Ripoti za Mapato See all 14 articles

  • Je, Nitalipwa Lini na kwa Njia Gani?

    Ripoti za mapato na za kutoa mapato zinapatikana pindi DistroKid inapochakata mapato kutoka kwa huduma za utiririshaji na maduka. Huduma huripoti mapato yako kila baada ya miezi 1-2, ripoti hizo zikiwakilisha mitiririsho au mauzo ya miezi michache iliyopita. Kwa kawaida unaweza kutarajia kuona mapato kutoka kwa huduma nyingi takriban miezi 3 baada ya toleo lako kuenda hewani.

    Baadhi ya huduma zinaweza kuripoti mapato mara chache, kama vile mara moja au mbili kwa mwaka. Kumbuka kwamba huduma haziripoti mapato siku moja, na hazibainishi tarehe za kutoa malipo kwa upande wao.

    Zaidi, tafadhali kumbuka kuwa baadhi ya huduma huenda zikahitaji wimbo husika ufikie viwango fulani vya kutiririshwa ili ustahiki kupata mapato.
     

    Ratiba ya Malipo Kupokelewa na DistroKid

    Huduma za kutiririsha hutuma mapato kwa wasambazaji kwa nyakati tofauti. DistroKid inaweza kuwa wa kwanza kupokea mapato, lakini hili halina uhakika. Ikiwa unatumia msambazaji mwingine, wanaweza kupokea mapato kutoka kwa huduma kabla au baada ya DistroKid.

    Kumbuka kuwa huduma zinazoripoti mapato ya kila mwezi huenda zisifanye hivyo kwa siku ile ile kila mwezi, na hivyo kusababisha tofauti fulani wakati tunapozipokea.

    Tafadhali kumbuka kuwa baadhi ya huduma huenda zikahitaji wimbo kufikia viwango fulani vya kutiririshwa kabla ya kustahiki kupata mapato. Kwa mfano, unaweza kuangalia taarifa za kina kuhusu mahitaji ya kupata mapato kwa wimbo kwenye Spotify hapa: https://support.spotify.com/cd-sw/artists/article/track-monetization-eligibility/.

     

    Kutoa Mapato

    Ili kutoa mapato yako, unaweza kuingia kwenye akaunti yako ya DistroKid na kutembelea https://distrokid.com/bank.

    Kwa maelezo zaidi kuhusu kufuatilia pesa ulizotoa ukishaomba kutoa, tafadhali angalia makala haya: https://support.distrokid.com/hc/sw/articles/16501620089747.

    Go to article
  • Ni Kiasi Gani cha Mapato Yangu DistroKid Huchukua?
    Hakuna!

    DistroKid haichukui asilimia yoyote kwa kile ambacho maduka hututumia kama mapato yako. Maduka yanapotutumia ripoti za mapato, tunatuma 100% ya mapato unayotengewa moja kwa moja kwenye benki yako ya DistroKid. Tunahisi kuwa hupaswi kutoa asilimia ya mapato yako yatokanayo na mitiririko / mauzo kwa msambazaji wako. Ni wewe ndie uliyechuma hizo pesa na sio wao.

    Wakati unapotoa pesa, unaweza kutozwa kodi na/au ada husika kutoka kwenye kichakata malipo chetu.*

    Wakati PEKEE tunaochukua asilimia, ni endapo utachagua kujiunga na huduma yetu hiari "Social Media Pack". Hiyo ndio huduma ambayo hutuwezesha kupata video zinazotumia muziki wako kwenye YouTube na TikTok -- na kuwaambia YouTube na TikTok wawezeshe uchumaji wa mapato kwa vidoe hizo. Hapo tunachukua 20% ya mapato kutoka kwenye video za YouTube na TikTok tunazopata, na kisha tunakutumia kiasi kinachobaki (80%). Lakini bado unabaki na pesa unazoingiza kutoka kwenye huduma za utiririshaji na maduka ya muziki kama iTunes, Spotify n.k. Mara zote unabaki na 100% ya hayo, ukiondoa ada za benki/kodi zilizopo.

    *Kumbuka: Kichakata malipo chetu, Tipalti, kinaweza kutoza ada kulingana na njia ya utoaji pesa. Unaweza kujua njia zipi zinazotoza ada kiasi gani kwa kuangalia makala hii: Je, Kuna Ada Wakati Ninapotoa Mapato Yangu?

    Zaidi ya hayo, kutegemea na nchi unayoishi, unaweza kukabiliwa na viwango vya kodi ya zuio. Angalia makala hii kwenye Tipalti kwa maelezo zaidi: Viwango vya Kodi ya Zuio. DistroKid haiwezi kutoa maelezo yoyote kuhusu kodi, au chochote kinachohusiana na kodi, fomu za kodi, kodi ya zuio, n.k. Tunafahamu kwamba mambo haya yanaweza kuchanganya, na kwa hivyo ikiwa una maswali yoyote kuhusu jambo lolote linalohusiana na kodi, tafadhali wasiliana na mtaalamu wa masuala ya kodi ambaye ataweza kukupa ushauri na maelezo ili kukusaidia.

