Inawezekana kabisa kudai wasifu wako wa Spotify for Artists kabla ya toleo lako la kwanza kabisa ukitumia jina la msanii ulilochagua. Ili kuhakikisha kuwa una muda wa kutosha wa kudai wasifu wako, hakikisha kuwa umepakia muziki wako angalau wiki nne kabla ya tarehe ya kutolewa.
Mara ukishapakia muziki wako kwenye DistroKid na unaweza kuona kwamba umefanikiwa kutumwa kwenye huduma, tutahitaji kutafuta URI yako ya Msanii wa Spotify. Habari njema! DistroKid ina zana kwa ajili hiyo!
Zana ya DistroKid ya Kuangalia Spotify
Ili kuangalia toleo lako litaunganishwa kwenye wasifu upi wa Msanii wa Spotify katika siku ya kutolewa kabla ya tarehe yako ya kutoa toleo husika, unaweza kuomba URI zako kupitia Zana ya DistroKid ya Kuangalia URI ya Spotify!
Kiangalizi cha URI ya Spotify https://distrokid.com/uri/spotify
Unapokuwa kwenye kiangalizi cha Spotify URI, chagua toleo lako kutoka kwenye menyu kunjuzi. Nina toleo moja pekee kwenye akaunti hii, na kwa hivyo tayari limechaguliwa. Kumbuka kwamba ikiwa huoni toleo, basi kuna uwezekano huenda bado hatujaliwasilisha toleo lako kwa Spotify, tafadhali angalia tena kesho!
Baada ya kuwa umechagua toleo lako, endelea na bofya kitufe cha "Spotify URI ni nini". Ikiwa toleo lako tayari limeshachukuliwa na Spotify, unapaswa kuona albamu yako, wimbo na URI za msanii
Ikiwa una wasanii wengi kwenye toleo lako ambao unajaribu kudai wasifu kwa jili yao, ondoa shaka! Wasifu wote wa wasanii na majukumu yao utaorodheshwa chini ya sehemu ya "Msanii:". Iangalie!
Endapo toleo lako bado halijachukuliwa na Spotify, kuna uwezekano utakutana na skrini hii:
Ondoa shaka! Kwa ujumla huchukua siku moja au zaidi kwa Spotify kuyachukua matoleo. Maelezo ya URI yako yatapatikana siku inayofuata au zaidi!
Kama hivyo ndivyo, angalia tena siku chache zijazo. Spotify itakuwa imeliingiza toleo lako na litapatikana kwa maombi ya URI kwenye ukurasa huu.
Nina URI yangu ya Msanii wa Spotify... sasa nifanye nini?
Sign Up