DistroKid haichukui asilimia yoyote kwa kile ambacho maduka hututumia kama mapato yako. Maduka yanapotutumia ripoti za mapato, tunatuma 100% ya mapato unayotengewa moja kwa moja kwenye benki yako ya DistroKid. Tunahisi kuwa hupaswi kutoa asilimia ya mapato yako yatokanayo na mitiririko / mauzo kwa msambazaji wako. Ni wewe ndie uliyechuma hizo pesa na sio wao.
Wakati unapotoa pesa, unaweza kutozwa kodi na/au ada husika kutoka kwenye kichakata malipo chetu.*
Wakati PEKEE tunaochukua asilimia, ni endapo utachagua kujiunga na huduma yetu hiari "Social Media Pack". Hiyo ndio huduma ambayo hutuwezesha kupata video zinazotumia muziki wako kwenye YouTube na TikTok -- na kuwaambia YouTube na TikTok wawezeshe uchumaji wa mapato kwa vidoe hizo. Hapo tunachukua 20% ya mapato kutoka kwenye video za YouTube na TikTok tunazopata, na kisha tunakutumia kiasi kinachobaki (80%). Lakini bado unabaki na pesa unazoingiza kutoka kwenye huduma za utiririshaji na maduka ya muziki kama iTunes, Spotify n.k. Mara zote unabaki na 100% ya hayo, ukiondoa ada za benki/kodi zilizopo.
*Kumbuka: Kichakata malipo chetu, Tipalti, kinaweza kutoza ada kulingana na njia ya utoaji pesa. Unaweza kujua njia zipi zinazotoza ada kiasi gani kwa kuangalia makala hii: Je, Kuna Ada Wakati Ninapotoa Mapato Yangu?
Zaidi ya hayo, kutegemea na nchi unayoishi, unaweza kukabiliwa na viwango vya kodi ya zuio. Angalia makala hii kwenye Tipalti kwa maelezo zaidi: Viwango vya Kodi ya Zuio. DistroKid haiwezi kutoa maelezo yoyote kuhusu kodi, au chochote kinachohusiana na kodi, fomu za kodi, kodi ya zuio, n.k. Tunafahamu kwamba mambo haya yanaweza kuchanganya, na kwa hivyo ikiwa una maswali yoyote kuhusu jambo lolote linalohusiana na kodi, tafadhali wasiliana na mtaalamu wa masuala ya kodi ambaye ataweza kukupa ushauri na maelezo ili kukusaidia.
Sign Up