    Go to article
  • Je, Huduma za Utiririshaji Hulipa Kiasi Gani kwa Kila Mtiririko?
    Viwango vya malipo ambavyo huduma za kutiririsha hulipa havipangwi na DistroKid, na hatuna uwezo wa kuvibadilisha. Tunapitisha tu kiasi halisi ambacho huduma hututumia. DistroKid imekuwa ikipitisha na daima itaendelea kupitisha 100% ya mapato ambayo huduma hututumia kwa mitiririsho/mauzo yako, ukitoa ada za benki/kodi zinazotumika.

     

    Kwa nini viwango vya malipo ya utiririshaji hutofautiana?

    Viwango vya kutiririsha vinatofautiana kwa sababu kuna mambo mengi ambayo huduma hutumia kukokotoa unachostahili kulipwa, na viwango vya kukokotoa vinatofautiana kutoka huduma hadi nyingine. Baadhi ya vitu ambavyo huduma hutumia kukokotoa viwango ni pamoja na (lakini sio hivi tu):

    • Wingi wa mitiririsho/kupakuliwa

    • Maeneo

    • Aina ya usajili (usajili wa bila malipo ikilinganishwa na usajili wa malipo)

    • Mapato ya matangazo/usajili

    Mbinu ya Malipo Kwa Uwiano

    Huduma nyingi zinasambaza mapato kwa kutumia mbinu ya malipo kwa uwiano. Katika mtindo huu, mapato yote ya kiwango cha bidhaa yanasanywa pamoja, na asilimia ya mapato hayo kutengwa kwa ajili ya wasanii. Mapato yaliyosalia kisha yanagawanywa kwa nyimbo kulingana na kiwango chao cha jumla ya mitiririsho iliyofanyika kwenye kiwango hicho cha bidhaa.

    Mfano:

    Huduma ina $1,000 za kusambaza kwa safu yao ya usajili unaolipiwa ambao umekusanya jumla ya mitiririsho milioni 10 kwa mwezi. Kati ya jumla ya mitiririsho milioni 10, wimbo wako ulitiririshwa mara 1,500.

    • 1,500/10,000,000*$1,000= $0.15 inadaiwa

    Tafadhali kumbuka kuwa mfano huo hapo juu haukutoka kwa huduma yoyote halisi, na kila huduma ina njia yake ya kutumia mbinu ya malipo kwa uwiano. Kwa mfano, Spotify ina video nzuri inayoelezea jinsi ambavyo mapato yanakokotolewa kwa upande wao: Jinsi Spotify Inavyokulipa

    Mauzo vs Mitiririsho

    Kwa huduma ambazo huuza vipakuliwa vya kidijitali badala ya kutiririsha, ni kawaida kwa huduma kuchukua asilimia ya mauzo, mara nyingi hadi 30%, huku msanii akipokea 70% inayosalia. Hata hivyo, asilimia hii inaweza kutofautiana kulingana na huduma.

    Go to article
  • Nikifuta Toleo, Je, Bado Ninapokea Mapato Yangu?

    Ndiyo. Tuseme unaamua kufuta toleo ili lisipatikane kwa sababu yoyote ile. Bado utapokea mapato yoyote ambayo itakuwa umepata wakati muziki wako ulipokuwa hewani kwenye huduma za utiririshaji, hadi pale ulipotoweka. Mapato yataingia kwenye akaunti yako, kutegemeana na ratiba ifuatayo ya kutoa ripoti.

    Tarajia kusubiri kuanzia wiki 1-2 kwa muziki wako uliofutwa uweze kutoweka kwenye huduma zote za utiririshaji, wakati mwingine hutokea mapema zaidi.

    Go to article
  • Kutumia Benki ya DistroKid ili Kuona Mapato Yako

    Ili kufikia Benki yako ya DistroKid, ingia kwenye DistroKid na ubonyeze "Benki" kwenye bango la juu, au nenda moja kwa moja pale https://distrokid.com/bank.

    Benki yako ya DistroKid inapatikana ili kukuonyesha jumla ya mapato yako, pesa ulizotoa na jumla ya mapato ambayo umetoa, na ni kiasi gani cha pesa unazodai DistroKid kinaweza kutolewa.

    Ikiwa ungependa kuona maelezo zaidi kuhusu mapato yako, bofya "Tazama Taarifa Kwa Kina" kwenye ukurasa wako wa Benki ya DistroKid.

     

    Sehemu ya Mapato Yako Yote

    Sehemu ya kwanza ya Benki yako ya DistroKid ni sehemu ya "Mapato Yote". Sehemu hii itaonyesha historia yote ya jumla ya mapato kwa wasanii wote kwenye akaunti yako. Zaidi, unaweza kufikia uchanganuzi wa mapato kwa msanii, wimbo au huduma.

     

    Sehemu yako ya Utoaji Wote

    Sehemu ya pili ya Benki yako ya DistroKid ni sehemu ya "Utoaji". Katika sehemu hii, utaona jumla ya kiasi cha pesa zote zilizotolewa kwenye akaunti yako. Unaweza pia kubofya "Tazama utoaji wote" ili kuona historia ya utoaji kwa akaunti yako, pamoja na kiasi cha kila utoaji (ukiondoa ada za benki na kodi inayotumika).

     

    Sehemu ya "Tuna Deni Lako"

    Sehemu ya tatu ya Benki yako ya DistroKid ni sehemu ya "Tuna Deni Lako...", inayoonyesha kiasi cha mapato ambacho kiko tayari kuondolewa kwenye akaunti yako. Kwa maelezo zaidi kuhusu kuondoa mapato yako, angalia makala haya: https://support.distrokid.com/hc/sw/articles/39076091905555.

