.k.
- Jifunze zaidi kuhusu mistari yako inakosambazwa.
Kupata mistari iliyooanishwa kwenye Spotify, TIDAL, Instagram na Facebook, chagua kujiunga Lyric Blaster unapowasilisha maneno ya mistari yako! Gharama za Lyric Blaster ni $14.99 kwa kila msanii, kwa mwaka, na hukupa uwasilishaji usio na kikomo wa mistari iliyooanishwa kupitia Musixmatch.
Kumbuka: Mistari iliyooanishwa inaweza tu kuwasilishwa kwa nyimbo ambazo zina maneno ya mistari iliyoidhinishwa. Kwa hivyo ikiwa umepakia maneno ya mistari kadhaa, subiri tu wakati tunakagua mistari yako. Inapaswa takribani siku moja kwa mistari kukaguliwa.
Iwapo wewe unajifunza kwa kutazama zaidi, basi angalia video hii ya haraka ili kuona jinsi unavyoweza kuongeza Maneno ya Mistari kwa matoleo yako yote:
- Bofya kwenye Menyu ya Vipengele ya DistroKid upande wa juu kulia
Waliochangia See all 4 articles
-
Je, Naweza Kuongeza Mtayarishaji, Mtunzi wa Nyimbo, Waliochangia, Maelezo kwenye Jalada na Metadata kwenye Nyimbo Zangu?
Hakika unaweza!
- Ingia kwenye DistroKid
- Bofya Menyu ya Vipengele ya DistroKid iliyopo upande wa juu kulia
- Bofya "Boresha muziki wako"
- Bofya "Waliochangia"
Wachangiaji wako watawasilishwa kwa huduma zote za utiririshaji ambazo kwa sasa zinawakubali.
Ikiwa ni mara yako ya kwanza kuongeza waliochangia, mfumo utakutaka kwanza kuorodhesha mtunzi wa nyimbo. Kwa sababu watunzi wa nyimbo ni muhimu, na kila wimbo unapaswa kuwa na mtunzi.
*Tafadhali kumbuka kwamba si huduma zote zitaonyesha waliochangia tunaowaorodhesha kwenye ukurasa wa waliochangia. Iwapo unataka kuhakikisha wachangiaji wako wataonyeshwa, tunapendekeza kuwaorodhesha chini ya michango ya Mtunzi wa Nyimbo au Mtayarishaji. Tutaendelea kufuatilia uwezo wa washirika wetu katika kuonyesha waliochangia zaidi katika siku zijazo!
Kwa video ya haraka kuhusu jinsi ya kuongeza waliochangia na Maelezo ya Jalada, angalia jinsi-ya hapa chini:
-
Je, Naongezaje Mtayarishaji Kwenye Toleo Langu?
Unaweza kuongeza michango ya Mtayarishaji wa Muziki kwenye matoleo yako wakati wowote kwa kutembelea ukurasa wako wa Waliochangia, hata kama toleo lako tayari lipo hewani madukani!
Ili kufanya hivyo, nenda tu kwenye ukurasa wa albamu wa toleo ambalo ungependa kuhariri. Bofya "Waliochangia"
Kutoka kwenye ukurasa wa waliochangia, bofya menyu kunjuzi "Ongeza Mpya..." na chagu "Mtayarishaji."
Baada ya kuchagua aina ya mchango wa Mtayarishaji, unaweza kuchagua aina maalumu ya mtayarishaji katika menyu kunjuzi ifuatayo. Baada ya kuchagua vipengele hivi, unaweza kwenda mbele na kuingiza jina la Mtayarishaji wako. Aidha, una hiari ya kuongeza ama kutoongeza barua pepe zao (barua pepe za watayarishaji hazitaonyeshwa kwenye huduma za utiririshaji).
Go to article -
Kwa nini Wachangiaji Wangu Hawaonekani katika Huduma za Utiririshaji?
DistroKid ina uwezo wa kutuma kiasi kikubwa cha metadata za kina katika huduma za utiririshaji. Kitu ambacho ni kizuri!
