Kulingana na namna unayofikia Spotify, unaweza kupata mistari uliyowasilisha katika maeneo tofauti ya kiolesura chao cha kucheza sauti.
Tazama makala ya Spotify ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu kuona mistari hapa: https://support.spotify.com/ke-sw/article/lyrics.
Programu ya Spotify ya simu
Hii ndiyo jinsi unavyoweza kupata mistari yako kwenye programu ya simu ya Spotify:
- Gusa upau wa Inayocheza sasa chini kwenye skrini.
- Teremka chini kwenye "Mistari ya nyimbo".
- Bofya mistari ili uzione kwenye skrini nzima.
Programu ya Spotify ya Kompyuta
Katika programu ya kompyuta ya Spotify, unaweza kuona mistari yako kwa kubofya ikoni ya maikrofoni wakati wimbo unacheza.
Programu ya Spotify ya TV
- Fungua "Mwonekano wa Inayocheza Sasa" kwenye wimbo.
- Nenda hadi na uchague kitufe cha "Mistari" ili kuwezesha mistari.
- Baada ya kuwezeshwa, utaaona mistari katika Mwonekano wa "Inayocheza Sasa".
Sign Up