    Go to article
  • Kuangalia Ni Mara Ngapi Wimbo Wako Umetiririshwa na Kupakuliwa

    Ili kuona jumla ya kutiririshwa na kupakuliwa kwa matoleo yako, ingia kwenye DistroKid na utembelee Benki yako ya DistroKid pale https://distrokid.com/bank kwa kubofya "Benki" kwenye upau wa kuvinjari wa juu. Kisha, bofya kitufe cha samawati kinachosema "TAZAMA MAELEZO KWA KINA".

    Hii itakuleta kwenye ukurasa wa maelezo ya Benki ambapo unaweza kuona jedwali kadhaa, lakini ile inayoonyesha ni mara ngapi toleo lako limetiririshwa au kupakuliwa ni lile la "KIASI".

    Kulingana na huduma, jedwali hili la idadi litaonyesha mitiririsho au kupakuliwa/mauzo. Hizi ndizo huduma zinazoripoti kupakuliwa (nyingine zote ni kutiririsha):

    • iTunes

    • Beatport

    • Amazon (ununuzi kwenye Amazon Webstore)

    • MediaNet

    • Upakuaji wa TIDAL

     

    Kupakua Lahajedwali la Data za Kutiririshwa/Mauzo

    Unaweza kuomba faili ya .tsv yenye maelezo yote kwa kina wakati wowote kwa kubofya kitufe cha kupakua kilicho upande wa juu kulia kwenye ukurasa wa maelezo ya kina. Hii itakuletea ukurasa wa kupakua faili hiyo.

    Ikiwa kuna rekodi chini ya 50,000 za kujumuisha kwenye lahajedwali, faili itachakatwa na kupakuliwa moja kwa moja kutoka kwenye ukurasa.

    Ikiwa kuna zaidi ya rekodi 50,000 za kujumuisha kwenye lahajedwali, ukurasa utakuruhusu kuweka vichujio vya ripoti yako kabla ya haijatengenezwa. Vichujio hivyo vinajumulisha tarehe, maduka, wasanii, matoleo na utoaji (pesa). Mara tu unapochagua vichujio unavyotaka, unaweza kubofya "Twende kazi" ili kuomba ripoti iliyotolewa.

    Ukishaomba ripoti, kuchakata kutaanza kutengeneza ripoti. Mchakato ukishakamilika na faili kuwa tayari kupakuliwa, barua pepe itatumwa kwako ili kukuarifu. Barua pepe itajumuisha kiungo cha ukurasa wako wa ripoti, ambao faili litakuwa tayari kwa kupakuliwa. Unaweza pia kuelekea moja kwa moja hadi https://distrokid.com/bank/priority ili kutazama ripoti zinazopatikana za kupakuliwa.

    Tafadhali kumbuka kuwa ripoti zinazotengenezwa zitakuwa zinapatikana kwa siku 7 pekee. Ikiwa siku 7 zimepita na ripoti haipatikani tena, utahitaji kuomba ripoti mpya itolewe.

    Go to article
See all 14 articles

Kutoa Mapato Yako See all 8 articles

  • Kuweka Mapendeleo ya Njia ya Kulipwa katika Tipalti

    Unapodaiwa mapato, DistroKid itakuuliza kuhusu mapendeleo ya njia ya kulipwa katika kichupo cha Benki cha akaunti yako ya DistroKid. Hutaulizwa mapendeleo haya hadi wakati huo.

    Ifikapo wakati wa kuweka au kubadilisha mapendeleo haya, bofya kwenye ikoni ya wasifu wako upande wa juu kulia, kisha chagua "Njia ya Malipo", au nenda moja kwa moja kwenye https://distrokid.com/payouts/.

    Baada ya hapo, utahitaji:

    1. Kujaza taaraifa zote zinazohitajika za mawasiliano.
    2. Chagua njia yako ya malipo unayopendelea.
    3. Chagua na ujaze Fomu za Kodi zinazohitajika. Ukiwa na maswali, bofya "Need Help? Start the tax form questionnaire".

    Kumbuka: Hatuwezi kukusaidia kwa maswali/masuala yoyote ya kodi. Tafadhali wasiliana na mtaalamu wa kodi ikiwa unahitaji mwongozo au usaidizi kuhusu masuala ya kodi.

    Go to article
  • Kutoa Mapato Yako

    Unaweza kutoa mapato yako wakati wowote kwa kutembelea https://distrokid.com/bank na kubofya kitufe cha "Toa Mapato".

    Ikiwa kitufe hiki hakipatikani, huenda ukahitaji kutembelea https://distrokid.com/payouts/ ili kufanya marekebisho ya njia yako ya malipo. Kitufe hicho hakitaonekana pia ikiwa huna mapato ya kutosha kukidhi kiwango cha chini cha kutoa ($6 USD) na/au ada yoyote ya kutoa inayohusiana na aina ya malipo uliyochagua.

     

    Kuchagua Njia Yako ya Malipo

    Ili kuweka mbinu yako ya malipo, unaweza kufungua menyu ya akaunti yako kwa kubofya ikoni iliyo juu kulia, kisha bofya "Njia ya Malipo." Unaweza pia kwenda moja kwa moja hadi https://distrokid.com/payouts/.