Maelezo zaidi hapa.
Baadhi ya huduma zinaweza kuzishughulikia zote. Zingine zina uwezo wa kukubali kiasi kidogo tu kwa sasa—lakini kuna uwezekano zitakubali kiasi kikubwa zaidi katika siku zijazo.
Tutafuatilia kila mshirika wa huduma, na kuendelea kuwajulisha kuhusu kiwango cha juu cha metadata wanachoweza kushughulikia muda wowote. Wengi wanaanza na watunzi wa nyimbo na watayarishaji.
Tafadhali kumbuka kuwa wachangiaji wanaweza kuchukua wiki 1-2 ili kuonekana katika huduma zozote zinazowakubali.
-
Kwanini DistroKid Huuliza Majina Halisi ya Waandishi wa Nyimbo?
Habari njema! Majukwaa ya Kutiririsha Muziki yameanza kutambua mchango wa kila mmoja pale inapostahili. Hiyo maana yake ni kwamba, miongoni mwa mambo mengine, kuonyesha aliyeandika kila wimbo.
Kwa kawaida, watunzi wa nyimbo wanaorodheshwa kwa kutumia majina halisi--sio majina ya kisanii au majina ya marapa au majina ya bendi.
Ondoa hofu endapo unatumia jina la kisanii--jina lako halisi halitaonyeshwa kama jina la msanii au chochote, lakini litaonyeshwa wakati msikilizaji akitazama waliochangia au mistari ya wimbo.
Kwa mfano, tazama 2 Chainz wimbo "Bigger Than You (feat. Drake & Quavo)" kwenye Spotify (hapa). Kama ambavyo ungetarajia, majina ya wasanii yameorodheshwa kama:- 2 Chainz
- Drake
- Quavo
Hata hivyo, ukiangalia waliochangia kwa wimbo huo kwenye Spotify (hivi ndivyo), utagundua hayo majina halisi ya wasanii yameorodheshwa kama watunzi wa nyimbo. Majina yao halisi ni, kwa mtawalia:
- Tauheed Epps
- Aubrey Graham
- Quavious Marshall
Tazama picha ya skrini kutoka Spotify, hapa chini.
Go to article
Nyimbo za Kava See all 5 articles
-
Kwa nini Nahitajika Kununua Leseni ya Wimbo wa Kava Kupitia DistroKid?
Kila unapopakia wimbo DistroKid, utaona kisanduku cha kuteua ili kubainisha ikiwa uliandika wimbo huo ("wa asili"), au uliandikwa na mtu mwingine ("kava").
Kuna sheria nchini Marekani inayoelekeza jinsi ambavyo mapato kutoka kwenye nyimbo za kava yanavyohitaji kugawanywa na mtunzi asili. Ikiwa ungependa kujua maelezo kwa kina, bofya hapa.
Habari njema ni kwamba DistroKid hurahisisha upakiaji wa nyimbo za kava, ni rahisi sana kiasi kwamba huhitaji kufikiria kuhusu hilo. Bofya tu kisanduku kwenye fomu yetu ya kupakia ukibainisha kuwa ni wimbo wa kava, na kwa ada ndogo ($12 kwa kila wimbo wa kava, malipo yakijirudia kila mwaka) DistroKid itakata kiasi kinachohitajika kisheria kiotomatiki kutoka kwenye mapato yako (kwa kawaida senti 9.1 kwa kila mauzo nchini Marekani) na kukituma kwa mtunzi asili wa wimbo.
"Na kama tayari nina leseni ya kusambaza wimbo huo wa kava?"
Samahani, lakini bado unalazimika kupata leseni ya DistroKid. Sababu ni kwamba, hatuna namna ya kuthibitisha kuwa mtunzi asili analipwa sehemu yake inayohitajika kisheria isipokuwa kama ni sisi ndio tunaowalipa. Kutoziingiza kava katika mpango wa DistroiKid wa kutoa leseni za nyimbo za kava kunaweza kusababisha huduma za utiririshaji kuondoa maudhui yako--au kukienda vibaya sana--watunzi wa nyimbo kuchukua hatua za kisheria. Na hakuna mtu anataka hilo litokee.
