Kila unapopakia wimbo DistroKid, utaona kisanduku cha kuteua ili kubainisha ikiwa uliandika wimbo huo ("wa asili"), au uliandikwa na mtu mwingine ("kava").
Kuna sheria nchini Marekani inayoelekeza jinsi ambavyo mapato kutoka kwenye nyimbo za kava yanavyohitaji kugawanywa na mtunzi asili. Ikiwa ungependa kujua maelezo kwa kina, bofya hapa.
Habari njema ni kwamba DistroKid hurahisisha upakiaji wa nyimbo za kava, ni rahisi sana kiasi kwamba huhitaji kufikiria kuhusu hilo. Bofya tu kisanduku kwenye fomu yetu ya kupakia ukibainisha kuwa ni wimbo wa kava, na kwa ada ndogo ($12 kwa kila wimbo wa kava, malipo yakijirudia kila mwaka) DistroKid itakata kiasi kinachohitajika kisheria kiotomatiki kutoka kwenye mapato yako (kwa kawaida senti 9.1 kwa kila mauzo nchini Marekani) na kukituma kwa mtunzi asili wa wimbo.
"Na kama tayari nina leseni ya kusambaza wimbo huo wa kava?"
Samahani, lakini bado unalazimika kupata leseni ya DistroKid. Sababu ni kwamba, hatuna namna ya kuthibitisha kuwa mtunzi asili analipwa sehemu yake inayohitajika kisheria isipokuwa kama ni sisi ndio tunaowalipa. Kutoziingiza kava katika mpango wa DistroiKid wa kutoa leseni za nyimbo za kava kunaweza kusababisha huduma za utiririshaji kuondoa maudhui yako--au kukienda vibaya sana--watunzi wa nyimbo kuchukua hatua za kisheria. Na hakuna mtu anataka hilo litokee.
Sign Up