    Kisha, unaweza kubofya "Sasisha mipangilio yako ya Tipalti" ili kufikia lango la kichakataji chetu cha malipo. Utahitaji kuingiza nenosiri lako la DistroKid ili kufikia lango hili. Mara tu unapoingiza nenosiri lako na kuingia kwenye lango, unaweza kuweka maelezo yako na kuchagua njia yako ya malipo unayopendelea.

    Kwa mwongozo maalum kuhusu kujaza taarifa zako pale https://distrokid.com/payouts/, tafadhali tazama makala haya: https://support.distrokid.com/hc/sw/articles/360013649013.

     

    Kuomba kutoa hela

    Ili kuomba kutoa hela, unaweza kutembelea benki yako ya DistroKid pale https://distrokid.com/bank na kubofya kitufe cha "Toa Mapato".

    Jumla inayoonyeshwa chini ya sehemu ya "Tuna Deni Lako" ya ukurasa wako wa Benki ya DistroKid itatumwa utakapotuma ombi.

    Ombi likishawasilishwa, malipo yatachakatwa kupitia njia ya malipo uliyoweka pale https://distrokid.com/payouts, na kwa kawaida utayapokea ndani ya siku 14.

    Go to article
  • Je, DistroKid Inatoa Njia Zipi za Kutoa Pesa?

    DistroKid wanakubali idadi kubwa ya machaguo ya kufanya malipo kupitia Tipalti, mtoa huduma wetu wa malipo. Machaguo haya ni pamoja na PayPal, ACH, uhamisho wa kielektroniki, eCheck, au hundi za karatasi. Tafadhali kumbuka kwamba DistroKid hawana ushirikiano wa kutoa fedha kutumia watoa huduma za malipo wa kati kama CashApp, Venmo, na Payoneer.

    Ili kubadilisha njia yako ya malipo, bofya kwenye ikoni ya wasifu wako iliyo upande wa juu kulia kisha uchague "Njia ya Malipo", au nenda moja kwa moja pale https://distrokid.com/payouts. Unaweza kubainisha jinsi ungependa kupokea mapato yako huko.

    Hutahitaji kuweka maelezo yoyote ya malipo hadi utakapokuwa na mapato ya kutoa kutoka kwenye ukurasa wako wa Benki ya DistroKid .

    Tafadhali kumbuka kuwa mifumo ya malipo inayopatikana kwako inategemea eneo lako, na sio mifumo yote ya malipo inapatikana katika eneo lako.

    Go to article
  • Kusasisha Taarifa Zako za Kodi kwa ajili ya Kutoa Fedha

    Ikiwa unahitaji kuweka taarifa au nyaraka za kodi zinazohitajika kwa ajili ya kutoa fedha kupitia Benki yako ya DistroKid, unaweza kuingia kwenye akaunti yako ya DistroKid na kutembelea https://distrokid.com/payouts. Kutoka hapo, ingiza nenosiri lako la DistroKid ili kufikia tovuti ya Tipalti kwa akaunti yako.

    Mara tu unapoingia kwenye tovuti ya Tipalti, unaweza kuongeza au kusasaisha taarifa na nyaraka za ushuru zinazohitajika, na pia kusasaisha njia yako ya malipo unayopendelea.

    Go to article
  • Hela Nilizotoa Ziko Wapi?

    DistroKid huchakata maombi ya malipo mara mbili kwa wiki. Kuanzia mwanzo hadi mwisho, inaweza kuchukua hadi siku 14 kwa ombi la kutoa hela lililowasilishwa kuonekana kwenye akaunti unayochagua pale https://distrokid.com/payouts.

    Ili kuangalia hali ya utoaji wako wa hela, unaweza kuingia katika akaunti yako ya DistroKid na kuelekea https://distrokid.com/bank. Ukurasa wako wa Benki utakujulisha ikiwa utoaji wako bado unasubiri au umekamilika. Ikiwa utoaji wako umekamilika na hujapokea hela, kuna uwezekano malipo yako yalikataliwa na kurejeshwa na benki yako.

     

    Kuangalia Hali ya Utoaji Wako wa Pesa

    Ili kuangalia kama utoaji wako bado unasubiri, unaweza kwanza kuelekea kwenye ukurasa wako wa Benki ya DistroKid pale https://distrokid.com/bank. Utoaji wa pesa unaosubiri huonyesha kisanduku cha kijivu ambacho kinajumuisha muda uliopita tangu ombi liwasilishwe. Kisanduku hiki cha kijivu kinatoa kiungo cha kuwasiliana na usaidizi wa DistroKid ikiwa tunahisi kuwa muda mrefu umepita tangu ombi la kutoa kuwasilishwa.

    Ikiwa utoaji wako umekamilika, utauona umeorodheshwa chini ya "Tazama Utoaji Wote" kwenye ukurasa wako wa Benki ya DistroKid.

    Kichakataji chetu cha malipo, Tipalti, pia hutuma arifa ya barua pepe kuhusu utoaji wako wa pesa kwa barua pepe ya mawasiliano uliyoweka pale https://distrokid.com/payouts.

    Baada ya utoaji wa pesa kukamilika, unaweza kufuatilia benki yako kuthibitisha kuwa wamepokea mapato hayo.

