Akaunti za Musician Plus na Ultimate kutoka DistroKid zinakupa ufikiaji wa Takwimu za Kila Siku Zilizokadiriwa kutoka Spotify, Apple Music, iTunes na Amazon.
Wakati mwingine, namba za Takwimu za Kila Siku kwa kiasi fulani hutofautiana na takwimu zilizoonyeshwa katika taarifa zako za mapato ya kila mwezi. Mara moja moja zinaweza kushuka hata hadi sifuri. Usiogope! Hiyo ni kawaida, na wala sio suala la kutia wasiswasi.
Kwa kawaida huwa ni suala la jinsi ambavyo huduma za utiririshaji zinavyoripoti kwa (API) ya DistroKid, na kwa kawaida, masuala ya aina hii hutatuliwa takribani ndani ya saa 24.
Aidha, ni muhimu kukumbuka kwamba takwimu zilizokadiriwa hutoka katika mfumo tofauti kabisa ikilinganishwa na ripoti za mapato, na utofauti wowote wa takwimu hautaleta athari yoyote kwenye mapato yako halisi yanayotokana na utiririshaji/mauzo.
Sign Up