Jibu fupi, inatofautiana.
Kiwango cha malipo ambacho huduma za utiririshaji hutoa kiko nje ya uwezo wetu -- na hatuna uwezo wa kuvibadilisha viwango hivyo. Tunatuma tu kiasi kamili ambacho huduma hututumia. DistroKid imekuwa ikipitisha na daima itaendelea kupitisha 100% ya mapato ambayo huduma hututumia kwa mitiririko/mauzo yako, ukitoa ada za benki/kodi zinazotumika. 💯
Kwa nini viwango vya malipo ya utiririshaji hutofautiana?
Kuna mambo mengi ambayo huduma hutumia kukokotoa unachodaiwa na viwango vya ukokotoaji hutofautiana kutoka huduma moja hadi nyingine. Baadhi ya vitu ambavyo huduma hutumia kukokotoa viwango ni pamoja na (lakini sio hivi tu):
-
wingi wa mitiririko/vipakuliwa
-
eneo
-
aina ya usajili (wa bila malipo vs usajili wa malipo)
-
mapato ya matangazo/usajili
Mbinu ya Malipo Kwa Uwiano
Maduka mengi husambaza kwa kutumia mbinu ya malipo kwa uwiano. Katika mtindo huu, mapato yote kutoka kwa kiwango cha bidhaa hukusanywa pamoja na % ya mapato hayo hutengwa pembeni kwa ajili ya wasanii. Mapato yaliyosalia kisha hugawanywa kwa nyimbo kulingana na sehemu yao ya jumla ya mitiririko ambayo iliyofanyika kwenye safu hiyo ya bidhaa.
Mfano (namba sio za kweli, kila huduma hutofautiana !!!!):
Huduma ina $1,000 za kusambaza kwa safu yao ya usajili unaolipiwa ambao umekusanya jumla ya mitiririko milioni 10 kwa mwezi. Kati ya jumla ya mitiririko milioni 10, wimbo wako ulitiririshwa mara 1,500.
-
1,500/10,000,000*$1,000= $0.15 inadaiwa
Spotify ina video nzuri inayoelezea jinsi ambavyo mapato yanakokotolewa kwa upande wao: Jinsi Spotify Inavyokulipa
Mauzo vs Mitiririsho
Kwa huduma zinazouza toleo lako kama vipakuliwa vya kidijitali kinyume na kutoa jukwaa la kutiririsha, ni kiwango cha kawaida cha tasnia kwamba hadi 30% ya kila mauzo inaenda kwenye huduma, huku 70% iliyosalia ikienda kwa msanii.
Sign Up