     

    Utoaji Ulikataliwa na Benki Yako

    Ikiwa utoaji wako wa pesa unaonekana chini ya sehemu ya "Tazama Utoaji Wote" pale https://distrokid.com/bank lakini bado hujapokea hela baada ya siku 14, huenda malipo yalikataliwa na kurudishwa na benki yako. Katika hali hii, utapokea barua pepe ya kukujulisha kuhusu kukataliwa. Kisha malipo hayo yatarejeshwa kwa benki yako ya DistroKid (ukiondoa ada) baada ya wiki chache. Malipo yakisharudishwa, unaweza kusasisha njia yako ya kulipa pale https://distrokid.com/payouts na kuomba kutoa tena.

    Go to article
  • Je, Kuna Ada Wakati Ninapotoa Mapato Yangu?

    Ndiyo, kuna ada unapoondoa mapato kutoka kwa Benki yako ya DistroKid. Kichakata chetu cha malipo, Tipalti, hutoza DistroKid ada ndogo ya kutuma pesa, ambayo hukatwa kiotomatiki kwenye mapato yako unapotoa.

    Kiasi cha Ada za Kutoa kwa Njia ya Malipo

    • ACH (Marekani pekee) —  $1.07 kwa kila malipo
    • Hundi ya Kieletroniki (Marekani) —  $1.61 kwa kila malipo
    • eCheck/Uhamishaji Kupitia Benki/SEPA (Wasio Marekani) —  $5.35 kwa kila malipo
    • Hundi ya Karatasi — $3.21 kwa cheki
    • Uhamisho kwa njia ya Benki (Marekani) — $16.05 kwa kila malipo
    • Uhamisho kwa Njia ya Benki (Kimataifa kwa sarafu za nyumbani) — $21.40 kwa kila malipo
    • Uhamisho kwa Njia ya Benki (Kimataifa kwa USD) — $27.82 kwa kila malipo
    • PayPal (Mkazi asiyeishi Marekani): USD 1.07 + 2% Hadi USD 22.47
    • PayPal (Mkazi wa Marekani): USD 1.07 + 2% Hadi USD 2.14

    Kiasi cha Chini cha Kutoa

    Kiasi cha chini unachohitaji ili kutoa ni $6 USD. Kwenye ukurasa wa benki yako, ikiwa jumla yako chini ya "Unachotudai" inaonyesha chini ya $6 au ikiwa ada za kutoa muamala za njia uliyochagua ya malipo hazijatimizwa, ombi lako la kutoa fedha halitashughulikiwa.

     

    Muhimu: Tafadhali hakikisha kuwa umechagua njia unayopendelea ya kutoa pesa, na unazingatia ada zinazohusiana na njia unayopendelea. Ombi la kutoa likikataliwa linaweza kulimbikiza ada ya kukataliwa kutoka kwa kichakata chetu cha malipo.

     

    Ada za Kubadilisha Fedha za Kigeni

    Kando na ada ya kutoa pesa, unaweza kutozwa ada ya kubadilisha fedha za kigeni ya hadi 3% iwapo sarafu ya malipo ni tofauti na ya nchi unayochagua. Maelezo zaidi kuhusu ada ya kubadilisha Fedha za Kigeni yanapatikana unapochagua njia ya kulipwa pale https://distrokid.com/payouts.

    Go to article
See all 8 articles

Kodi See all 6 articles

  • Je, DistroKid Inaweza Kunisaidia Kwa Masuala Yangu ya Kodi?

    DistroKid haiwezi kukusaidia katika masuala yoyote yanayohusu kodi, kwa kuwa sisi si wataalamu wa kodi.

    Unahitaji kushauriana na mtaalamu wa kodi kwa usaidizi wa jambo lolote linalohusiana na kodi.

    Go to article
  • Kwanini DistroKid Hukusanya Taarifa za Kodi?

    Wasanii wanaoishi Marekani wanaombwa kujaza Fomu ya W-9, na wasanii walio nje ya Marekani wanaombwa kujaza Fomu ya W-8BEN. Tunatakiwa kukusanya taarifa hizi mara moja kwa mwaka, na watumiaji wote wa DistroKid wanatakiwa kukamilisha nyaraka zinazohitajika za kodi ili kupokea mapato kutoka kwa DistroKid.

    Kwa usaidizi wowote kuhusu kujaza fomu, tafadhali wasiliana na mtaalamu wa kodi.

     

    TIN/EIN kwa Fomu ya W-9

    Wasanii wanaoishi Marekani wanaombwa kujaza Fomu ya W-9, ambayo inakuuliza TIN/EIN yako. Kama mtu binafsi, TIN yako ni nambari yako ya social security (SSN) au Nambari ya Utambulisho ya Mlipakodi Binafsi (ITIN) ikiwa umekabidhiwa moja na IRS kwa madhumuni ya kodi ya nchi. Ikiwa umejiandikisha kama biashara, TIN yako ni EIN yako.

    Kwa usaidizi kuhusu maswali ya zaizi yanayohusiana na fomu za kodi, tafadhali wasiliana na mtaalamu wa kodi.

    Go to article
  • Zenwork Tax1099, Idhini ya Kielektroniki, na Kuwasilisha Fomu ya Kodi

    DistroKid inafanya kazi na Zenwork Tax1099 kuwasilisha nyaraka zote za kodi. Tax1099 hivi sasa inahitaji idhini ya mtu binafsi ili kuwasilisha fomu hizo za kodi kupitia uwasilishaji wa kielektroniki (eDelivery).