-
Je, Nalazimika Kununua Leseni ya Kava Kupitia DistroKid Ikiwa Tayari Nina Leseni Kutoka Kwa Wakala Mwingine?
Ndiyo.Go to article
Sababu ni kwamba hatuna njia ya kuthibitisha kwamba mtunzi asili wa wimbo analipwa sehemu yake inayohitajika kisheria--isipokuwa kama sisi ndio tunaowalipa.
Kutochagua kava katika mpango wa DistroKid wa leseni za nyimbo za kava kunaweza kusababisha huduma za utiririshaji kuondoa maudhui yako--au kukienda vibaya sana--watunzi wa nyimbo kuchukua hatua za kisheria. Na hakuna mtu anataka hilo. -
Nikipakia Kava Kama Singo, Je, Naweza Pia Kuingiza Kava Hiyo Kwenye Albamu?
Ndiyo!
Hata hivyo, kumbuka, utahitaji kununua tena leseni ya kava kwa ajili ya kava iliyojumuishwa kwenye albamu.
Lazima ununue leseni ya kava ya DistroKid kila unapopakia wimbo wa kava kwenye DistroKid.
Endapo unapakia wimbo huo huo wa kava mara mbili, unahitaji kuchagua chaguo la "Wimbo wa Kava" kwa kila upakiaji, hivyo kununua leseni mbili. Hivyo ndivyo mfumo wetu unavyofahamu kukata sehemu ya mapato ya mtunzi wa wimbo kutoka kwenye mapato yako (kwa upakiaji wote wa wimbo huo, katika mfano huu). Zaidi ya hayo, leseni za DistroKid zinatumika tu kwa maudhui yanayosambazwa moja kwa moja na DistroKid, na hayawezi kutumika kwa madhumuni yoyote nje ya DistroKid.
Ni wajibu wako kuhakikisha kuwa wimbo wako utasimamiwa chini ya leseni ya kimekanika ya lazima.
Kwa maelezo zaidi kuhusu ununuzi wa leseni za kava kupitia DistroKid, tafadhali angalia makala hii. -
Muziki Wangu Una Sampuli Kutoka Nyimbo Zingine. Hiyo ni sawa?
DistroKid inaweza kusaidia kwenye kava. DistroKid haiwezi kusaidia kwenye sampuli.Go to article
Tofauti ni ipi?
Kusampuli
Kusampuli ni pale unapotumia rekodi halisi iliyoimbwa na msanii mwingine. Kwa mfano, endapo unaitumia rekodi ya 1971 ya Led Zeppelin inayoitwa "When The Levee Breaks" kama ngoma kwa wimbo wako. Kwa kawaida hiyo ni kinyume na sheria, labda kama umepata idhini kutoka kwa msanii asili au mwenye haki miliki.
Wimbo wa Kava
Wimbo wa kava ni wimbo ambao umeimba na kuurekodi wewe mwenyewe, lakini muziki uliandikwa na mtu mwingine. Kwa mfano, bendi yako ikipiga wimbo wa "Smooth Criminal" (ulioandikwa na Michael Jackson). Hii ni sawa kabisa—DistroKid hurahisisha na kuhalalisha uuzaji wa nyimbo za kava. Chagua tu "Mtu mwingine aliuandika" katika sehemu ya "Mtunzi wa nyimbo" kwenye fomu ya kupakia ya DistroKid. Utaona bei na maelezo zaidi, hapo. -
Je, Naweza Kupakua Leseni za Kava Zangu?
Ndiyo!
Ingia tu kwenye akaunti yako kisha bofya ikoni ya Wasifu wako kwenye sehemu ya juu kulia. Kutoka hapo, bofya "Leseni za nyimbo za Kava" ili kuona leseni zako zilizopo.
Go to article