    Huenda ukapokea barua pepe kutoka statements@tax1099.com kabla ya kupokea fomu zako za kodi, kuhusu kutoa idhini kwa Zenwork ya kuwasilisha fomu zako za 1099 au 1042 kwa njia ya kielektroniki kupitia xForce, jukwaa lao la kujihudumia.

    Tafadhali rejelea huu muhtasari uliotolewa na Zenwork Tax1099 kuhusu kutoa idhini ya kuwasilisha nyaraka zako za kodi kwa njia ya kielektroniki.

    Wakati fomu yako ya ushuru itakuwa tayari, utapokea barua pepe kutoka statements@tax1099.com. Kutoka hapo unaweza kubofya "Consent Now" ili kupokea nenosiri la muda.

    DistroKid haiwezi kutoa taarifa zozote kuhusu kodi, au kitu chochote kinachohusiana na kodi, fomu za kodi, zuio la kodi, n.k. Tunaelewa kwamba michakato ya kodi inaweza kutatanisha, kwa hivyo ikiwa una maswali yoyote kuhusu jambo lolote linalohusiana na kodi, tafadhali wasiliana na mtaalamu wa kodi kwa mwongozo na usaidizi.

    Go to article
  • Kupokea 1099 au 1042 kwa ajili ya Mapato Yako

    Ikiwa ulitoa pesa katika mwaka wa fedha uliopita, utapokea 1099 au 1042 kupitia barua pepe kutoka statements@tax1099.com. DistroKid haitoi fomu za W-2 kwa wakati huu.

    Ikiwa ulisasisha taarifa zako za kodi mara kadhaa kwa mwaka mmoja wa fedha, kila mlipwaji mahususi atapokea fomu tofauti kwa ajili ya kutoa zilizochukuliwa chini ya utambulisho wake wa kodi ulioidhinishwa.

    Kwa maelezo zaidi juu ya jinsi ya kufikia fomu zako za 1099 au 1042, ikiwa ni pamoja na nenosiri lililotengenezwa kwa ajili yako, tafadhali soma Makala hii.

    Kumbuka: Hatuwezi kukusaidia kwa maswali/masuala yoyote ya kodi. Tafadhali wasiliana na mtaalamu wa kodi ikiwa unahitaji mwongozo au usaidizi kuhusu masuala ya kodi.

    Go to article
  • Nenosiri la Fomu yangu ya 1099 au 1042 ni lipi?

    Wakati fomu yako ya ushuru itakuwa tayari, utapokea barua pepe kutoka statements@tax1099.com. Barua pepe hiyo itaomba idhini yako ya kuwasilishwa kieletrokini kwa 1099 au 1042 yako, na itajumuisha hatua zinazohitajika kutoa idhini yako kwa kuwasilisha kielektroniki.

    Unaweza kubofya “Idhinisha Sasa” katika barua pepe ili kupokea nenosiri la muda ili kuanza mchakato wa kuunda akaunti ya Zenwork xForce inayohitajika ili kukamilisha mchakato wa kutoa idhini. Nenosiri la muda litatumwa kwako, na unaweza kulitumia kuingia na kuunda nenosiri la kudumu.

     

    Hatua za Kutoa Idhini ya Kuwasilisha Kielektroniki:

    Kwenye barua pepe, utapata hatua hizi ili kutoa idhini ya kuwasilisha kielektroniki (eDelivery):

    1. Jisajili kwa Zenwork xForce.
    2. Kwenye Dashibodi, bofya kitufe cha "eDelivery Requests".
    3. Kwenye ukurasa wa Wanaolipa, bofya kitufe cha "Consent Now" kinachohusishwa na mlipaji ambaye ameomba idhini yako.
    Go to article
  • Zuio la Kodi kwa Wakaazi Wasio wa Marekani

    Iwapo nchi yako unakolipa kodi sio Marekani, hadi 30% ya mapato yako yanaweza kukabiliwa na zuio la kodi. Iwapo kuna mkataba wa kodi kati ya nchi yako na Marekani, na ikiwa unakidhi masharti ya kunufaika na mkataba huo, kiwango cha zuio kinaweza kupunguzwa au kuondolewa.

    Kutegemea na sheria na kanuni katika nchi unakostahiki kulipa kodi, unaweza kuweka baadhi ya au kodi yote iliyozuiwa na Marekani (kama ipo) dhidi yakodi yako.

    Orodha ya kina ya viwango vya zuio la kodi kwa kila nchi inaweza kupatikana katika safu wima iliyoandikwa "Copyrights" hapa:
    https://support.tipalti.com/Content/Topics/UserGuide/Taxation/TaxWithholding/WithholdingRates.htm

    Taarifa za mikataba ya kodi zinaweza kuingizwa pale www.distrokid.com/payouts, katika Sehemu ya 3 (Tax Forms), Sehemu ya II (Claim of Treaty Benefits).

    DistroKid haiwezi kutoa ushauri wa kodi, kwa hivyo tunalazimika kusema kwamba huu sio ushauri kuhusu masuala ya kodi. Tafadhali wasiliana na mtaalamu wa kodi ikiwa una maswali yoyote kuhusu maelezo hapa.

    Go to article

Mgawanyo See all 6 articles

  • Kutumia Mgawanyo Kulipa Washirika Wako Kiotomatiki

    Ukiwa na kipengele cha Mgawanyo, DistroKid inaweza kugawanya mapato kutoka kwa wimbo au albamu yoyote na kutuma mapato hayo kwa watumiaji wengine wa DistroKid kiotomatiki. Unaweza kuongeza washirika wako, watayarishaji, wanabendi, mameneja na zaidi, na tutawatumia mapato moja kwa moja.

    Kwa ajili ya faragha, washirika wanaweza tu kuona ni asilimia ngapi wanapata. Hawawezi kuona washirika wako wengine, au asilimia ambayo watu wengine wanapata.

    Ili kuanza, ingia kwenye DistroKid kisha bofya "Mgawanyo," au nenda kwenye ukurasa wa albamu unaotaka kusanidi mgawanyo kwake kisha bofya "Hariri Mgawanyo" chini ya sehemu ya "Mgawanyo".

    Unapomwalika mtu kwenye Mgawanyo na bado hana akaunti ya DistroKid, unaweza kuchagua kulipa $10 kwa mwaka ili kumruhusu kukusanya na kutoa mapato yoyote kutoka kwa Mgawanyo bila kuhitaji usajili kamili wa DistroKid. Vinginevyo, usajili wa DistroKid unahitajika ili kukubali na kutoa mapato kutoka kwa Mgawanyo - ukimwalika mtu kwenye Mgawanyo na hana usajili, atapata punguzo la 50% ili ajisajili kwenye DistroKid upande wake!

     

    Kuweka Mgawanyo

    Ili kuweka Mgawanyo kwa wimbo au albamu, bofya "Mgawanyo" kwenye sehemu ya juu baada ya kuingia kwenye DistroKid au nenda kwa https://distrokid.com/teams. Kwenye ukurasa huu, unaweza kuchagua toleo kutoka kwa menyu kunjuzi kisha kubofya "Kinachofuata." Halikadhalika, Unaweza pia kutembelea ukurasa wa albamu na kuchagua "Hariri Migawanyo" katika sehemu ya "Mgawanyo".

    Kwenye ukurasa unaofuata, utaona kikundi cha sasa cha Mgawanyo kwa singo/albamu. Ikiwa hakuna Mgawanyo uliowekwa hapo awali, utaona 100% ya mapato yamewekwa kwako, mmiliki wa akaunti. Ili kuongeza mshirika, bofya "+ Ongeza mshirika" chini ya wimbo. Hii itaunda nafasi mpya ya mshirika, na kukuruhusu kuweka asilimia ya Mgawanyo kwake pamoja na barua pepe yake. Kurekebisha asilimia hii kutapunguza asilimia kiotomatiki kwa washirika wengine wote ili jumla kamwe iwe 100%.

    Ukishaongeza washirika wote na kuweka asilimia zao, bofya "Kagua Mabadiliko." Hii itakuleta kwenye ukurasa wa kukagua mabadiliko yote ya Mgawanyo wako. Iwapo washiriki wowote walioongezwa bado hawana akaunti ya DistroKid, ukurasa huu utakuruhusu kuchagua kulipa $10 kwa mwaka ili kuwaruhusu kupokea na kuondoa mapato bila kujisajili kwa DistroKid, au kuwaruhusu washirika wako kulipia usajili wao wenyewe kwa punguzo la 50% kwa mwaka wa kwanza. Ukishakagua maelezo, bofya "Hifadhi Mabadiliko" ili kuwasilisha Mgawanyo mpya.

    Unaweza kubadilisha Migawanyo kwa njia hii wakati wowote - kumbuka tu kwamba mabadiliko yoyote kwenye Migawanyo iliyopo yatahitaji washiriki kukubali mwaliko wao kwa mara nyingine tena.

    Kwa maelezo ya haraka kuhusu jinsi ya kugawanya mapato, tazama video hii:

    Kutazama Historia ya Migawanyo kwenye Toleo

    Ili kutazama historia ya Mgawanyo ya toleo, unaweza kuelekea kwenye ukurasa wa albamu yake kupitia dashibodi yako ya DistroKid, na kisha bofya kwenye "Tazama Historia ya Mgawanyo" chini ya sehemu ya Mgawanyo.

    Kwenye ukurasa huu, unaweza kuona historia ya mabadiliko yote ya Mgawanyo kwa kila wimbo katika toleo. Zaidi, unaweza kutuma mialiko tena au kuwaondoa washirika ambao bado hawajakubali mwaliko wao.

    Ikiwa mshirika bado hajakubali mwaliko, unaweza kutuma mwaliko tena au kumuondoa kwenye Mgawanyo kwa kubofya "Chaguo..." chini ya safu ya "Umekubaliwa" kwa mshirika husika. Kutoka hapo, bofya "Tuma tena" au "Ondoa."

    Kumwondoa mshirika ambaye bado hajakubali mwaliko wake kutarejesha mapato yote aliyotengewa kwako.

    Je, Ni Nini Kinatokea Ikiwa Mshirika Hatakubali Mgawanyo Papo Hapo?

    Matoleo yako hayatacheleweshwa endapo mshirika wako anachelewa kujisajili. Badala yake, tutahifadhi mapato hayo hadi watakapojiunga.

    Mgawo wa mapato aliyotengewa mshirika wako utahifadhiwa kwa ajili yake hadi atakapokubali mwaliko wako. Anapokubali na kufungua akaunti, mapato yaliyoshikiliwa yatawekwa katika Benki yake ndani ya saa 24.

    Ikiwa mshirika wako hatajiunga kamwe, unaweza kughairi mwaliko wao kwa urahisi na mapato aliyokuwa ametengewa yatarudi kwako. Kumwondoa mshirika ambaye hajakubali kutoka kwa Mgawanyo, unaweza kuelekea kwenye ukurasa wa kuhariri Migawanyo, kubofya kitufe cha kutoa (-) karibu na jina lao kwa nyimbo zozote ambazo ni mwanachama wa Migawanyo, kisha kubofya "Pitia Mabadiliko".

    Go to article
  • Kuweka Marejesho katika Mgawanyo

    Marejesho katika kipengele cha DistroKid cha Mgawanyo kinakuruhusu kuweka washiriki mmoja mmoja kupokea mapato yote ya toleo hadi kiasi mahususi cha marejesho kinapofikiwa. Mara tu fedha za awali zinapokuwa zimerejeshwa, asilimia za Mgawanyo zitaenda moja kwa moja kwa washirika wengine wote kwenye Mgawanyo.

    Jinsi ya Kuweka Marejesho kwenye Toleo Lako

    Ili kuweka Marejesho kwenye toleo lako, kwanza nenda kwenye ukurasa wa toleo katika DistroKid kutoka https://distrokid.com/mymusic/. Ukiwa kwenye ukurasa wa toleo, bofya "Hariri Mgawanyo".

    Katika ukurasa unaofuata, bofya "Ongeza mshirika" ili kuongeza anwani ya barua pepe ya mshirika ambaye ungependa kumwekea marejesho kwa wimbo wowote. Kisha, bofya "Ongeza marejesho" ili kuweka kiasi cha marejesho kwa mshirika huyo. Hakikisha pia unaweka kiwango cha asilimia ya Mgawanyo ili mshirika atumie mara tu kiwango cha marejesho kinapofikiwa.

    Mara tu kiasi na asilimia za marejesho zimewekwa, bofya "Pitia Mabadiliko," kisha upitie mabadiliko hayo. Ikiwa yote yako sawa, bofya "Hifadhi Mabadiliko".

    Tafadhali kumbuka kwamba hakuna mapato yatakayogawanywa kwa washirika wengine katika Mgawanyo hadi kiasi cha marejesho cha mshirika kitakapotimizwa.

    Go to article
  • Ununuzi wa Albamu Unashughulikiwaje Katika Mgawanyo?

    Mtu anaponunua albamu nzima (badala ya kununua au kutiririsha wimbo mmoja), tutakokotoa kiotomatiki uwiano wa mapato kwa asilimia za Mgawanyo kwa nyimbo za albamu hiyo.

    Kwa mfano, ikiwa albamu ina nyimbo 2, na unapaswa kulipwa 50% ya wimbo mmoja kupitia Mgawanyo, basi utapokea 25% ya mauzo kamili ya albamu.

    Ikiwa wewe ni mmiliki wa Mgawanyo, unaweza kuona maelezo haya kwa kuelekea kwenye ukurasa wa toleo, kubofya "Hariri Mgawanyo", kisha kubofya "Kagua Mabadiliko," na kusonga hadi chini ya ukurasa.

    Go to article
  • Barua Pepe ya Mgawanyo "Sio Sahihi"?

    Chunguza ili kuona kama kuna nafasi baada ya barua pepe. Huenda ipo!

    Tafadhali rekebisha na jaribu tena.

     

    sw_extra_space_split.png

    Go to article
  • Nilituma mwaliko wa Migawanyo, lakini haukukubaliwa. Je, ninaweza kuondoa hiyo barua pepe kutoka kwenye Mgawanyo wangu?
     

    Ndiyo!

    Kumwondoa mtu kutoka kwenye Mgawanyo, nenda "Onyesha Historia ya Mgawanyo" kwenye ukurasa wa toleo, kisha bofya "Machaguo" --> "Ondoa" kando ya barua pepe unayotaka kuondoa.

    Wakishaondolewa, mapato yoyote ambayo yalikuwa yamezuiliwa yataonekana kwenye Benki yako ndani ya saa 24-48.

    (Ikiwa bado unataka kugawanya mapato na wao, lakini wanahitaji kukumbushwa, bofya "Tuma tena" badala yake!)

    remove_splits.png

     

     

    Go to article
  • Artists for Change ni Nini?

    Artists for Change inawaruhusu wasanii kuchangia kiotomatiki asilimia ya mirabaha kwa mashirika ya hisani na kampeni.

    Wasanii wanachangia asilimia ya mirabaha yao kwa:

    Miracle Messages

    North Brooklyn Angels

    Slice Out Hunger

    Stop AAPI Hate

    Support + Feed

    Vouchers 4 Veggies

    Asian Americans Advancing Justice

    GroundUp Music Foundation

    NAACP Legal Defense Fund

    National Independent Venue Association

    Ni rahisi kuanza! Chagua shirika au kampeni ambayo ungependa kuunga mkono kutoka kwenye orodha iliyo hapo juu, au hapa, ili kupata maagizo ya Kuchangia Kiotomatiki. Utapokea barua pepe unayoweza kutumia kuingia katika DistroKid, bonyeza "Splits" na ongeza ili uanze kutoa asilimia yoyote unayopenda!

    Go to article